in , , ,

Sterling hawataki Liverpool


*James Milner na Sinclair kuwakataa City
*Man U wazidiwa, wataka £29M kwa De Gea

Mshambuliaji kinda wa Liverpool, Raheem Sterling amemwambia kocha wao, Brendan Rodgers kwamba anataka kuondoka.

Sterling alizungumza na Rodgers majuzi lakini amekubali kuketi tena chini Ijumaa ijayo na Ofisa Mtendaji Mkuu, Ian Ayre na Kocha Brendan Rodgers.

Mpachika mabao huyu wa England tayari amekataa ofa ya mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki na kusema anataka kwenda kwenye timu inayotwaa makombe.

Klabu wamekataa kuzungumzia suala la mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 20 lakini inaelezwa kwamba wanataka kumsajili Edin Dzeko wa Manchester City ili kujiimarisha kwani Daniel Sturridge ana matatizo ya kuumia mara kwa mara.

Liverpool wanatarajia kuanza msimu ujao na mshambuliaji mwenye asili ya Kenya na raia wa Ubelgiji, Divoc Origi, akitarajiwa kucheza vyema na raia huyo wa Bosnia Herzegovina.

Manchester City wanataka kumsajili Sterling, lakini Arsenal nao wanadaiwa kumhitaji, lakini Kocha Arsene Wenger amekataa kukiri au kukanusha kuhusishwa naye.

Inaelezwa kwamba ikiwa watalazimika kumuuza, watadai pauni kati ya milioni 30 na 35.

Kwa sasa Sterling analipwa £35,000 kwa wiki na msimu ujao wanatarajiwa kufuzu kwa Ligi ya Europa lakini Sterling na Liverpool wenyewe wangependa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL).

Manchester United wamewataka Real Madrid kuwalipa pauni milioni 29 ili kumpata kipa wao, David De Gea wakati Wahispania hao wakijiandaa kumtoa Fabio Coentrao.

Man U wamejitahidi kuhakikisha kipa wao anabaki, lakini habari mpya ni kwamba De Gea ameshakubaliana maslahi binafsi na Real na sasa kinachosubiriwa ni klabu mbili hizi kuzungumza.

United wanadaiwa kupanga kumpatia mshahara mkubwa De Gea hivyo kwamba katika mwisho wa mkataba mpya wa miaka minne ambao wangempa angekuwa analamba pauni 250,000 kwa wiki lakini haoneshi kukubali.

Kiungo wa Manchester City, James Milner, 29, anadaiwa kukataa ofa mpya ya mshahara wa pauni 165,000 kwa wiki kiangazi hiki mkataba wake unapomalizika, hivyo kuacha njia iwe nyeupe kwa ama Arsenal au Liverpool.

Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal amesema kwamba kipa wao, David De Gea ana wakati mgumu wa kufanya uamuzi wa ama kubaki au kuhamia nyumbani kwao Madrid ili kujiunga na Real Madrid.

Mshambuliaji wa Manchester City, Scott Sinclair, 26, anataka kubadili mkopo wake Aston Villa uwe usajili wa kudumu, kwani anataka kupata muda wa kutosha wa kucheza msimu ujao.

Kocha wa Real Sociedad, David Moyes aliyefurushwa Manchester United anataka kumsajili beki wa kushoto wa klabu yake nyingine ya zamani ya Everton, Bryan Oviedo, 25 ili kuimarisha kikosi chake.

Mchezaji wa Arsenal, Theo Walcott, 26, anatarajia kukutana na kocha wake Wenger kuzungumzia hatima ya usajili wake baada ya fainali ya Kombe la FA Mei 30.

Mpachika mabao wa Tottenham Hotspur, Harry Kane anaweza kukosa mechi za mwanzo za Ligi Kuu ya England msimu ujao iwapo ataitwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Vijana (U-21) ya England, anasema kocha wao, Mauricio Pochettino.

Beki wa pembeni wa Manchester United, Luke Shaw anatarajiwa kubeza matakwa ya kocha wake kwa kutaka kujiunga na kikosi cha timu hiyo ya taifa, bila kujali jinsi anavyoumia mara kwa mara.
Hatima ya Kocha wa West Ham, Sam Allardyce inatarajiwa kujulikana ndani ya saa 24 baada ya mechi yao ya mwisho dhidi ya Newcastle.

Liverpool wameanza kmjaribu kipa mwenye umri wa miaka 18 kutoka klabu ya Torquay United, Daniel Lavercombe.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Chelsea watandikwa 3-0

STARS KUWAVAA MADAGASCAR LEO