in

LoveLove SurprisedSurprised

Aubamayang ni tofauti kabisa na Van Persie..

RVP, Aubayang

Arsenal moja ya timu inayopitia wakati mgumu hasa kuwabakisha mastaa wao wakati wa dirisha la usajili linapojongea.

Leo sitaki kupiga porojo sana nakupa ‘fact’ tu, leo hii tuangalie utofauti wa Pierre-emerick Aubameyang na Robin van Persie.

Huenda shabiki wa Arsenal anaweza kumuita jina lolote huyu mchezaji Robin Van Persie kwa ambacho kilichotokea msimu wa 2012/13.

Katika vitu vyote hivyo nyota hawa wanafana, vitu viwili tu ila hata kama Aubameyang akiamua kuondoka hatokuwa kama Van Persie.

Tuanzie hapa sasa, Aubameyang  amebakisha msimu mmoja tu mkataba wake kuisha ambao aliusaini mwaka 2018, huku Van Persie naye alibakiwa na msimu mmoja wakati anaondoka Arsenal.

Sehemu ya pili wote walikuwa wanafunga magoli muhimu ya timu hiyo huku wakiwa na wastani mzuri wa kila mechi na kuchukua kiatu bora cha dhahabu ‘Golden boot’.

Lakini kama Auba ataondoka Arsenal hatochukiwa kama alivyoondoka Van Persie.

Unauliza kwanini wakati huo, wote wana umuhimu mkubwa katika kikosi hasa ukiingia kwa upande wa kufunga magoli.

Iko hivi, Robin Van Persie alitumia miaka minane (8) Arsenal, alisajiliwa mwaka 2004 akitokea Feyenoord ya Uholanzi.

Katika misimu yote hiyo ameitumikia Arsenal kwa ufasaha kabisa ni miaka 2, miaka mingine yote alisumbuliwa na majeraha lakini Arsene Wenger hakuweza kumchoka na akaendelea kumpa nafasi hadi kuwa ‘Brand’ kubwa ya ufungaji wa magoli duniani.

Tanzania Sports
Mwaka wa kumalizika kwa mikataba kwa wachezaji wa Arsenal

Tena wakati anaondoka ni wakati ambao Wenger na Arsenal yake walikuwa wanamuhitaji sana ili aweze kuisaidia timu, baada ya kukaa sawa na kupona kabisa majeraha yake.

Van Persie amesepa tena mechi ya kwanza amefunga Arsenal hajashangilia ila ya pili ameshangilia na kuvua jezi kurusha angani kwa furaha hii chuki imeanza hapo pia haya twende chini  endelea kusoma.

Sehemu alipoenda ni mahasimu wakubwa wa Arsenal, hapa nieleweke kidogo, kipindi cha Wenger na Ferguson timu zao zilikuwa na ushindani mkubwa, licha yakuwa mahasimu wakubwa wa Manchester United ni Liverepool.

Ukitaka kujua kama walikuwa mahasimu wakubwa 1996 hadi 2012 hakuna timu nyigine yoyote iliyochukuaa EPL zaidi ya Arsenal na Manchester United.

Arsenal ilichukua kwa miaka 3, yaani 1998, 2001 na ‘Unbeaten’ 2003 na zilizobaki kachukua Man u kwanini nisiwaite mahasimu, unakumbuka ‘Battle’ la Roy Keane, Patrick Vieira?

Wakati huo ‘derby’ ya Man U ni Manchester City, huku Arsenal ‘Derby’ yao ni Tottenham Spurs.

Narudia tena nieleweke kuwa wakati Persie anaondoka alihitajika zaidi kuliko kipindi cha Auba, kwani Wenger alimpa njia na kumuamini na ndio maana ‘legend’ wa Arsenal wanaona kama kuondoka kwake ni aina fulani ya usaliti katika timu hiyo iliyopo jijini London, England. 

