Baada ya ligi kuu Tanzania Bara kurejea Juni 13, Yanga, Simba na Azam zote ziliingia uwanjani na matokeo yao tunayo.
Yanga ilikuwa ya kwanza kucheza ambapo ilipata ushindi wa goli 1-0 dhidi Mwadui FC mchezo uliofanyika mkoani Shinyanga .
Matokeo ya mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC wengi walijua kabisa Yanga ingepoteza katika mchezo huo baada ya kubamizwa magoli 3-0 dhidi ya KMC lakini stori ikawa tofuati wakaibuka na ushindi.
Kuna wakati unaweza ukasema kuwa utofauti wa timu kubwa na ndogo unaonekana mchezoni, walichokifanya Yanga ndio ‘Reaction’ ya timu kubwa inakuwa iliandaliwa vyema sana, iliandaliwa sana kimawazo na kiakili.
Kocha alikuja na mbinu bora kwenye kutumia mfumo wa kuwaweka wachezaji wanne nyuma, mmoja kati wanne mbele na mmoja katika sehemu ya ushambuliaji.
Lamine Moro huenda ndiye alikuwa mchezaji bora wa mechi hiyo kwa kuwa na utimamu wa mwili pamoja na ubora ambao kila mmoja aliuona huku Haruna Niyonzima naye akicheza vizuri.
Kituko zaidi bado kipo kwa mshambuliaji wao Yikpe sijui kama anakuwa anawaza nini ndani ya uwanja, hakuna kinachoendelea ndani yake na huenda akaishia njiani msimu ujao.
Hatimaye Yanga wanaongeza alama tatu na kufikia 54 japo haikuwa katika ubora ule ambao tumeuzoea kuuona huenda Korona imeharibu utaratibu wao wa kila siku.
Katika mchezo mwingine timu ya Simba nayo ilionekana kuzama kwa kulazimishwa sare ya goli 1-1 huku kocha wa Ruvu Shooting Salum Mayanga alikuja na mbinu mbadala ambayo iliweza kufanya kazi.
Huenda mchawi wa Simba siku ile ni Fullyzulu Maganga ameweza kuwachambua vizuri mabeki wa Simba na kutengeneza umiliki wake.
Sehemu ya kiungo ya Simba kitaalamu ilifeli kutokana na watu waliopangwa hawakuwa katika ubora huo, wengi wanafahamu Jonas Mkude ndiye nyota pekee anayeweza kuhimili vishindo siku hiyo hakuwepo.
Huwezi kumlaumu Mzamiru Yassin kwani hakucheza kwa muda mrefu hivyo alipopata nafasi kwa mechi kama ile lazima apwaye kila mmoja anafahamu uwezo wa nyota huyo.
Japo ya kudorola kwa wachezaji wa Simba haukumuathiri nyota wao Luis Miquissone alionesha kiwango kikubwa na ile programu aliyopewa na kocha kipindi cha’Lockdown’ ilifanya kazi kubwa.
Utofauti wa Mohamed Hussein na Gadiel Michael unaonekana wazi hii sio ajabu kwani hata Ulaya ipo hiyo kuwa kama kocha unahitaji timu ishambulie basi kuna aina yake ya mchezaji.
Kama Simba wakihitaji kushambulia na kugawa maji sana basi Mohamed Hussein yupo ila kama inahitaji kuzuia sana basi Gadiel mpe nafasi.
Safu ya ulinzi wa Simba imeonekana kusinzia sana kwani goli la kusawzisha la Mwadui ni uzembe wa mabeki pamoja na golikipa Aishi Manula.
Simba wanakosa ‘Clean sheet’ kwa uzembe wa safu ya ushambuliaji wanatakiwa wakae na waangalie.
Simba na Yanga kuna vitu vingi vinatakiwa vibadilishwe haraka hasa Simba licha ya kuwa na wachezaji bora wanatakiwa waangalie namna ya kumaliza mechi zao.
Endapo watapoteza hata michezo miwili watavurugwa sana japo siamini kama watakosa ubingwa.
Yanga waangalie muunganiko wa timu wasicheze kwa ubora wa mmoja mmoja huenda wakarudi vizuri.
Jumatano Yanga watacheza na JKT Tanzania kazi kubwa itakuwepo kwani hizi timu za majeshi zinaonekana zina mazoezi makubwa.
Kocha wa Simba Sven Vanderbroeck anatakiwa ajitathimini haraka kabla ya uchukuaji wa hatua.
Azam FC nayo imefanya yake kwani imeitandika Mbao FC kwa jumla ya magoli 2-0 japo mchezo ulikuwa mkali wa aina yake imecheza kwa kiwango cha saizi japo haikuwa katika kiwango ch juu kama tulivyozoea.
Azam FC imeonesha utofauti kidogo wa miamba mitatu iliyopo katika zile tatu bora yaani Simba,Yanga na Azam yenyewe imekuwa katika kiwango cha wastani ila chenye ubora wake.
Kwingineko ligi imerejea ukweli ni kwamba mechi bora ya wiki iliyopita Coastal Union dhidi ya Namungo FC ambapo mchezo huo uliisha kwa magoli 2-2 , Coastal Union imerudisha goli kwa muda mchache huku ikigonga pasi nyingi sana na mpira wa kuvutia.
Ni kweli ligi imerudi viwango vya timu mbalimbali vinaonekana viko katika ubora wake licha ya kukaa nje ya uwanja kwa kitambo kidogo.
Comments
Loading…