*Yanga waja na mbinu mbadala

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC wameshindwa kupata heshima waliyokuwa wakiitafuta mkoani Kagera baada ya kulazimishwa sare.

Simba walikwenda sare ya 1-1 na Kagera Sugar kwenye dimba la Kaitaba, ambapo Simba walikuwa wamedhamiria kushinda mechi zote zilizobaki kwa ajili ya kulinda heshima yake, hata kama suala la ubingwa limewaponyoka.

Simba walichomoza vyema kuliko wenzao na alikuwa Zahoro Pazi aliyefunga bao la kwanza dakika ya 45 na kuamsha hoi hoi kote Tanzania, wala si Kaitaba tu.

Hata hivyo ngebe hizo zilikatika dakika ya 51 pale Kagera walipofanikisha kurudisha bao hilo kupitia kwa Themi Felix kunako dakika ya 51.

Kama Simba hawatagangamala zaidi kwenye mechi zijazo, wanaweza kuja kupitwa hata na Kagera au Ruvu kulingana na matokeo yao yajayo, kwani sasa Simba wapo nafasi ya nne kwa kufikisha pointi 37.

Wangependa walau kupata nafasi ya tatu ili wasomeke vyema kwenye ramani ya Afrika na dunia kwa ujumla.

Katika mechi nyingine, Mbeya City walibanwa na vijana wa Ashanti wanaonolewa na King Abdallah Kibaden kwa kwenda suluhu na kufikisha pointi 46 sawa na Yanga.

Mbeya hawakuamini kwamba wameshindwa kuwafunga Ashanti ambao walitokea kuwa kama gunia la mazoezi kitambo kidogo, na hivyo kujinyima nafasi ya kuwaengua Simba.

Nguvu ya Mbeya City waliyoanza nayo mwanzo wa msimu inaelekea kupungua kwa kadiri mechi zinavyokwenda, na kocha Juma Mwambusi atatakiwa kujiuliza tatizo ni lipi, ikiwa ni stamina au mengine nje ya dimba.

Kana kwamba hiyo haitoshi, Mbeya City wana Amsha Amsha wanafikisha pointi za Yanga huku wakiwa wamecheza mechi mbili zaidi ya Yanga, hivyo mabingwa hao watetezi hawana hofu sana.

Yanga ambao wanacheza Jumapili hii dhidi ya Ruvu, wametumia mbinu nyingine inayoweza kuwasaidia kupata pointi zaidi ya vinara wa ligi Azam.

Yanga wamewasilisha rufaa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakidai kwamba mchezaji Mohamed Neto wa Mgambo Shooting Stars aliyeshiriki pambano ambalo Yanga walilala kwa 2-1 si raia na hana hati ya uhamisho wa kimataifa.

Pamoja na TFF kudai ombi hilo lipo nje ya muda, wamelipeleka kwa kamati husika ili litazamwe, kufanyiwa kazi na kutolewa uamuzi. Azam wanaongoza ligi kwa pointi 53 lakini wana mechi moja zaidi ya Yanga.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Chelsea, Man U, Man City ushindi

Bayern ujanja wamalizika