Kwa upande wa Aubameyang iko tofauti sana na hapa inatakiwa nieleweke pia kuwa Auba amesajiliwa akiwa na miaka 28 ndio kwanza anamaliza misimu yake miwili.

Mashabiki wengi walitegemea nyota huyo angefunga magoli na kweli kitendo hiko kimetokea anacheka na nyavu kila kukicha. 

Ameshinda mfungaji bora kwa msimu wake wa kwanza akigawana na Mohamed Salah na Sadio Mane tena msimu wake wa awali huenda akafanya hivyo msimu huu tena.

Kama ataondoka sio tatizo lake bali ni uchovu wa bodi ya Arsenal kuweka ulinzi mkali kwa nyota huyo yaani kumpa mkataba mzuri ambao ungefanya timu hiyo kuwa na uhakika angalau hata miaka mitano kuwa na nyota huyo baada ya kuonesha makali yake kama aliyokuwa nayo wakati anatoka Ujerumani.

Hapa sasa Auba anaweza kuchagua aongee vizuri na uongozi wa washika mitutu asiondoke ili aimbwe wimbo mzuri na mashabiki wa Arsenal.

Anaweza kujiuliza anataka kuwekwa katika ukurasa mmoja wa marejendari wa timu hiyo au anatakaje? 

Endapo atabaki tena hata kwa misimu mitatu au miwili ndani ya Arsenal atawekwa katika vitabu vya wachezaji muhimu ndani yake huku akisemwa vizuri kwa miaka yake sita, pengine kufunga kwake pia kukamuongezea mahaba ya dhati kabisa kwa wapenzi wa timu hiyo.

Lakini kwa upande mwingine ameenda kucheza mpira Ulaya kwa lengo moja tu apate pesa na kama atasaini dili msimu huu itakuwa dili lake la mwisho kubwa akikosea tu akifuata mahaba ya mashabiki pesa nzuri hapati atafanyaje? 

Hayo yote tumuachie Aubameyang kwani hatupo katika moyo wake hadi sasa anajua yeye  anachotaka.

Jibu kamili tutalipata wakati Arsenal wakikaa na Auba kumpa dili lao maana hadi sasa siamini kama wamekaa kwani wangekaa tungejua tu kuwa anabaki au habaki.

Na kama akitaka kuondoka ungesikia anauzwa maana msimu ujao ataenda bure kabisa.

Wenger moja ya makocha walioweka alama kubwa sana na ataweza kukumbukwa ikiwa usajili wake wa kwanza mwaka 1997-/98 alisajili nyota aliyekuwa na uwezo mzuri wa kufunga magoli Nicolas Anelka aliondoka huku akiandikwa katika magazeti akiwa na sura mbili, na usajili wake wa mwisho ulikuwa mwaka 2018 Pierre-Emerick Aubameyang ‘That is Professor’.

Lakini kwanini siku zote Arsenal ina kwama, katika kuwawekea kinga nyota wake ili wasiondoke kirahisi kama ilivyo sasa kwanini wasiwe na utaratibu mzuri wanafanya kama mpira wa Tanzania wakati wapo duniani huko.

Wakati namalizia niwarudishe nyuma mwaka 2017 Van Persie aliwahi kusema kuwa aliwapa vipengele saba Arsenal ili waingie mkataba mpya lakini hawakuweza kumpa hata huo mkataba, swali la kujiuliza ni  kweli watu waliokuhudumu kwa miaka 8 tena ukiwa majeruhi unakuja kukaaa vizuri watakuacha kweli?

Siwaingilii wapenzi wa Arsenal ila wana haki ya kumchukia.

Usajili pekee ambao ‘Gunners’ wanaufurahia ule wa Alexis Sanchez baada ya kulinga na kutaka kuondoka huko alikoenda nako amekuta majanga hadi leo anatapatapa.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

76 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
VPL

Simba,Yanga na Azam, mdogo mdogo

Mbwana Samatta

Samatta atafanya vizuri sana- Shahanga