Jioni ya kesho Taifa Stars itapambana na Nigeria kwenye mchezo wa Kundi G wa michuano ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2017. Stars inaburuza mkia kwenye kundi hili baada ya kupokea kipigo cha 3-0 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Misri kule Alexandria mwezi Juni.

Kikosi cha Nigeria chini ya kocha mzalendo Sunday Oliseh kinakuja kikiwa na nyota takriban 15 wanaochezea klabu za Ulaya. Kati ya nyota wote wanaotarajiwa kuanza kwa upande wa Nigeria hapo kesho, kijana Ahmed Musa amekuwa gumzo miongoni mwa wadau wa soka na baadhi ya wanahabari.

Kijana huyu wa CSKA Moscow anakumbukwa zaidi kwa mabao mawili aliyowafunga Argentina kwenye mchezo wa michuano ya Kombe la Dunia 2014 kule Brazil. Wengi wanajiuliza kuwa kama aliweza kuwafunga Argentina mabao mawili wakiwa na walinzi kama Federico Fernandez na Ezequiel Garay sisi atatufanya nini hapo kesho?!

Maneno wanayoyaongea baadhi ya wachambuzi na wadau wa soka hapa nyumbani kwenye vyombo vya habari na mitandao kuhusu Musa yanaweza kuwa na faida kwa kuwa yatawafanya walinzi wetu kumuangalia winga huyo kwa umakini. Hata hivyo huenda yakawa na hasara mbili zifuatazo.

Kwanza walinzi wetu watajenga hofu juu ya mchezaji huyo na hili litapelekea kumkaba kiuwoga ama kumchezea madhambi na kuigharimu timu. Na hasara nying

Kikosi cha Nigeria chini ya kocha mzalendo Sunday Oliseh kinakuja kikiwa na nyota wake wengi wanaocheza soka ulaya.
Kikosi cha Nigeria chini ya kocha mzalendo Sunday Oliseh kinakuja kikiwa na nyota wake wengi wanaocheza soka Ulaya.

ine ni kwamba wachezaji wengine hatari kama Emmanuel Emenike wanaweza kuonekana wa kawaida na kutoangaliwa vizuri na hatimaye wakatudhuru.

Walinzi wetu wanapaswa kufuata maelekezo ya mwalimu Mkwasa pekee hapo kesho na waachane na maneno mengine yanayoongelewa kuhusu Ahmed Musa. Ila ni lazima wakumbuke kuwa wanatakiwa kujiepusha kumchezea madhambi Musa na wenzie hapo kesho ili tusiadhibiwe kwa mkwaju wa penati ama na kupunguzwa uwanjani.

 

Pia walinzi wetu wakumbuke kuwa kuna Emmanuel Emenike, Gbolahan Salami na wachezaji wengine tishio. Emenike anakipiga katika klabu ya Al-Ain ya Uarabuni kwa mkopo akitokea Fenerbahce ya Uturuki. Kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2013 ndiye aliyekuwa mfungaji bora.

Gbolahan Salami ni nyota anayechezea Warri Wolves ya Nigeria. Kwenye mchezo wa kwanza wa kundi hili ambao Nigeria walicheza dhidi ya Chad na kushinda 2-0 huyu jamaa alikuwa mchezaji pekee wa Nigeria aliyeanzishwa kati ya wachezaji wanaocheza nyumbani kwao Nigeria.

Salami alionyesha kiwango cha juu mno kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Chad. Pengine ndiye alikuwa nyota wa mchezo huo. Hivyo kama ataanzishwa na mwalimu Oliseh naye pia anahitaji uangalizi wa kutosha.

Hivyo ni wazi kuwa ingawa Ahmed Musa ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa uwanjani hasa kwenye swala la kukokota mpira bado kuna wengine ambao pia ni tishio kwenye kikosi cha Nigeria. Nafikiri kila mshambuliaji atakayeanza kwenye kikosi cha Nigeria kwenye mchezo wa kesho anahitaji uangalizi.

Walinzi wetu na wachezaji wa nafasi nyingine wanatakiwa kuhakikisha kuwa haturuhusu bao lolote kwenye mchezo wa kesho. Hili linawezekana ikiwa watafuata kwa umakini maelekezo ya mwalimu Charles Boniface Mkwasa na kupigana kwenye dakika zote za mchezo.

Uamuzi juu ya aina gani ya mkakati wa ukabaji utumike hapo kesho ni uamuzi wa mwalimu Mkwasa pekee na benchi lake la ufundi. Hatujui amepanga kutumia mkakati wa kukaba mtu kwa mtu ama kukaba kieneo ama vinginevyo. Ila tu nikumbushe Mussa si adui pekee hapo kesho.

Report

Written by Kassim

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

England usajili wa tsunami

Tanzania Sports

Ujerumani wawapopoa Poland