Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara Simba SC imeshinda magoli 4-1 dhidi ya Yanga katika nusu fainali ya kombe la ‘Azam Sportas Federation Cup’ uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Katika mchezo huo nimepata kugundua mambo mengi hasa ubora wa timu ya Simba kwa kipindi cha miaka mitatu.
Ubora wao unaanza na kikosi kipana chenye wachezaji bora ndani ya timu hiyo inaweza ikawa sababu kubwa inayoipa utofauti na timu nyingine zinazo shiriki ligi kuu Tanzania Bara.
Mabadiliko ya Simba yameifanya timu iwe bora kutokana na kuwa na uhakika wa kupata mishahara kwa wakati pamoja na motisha nyingi ndani ya timu hiyo.
Ukweli ni kwamba kikosi cha kwanza cha timu hiyo hakina tofuati sana na kikosi cha pili kwa ubora hii inatokana na uchaguzi mzuri wa wachezaji.
Simba hii inaweza ikafanya kitu chochote uwanjani na kikawa kweli kama wakihitaji kufanya hivyo.
Labda tuangalie mchezaji mmoja mmoja badala ya mwingine katika kikosi cha kwanza.
Luis Miquissone, aliwahi kutakiwa na Yanga wakati anacheza UD Songo ya nchini Msumbiji, Simba waliingilia dili lake kati na kuipata huduma yake ni moja ya wachezaji wasumbufu sana kwa kasi yake na akili kuwa ‘sharp’ pale anapotaka kufanya maamuzi ndio sababu ya kuwa mchezaji bora ndani ya timu hiyo.
Miquissone ni hatari pamoja na machachari kwani anauwezo wa kuitwa wa kimataifa kwa ligi yetu ya bongo.
Clatous Chama, huyu ni mwamba wa Lusaka pale Zambia anacheza kiungo mshambuliaji kiwango chake hakina ubishi kuna wakati unaweza kujiuliza kwanini amekuja kucheza soka Tanzania.
Majibu anayo mwenyewe ni mchezaji hodari sana ubora wake kawazidi wachezaji wengi wa timu nyingine 19.
Gerson Fraga, Mbrazil aliyekuja huku akipewa majina mengi, yaani imefika hatua anaitwa raia kutoka India hata shabiki wa Simba kuna wakati walitaka aondoke kama alivyoondoka mwenzake.
Kwa sasa unapotaja eneo la kiungo huwezi kukosa kumtaja Fraga kwa mpira wa akili anaocheza.
Na amewekwa katika historia ya kuifunga Yanga ni miongoni mwa rekodi nzuri ni wachezaji wachache sana wanaweza kufunga katika timu hizi kubwa mbili.
Meddie Kagere, Mnyarwanda huyu huenda akawa mfungaji bora mara mbili mfululizo kwani tayari amefunga magoli 19 ikiwa msimu uliopita alifunga magoli 20 ni tegemeo la Simba na anauwezo mzuri huenda kawazidi washambuliaji wengine wa timu nyingine.
John Bocco, mzawa ambaye amecheza miaka 12 mfululizo katika kiwango bora zaidi ni mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi kwa ligi kuu Bara.
Kiwango cha Bocco na heshima aliyojizolea huenda akahesabiwa mshambuliaji bora Tanzania wa muda wote japo kutakuwa na maswali mengi kwa wachezaji wa zamani.
Aishi Manula, wengi wanabishana kuwa ndiye ‘Tanzania one’ lakini ubora wake unajidhihirisha pale anapokaa langoni amepata ‘Clean Sheet’ zaidi ya 15 kwa misimu miwili mfululizo.
Manula anabaki kuwa bora kwa kipindi hiki bado anacheza kwa kiwango kikubwa naye miongoni mwa wachezaji waliopo Simba na wanatengeneza ulinzi mzuri.
Erasto Nyoni, beki kisiki aliyekuwa na akili nyingi, aliwahi kumpiga chenga tamu sana Mohamed Salah wa Liverpool wakati wakiwa katika timu zao za taifa.
Amecheza kwa muda mrefu na kiwango bora anadhihirisha kuwa muhimu ndani ya kikosi hiko.
Shomari Kapombe, beki bora upande wa kulia nchini Tanzania kama akicheza msimu mzima bila kuwa majeruhi anakupa huduma safi kabisa ambayo unaweza kuifurahia.
Kama isingekuwa majeraha yake basi angekuwa mchezaji mwingine kabisa.
Fransic Kahata Mkenya anayesaga vizuri katika mpira wa bongo, kusaga maana yake kucheza vizuri.
Jonas Mkude, Kiungo mkabaji ndiye aliyechukua makombe manne ya ligi kuu Tanzania Bara akiwa na Simba, yaani yeye ndiye aliyechukua mara nyingi zaidi baina ya wachezaji wa Simba.
Kiwango chake kizuri mno hana mambo mengi anacheza kwa tahadhari na akili kubwa.
Mohamed Hussein, beki wa kushoto akiwa na kiwango bora kabisa na anauwezo wa kupanda na kushuka.
Katika ile 11 bora tuna maliza na Pascal Wawa yeye anakaa kama namba tano angalia viwango vyao kisha njoo kwa timu nyingine.
Kama huamini angalia kikosi cha Simba kilichopo nje yaani kikosi cha pili.
Beno Kakolanya, Haruna Shamte, Gadiel Michael, Kenedy Wilson, Yusuph Mlipili, Said Ndemla, Deo Kanda, Sharaf Shiboub, Ibrahim Ajib, Miraji Athumani, Hassan Dilunga na Shiza Kichuya.
Sababu nyingine huenda yote hayo ya kupata matokeo mazuri yasingetokea kama kusingekuwepo na mabadiliko.
Baada ya Simba kuamua kubadilisha mfumo hisa nyingi amechukua mwanachama wa timu hiyo Mohamed Dewj basi ndio ikawa sababu ya haya tunayoyaona hivi sasa.
Fedha nyingi zinatumika kupata wachezaji bora huku wakiajiri, mtendaji mkuu aliye na weledi Senzo akifanya vitu tusivyozizoea vya kiweledi zaidi.
Comments
Loading…