in , , ,

Sagna sasa rasmi Man City

Bacary Sagna

 

Hatimaye Mabingwa wa England wamekubaliana rasmi na Bacary Sagna wa Arsenal na kutiliana saini mkataba wa miaka mitatu.
Beki huyo wa kulia amesajili kama mchezaji huru baada ya Arsenal kuzembea kumpa mkataba mapema, ambapo walitaka asichukue zaidi ya mwaka mmoja, kwa madai ya umri wake kwenda.

 

Sagna (31) amekabidhiwa jezi ile ile namba tatu aliyokuwa akitumia Arsenal ambako amecheza kwa miaka saba na anakuwa ingizo jipya la kwanza kwa Kocha Manuel Pellegrini.

Jezi hiyo ilikuwa ikivaliwa na mlinzi wa zamani wa City, Mbrazili Maicon. Arsene Wenger alimnunua Sagna kwa pauni milioni saba kutoka Auxerre Julai 2007.

 

Sagna alicheza mechi 284 kwa klabu huyo ya London Kaskazini na amepata kupigiwa kura akaingia kwneye timu ya mwaka ya PFA katika Ligi Kuu.

Alicheza mechi yake ya mwisho katika fainali ya Kombe la FA dhidi ya Hull ambapo aliwasaidia Arsenal kutwaa kombe hilo baada ya ukame wa miaka tisa, ambapo walitoka nyuma 2-0 na kushinda 3-2.

 

Sagna ataungana na City baada ya majukumu yake Brazil ambako anacheza na Timu ya Taifa ya Ufaransa; ametoa salamu za kuaga kwa The Gunners.

Sagna anatarajiwa kuanza kuchezea City katika mechi za ziara nchini Marekani ambapo Julai 27 wataceza na AC Milan jijini Pittsburgh, Julai 30 watacheza na Liverpool jijini New York na Agosti 2 watakipiga na Wafaransa wenzake, Olympiakos huko Minneapolis.

 

Sagna kwenda rasmi City kunawatia kidonda au kuwatonesha washabiki wa Arsenal, kwa sababu ni mfululizo wa wachezaji wazuri wa Emirates kuondoka na kwenda kwa wapinzani wao.

Ni wiki hii tu Chelsea wamemsajili nahodha wao wa zamani, Cesc Fabregas ambaye walikuwa na fursa ya kumsajili kutoka Barcelona lakini wakuu wa Emirates wakakataa kutumia fursa hiyo.

 

Wengine walioondoka Arsenal na kung’ara kwenye klabu pinzani ni Samir Nasri, Gael Clichy, Kolo Toure waliokwenda City, Emmanuel Adebayor aliye Tottenham Hotspur sasa, Ashley Cole aliyekwenda Chelsea, Robin van Persie aliyekwenda Manchester United.

 

Sagna atapeleka ushindani kwa beki mwingine wa kulia Pablo Zabaleta. Hata hivyo, wanaweza wakacheza pamoja kwa sababu kuna wachezaji wanaotarajiwa kuondoka kama Joleon Lescott, Jack Rodwell na Scott Sinclair.

Kiungo wa Porto, Fernando (26) anatarajiwa kuongeza nguvu Etihad siku zijazo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Barcelona wamchana Fabregas

Klose kuvunja rekodi ya Ronaldo?