*Chelsea wawataka Koke, Lambert

*Mclaren akataa ofa ya Newcastle

 

Mabingwa wapya wa England, Chelsea, wamepanga kulipa pauni milioni 30 kwa Atletico Madrid ili wampate kiungo Koke, 23, na juu ya hapo wawape beki wao, Filipe Luis, 29, katika dili la kusisimua.

 

Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho, anamtaka kwa udi na uvumba Koke anayetoka Hispania, ambapo akiingia Stamford Bridge ataungana na mwenzake, Diego Costa, ambaye ni Mhispania na pia katoka Atletico.

 

Mourinho pia anaweka mipango chini chini ili kumnunua mshambuliaji wa Liverpool, Rickie Lambert, 33, ili achukue nafasi ya Didier Drogba, 37, atakapoondoka Stamford Bridge.

 

Winga wa Manchester United, Ashley Young, 29, anatarajiwa kupewa mkataba mpya Old Trafford, baada ya kocha Louis van Gaal kumkubali kutokana na kubadilika kwake ndani na nje ya dimba.

 

Southampton wanataka kumsajili kiungo raia wa Slovakia, Ondrej Duda, 20, kutoka Legia Warsaw kwani wanaamini kwamba kiungo wao mahiri, Morgan Schneiderlin, 25, ataondoka na kujiunga na ama Arsenal au Tottenham.

 

Manchester United wana hofu kwamba Borussia Dortmund watawawekea kigingi kumpata Mats Hummels, 26, kutokana na mchezaji mwenzake, Ilkay Gundogan kuamua kuondoka kwenye klabu hiyo ya Bundesliga kiangazi hiki.

 

Sunderland wanatarajia kuwasiliana na Manchester City kwa ajili ya kumsajili beki Micah Richards, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo Fiorentina.

 

Kipa wa Stoke, Asmir Begovic, mmoja wa makipa wazuri, anaonesha dalili za kutaka kuondoka klabuni hapo baada ya kutupwa benchi kwenye mechi ya Jumamosi iliyopita, ambapo walipoteza dhidi ya Swansea. Liverpool wanaaminika kuwa na nia ya kumsajili ili kumpa changamoto kipa wa sasa, Simon Mignolet.

 

Kocha wa Derby wanaocheza Ligi Daraja la Pili, Steve McClaren amekataa ofa ya  kwenda kuwa kocha wa Newcastle kwa michezo miattu ya mwisho wa Ligi Kuu ya England, huku Magpies wakiwa hatarini kushuka daraja iwapo wataendelea kufungwa na walio chini yao wakashinda.

 

Crystal Palace wametoa ofa ya pauni milioni 5.8 kwa Sampdoria kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wao, Eder, 28, huku Stoke na Southampton wakimtaka mchezaji mwingine wa klabu hiyo, Stefano Okaka, 25.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

VPL KUENDELEA

Juventus wawaduwaza Real Madrid