*Toure awania kuvunja rekodi ya Eto’o

*Pia Gervinho, Enyeama, Serge Aurier

Mshambuliaji machachari wa Timu ya Taifa ya Tanzania – Taifa Stars na TP Mazembe, Mbwana Samatta ametajwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika.

Samatta aliyetamba sana karibuni na kupachika mabao muhimu kwa klabu hiyo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kwa timu ya taifa, pia ana ndoto za kucheza Ulaya.

Huyu ndiye mchezaji pekee wa Tanzania aliyewekwa kwenye orodha mbili – moja ikijumuisha Waafrika wanaocheza nje na nyingine ya wanaokipiga barani.

Katika kinyang’anyiro hicho ambacho atakayeibuka kidedea atatangazwa Desemba 22 mwaka huu, yumo pia Yaya Toure wa Manchester City.

Toure atakuwa anatafuta tuzo kwa mara ya tano, ambapo amekuwa pia nahodha wa Ivory Coast na mmoja wa viungo bora zaidi duniani. Aliwaongoza Tembo hao kutwaa ubingwa wa afrika nchini Guinea ya Ikweta Februari hii.

Katika historia ya tuzo hizo, Samuel Eto’o wa Cameroon anaongoza sambamba na Toure kwa kuitwaa mara nne.

Pamoja na Toure, wengine wanaoiwania ni wachezaji wenzake wa Ivory Coast, Gervinho, Max Gradel na Serge Aurier.

Wachezaji waliotajwa kuwania tuzo hiyo wanaocheza nje ya Afrika, majina ya klabu wanazochezea na timu za mataifa ni Ahmed Musa – CSKA Moscow na Nigeria, Andre Ayew – Swansea City na Ghana.

Wengine ni Aymen Abdennour – Valencia na Tunisia, Baghdad Bounedjah – Etoile du Sahel na Algeria, Bassem Morsi – Zamalek na Misri, Chrisitian Atsu – Bournemouth na Ghana.

Wamo pia Dieumerci Mbokani – Norwich City na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, El Arbi Soudani – Dynamo Zagreb na Algeria, Faouzi Ghoulam – Napoli na Algeria.

Orodha hiyo inao Ferebory Dore – Angers na Kongo, Ibrahima Traore – Borussia Monchengladbach na Guinea, Javier Balboa – Al Faisaly na Guinea ya Ikweta, Heldon Ramos – Rio Ave na Cape Verde, Mame Biram Diouf – Stoke City na Senegal, Mehdi Benatia – Bayern Munich na Morocco.

Nyota wengine wanaowania tuzo hiyo ni Mudather El Tahir ‘Careca’ – Al Hilal na Sudan, Mohamed Salah – Roma na Misri, Nicolas Nkoulou – Marseille na Cameroon, P-Emerick Aubameyang – B Dortmund na Gabon.

Advertisement
Advertisement

Golikipa Robert Kidiaba wa TP Mazembe na Kongo yumo sambamba na Rudy Gestede – Aston Villa na Benin, Riyad Mahrez – Leicester City na Algeria,

Sadio Mane – Southampton na Senegal, Seydou Keita – Roma na Mali na Sofiane Feghouli – Valencia na Algeria.

Wengine ni Stephane Mbia – Trabzonspor na Cameroon, Thievy Bifouma – Granada na Kongo,

Victor Wanyama – Southampton na Kenya, Vincent Aboubakar – Porto na Cameroon,

Vincent Enyeama – Lille na Nigeria, Yacine Brahimi – Porto na Algeria, Yannick Bolasie – Crystal Palace DR Kongo, Yasine Chikhaoui – Al Gharafa na Tunisia.

Kwa upande wa walio barani Afrika mbali na Samatta na Kidiaba ni Abdeladim Khadrouf – Moghreb Tetouan na Morocco, Abdelmalek Ziaya – Entente Setif na Algeria.

Pia wamo Ahmed Akaichi – Etoile du Sahel na Tunisia, A. Carolus – USM Algers na Madagascar,

Baghdd Bounedjah – Etoile du Sahel na Algeria,

Bakri El Madina – Al Merriekh na Sudan, Bassem Morsi – Zamalek na Misri.

Wengine ni Boris Moubhio – AC Leopards na Kongo, Djigui Diarra – Stade Malien na Mali, Felipe Ovono – Orlando Pirates na Guinea ya Ikweta, Sylvain Gbohouo – TP Mazembe na Ivory Coast, Hazem Emam – Zamalek na Misri.

Orodha inawataja pia Hocine Ragued – Esperance na Tunisia, Kermit Erasmus – Orlando Pirates na Afrika Kusini, Malick Evouna – Al Ahly na Gabon,

Mohamed Koffi – Zamalek na Burkina Faso na Mohamed Meftah – USM Algers na Algeria.

Wamo pia Mudather El Tahir ‘Careca’ – Al Hilal na Sudan, Oupa Manyisa – Orlando Pirates na Afrika Kusini, Roger Assale – TP Mazembe na Ivory Coast.

Orodha ya wawaniaji inafungwa na Thamsanqa Gabuza anayekipiga klabu ya Orlando Pirates na Afrika Kusini pamoja na Zein Edin Farahat wa USM Algers na Timu ya Taifa ya Algeria.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

JURGEN KLOPP HAWEZI TENDA MIUJIZA

Tanzania Sports

Hayatou ataimudu Fifa?