in

Klose kuvunja rekodi ya Ronaldo?

 

Ujerumani ni moja ya nchi chache zinazopewa nafasi ya kutwaa Kombe la Dunia mwaka huu.
Wana kikosi kilichosheheni vipaji vya vijana pamoja na wakongwe.

 

Mmoja wa wakongwe hao ni Miroslav Klose ambaye huenda ikawa michuano yake ya mwisho na anaweza kuweka historia kubwa sana.
Mjerumani huyu ana fursa ya kuvunja rekodi ya Ronaldo de Lima katika kufunga mabao. Hadi sasa Ronaldo anaongoza kwa kufunga mabao 15 huku Klose akiwa amefunga 14.

 

Gerd Muller wa Ujerumani naye amefunga mabao 14 lakini alishastaafu. Rekodi yake ilivunjwa na Ronaldo 2006 na inasimama hadi leo, hivyo Klose ndiye mwenye nafasi ya kuivunja.

Klose (36) ndiye mpachika mabao pekee kiasili wa Ujerumani katika kikosi cha Joachim Loew na alidhani kwamba 2010 ilikuwa mwisho wake kwa michuano hii kabla ya Loew kumwita tena kikosini.

 

Bundesliga inatawaliwa na viungo wa Kijerumani lakini washambuliaji wengi ni wa kigeni na Klose mwenyewe anachezea Lazio ya Italia.
Haya ni mashindano yake ya nne na akipewa nafasi anaweza katika mechi tatu za mwanzo akabadili historia.

 

Loew anachezesha viungo washambuliaji zaidi kwa sababu hana washambuliaji kiasili, na inadhihirika kwa jinsi anavyowatumia Thomas Mueller na Mario Goetze.

Wamempoteza Marco Reus aliyeumia na alikuwa kiungo mshambuliaji hatari ambapo alicheza walipowafunga Armenia 6-1 kwenye mechi ya mwisho ya kujipima nguvu.

 

Klose alifunga katika mechi hiyo, likiwa ni bao lake la 69 katika mechi 132 kwa taifa lake, akimzidi Mueller mwenye mabao 68.
Klose anahitaji bao moja tu kufikia rekodi ya Ronaldo na angeweza kumzidi ikiwa atafunga zaidi ya hapo.

 

Meneja wa Ujerumani, Oliver Bierhoff aliyekuwa mshambuliaji, anasema Ujerumani wana bahati mbaya kutokuwa na washambuliaji wa asili huku kizazi cha akina Klose kikikaribia ukingoni.

Kocha Msaidizi, Hansi Flick anasema anatarajia Klose aliyezaliwa Poland atapewa jukumu kubwa Brazil na atalitumikia vyema.
Alipoanza kuichezea Ujerumani 2002 katika Kombe la Dunia alifunga mabao matatu kwenye ushindi wa 7-1 dhidi ya Saudi Arabia.
Ujerumani wanafungua dimba Jumatatu hii kwa kucheza na Ureno.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Bacary Sagna

Sagna sasa rasmi Man City

Bendera ya Nigeria yakosewa