in , ,

SABABU ZA KWANINI LIVERPOOL WATASHINDA DHIDI YA CHELSEA.

Mwendelezo wa kupanda na kushuka wa viwango vya wachezaji wa Liverpool?

Kufungwa kwao katika michezo yao mitatu iliyopita katika uwanja wao wa
nyumbani ( Anfield ) na kushinda mechi moja tu kwenye michezo minane
iliyocheza mwezi January, inaweza ikawa sababu kubwa ya wao kushinda
mechi ya leo.

Kwanini nasema hivo?

Mpaka sasa Liverpool watakuwa wanatafuta kupandisha hali ya kwenye
timu yao, na hii itawafanya kuingia kwenye mchezo huu wakiwa na hali
kubwa ya kushinda ili kurejesha hali ya kujiamini katika kikosi.
Nafasi ya Countinho katika mchezo wa leo ikoje?

Ametoka katika majeraha hivi karibuni, ameanza kurejea katika hali
yake ya kawaida baada ya kupata match fitness.

Countinho ndiye mtu muhimu kwenye kikosi na mimi ndiye namtazama kama
mtu pekee ambaye anaweza kuibeba Liverpool kama akiwa kwenye kiwango
chake kizuri.

Madhaifu ya Liverpool yako wapi??

Urejeo wa Matip unaweza ukawa umepunguza madhaifu ya safu yao ya
ulinzi kwa kiasi kidogo, Combination ya Klavan na Lovren ilikuwa na
makosa mengi sana tangia waanze kucheza kwa pamoja.

Kuna vitu viwili ambavyo mabeki wa kati wa Liverpool wanavikosa sana.

Moja, wamekuwa Hawachezi vizuri mipira ya juu, inayopigwa kutokana na
krosi zinazokuja langoni mwao.

Pili, Mabeki wa Liverpool wamekuwa hawana kawaida ya kukaba man to
man ndiyo maana hata marking yao ni mbovu sana kwenye mechi
zilizopita.

Makosa Binafsi ya golikipa yanaweza kuwagharimu Liverpool?

Kati ya eneo ambalo limekuwa likiwagharimu sana Liverpool ni eneo
hili. Makipa wote wawili yani Mignolet na Loris Karius wamekuwa na
makosa mengi ya kibinafsi, na linaweza kuwagharimu kwenye mchezo wa
leo.

Mwendelezo wa kupanda na kushuka wa viwango vya wachezaji wa Liverpool?

Kumekuwa na mwendelezo wa kusuasua wa viwango vya wachezaji wa
Liverpool ,mfano mzuri ni Emre Can .Hii inaweza ikawagharimu
Liverpool , maana kama baadhi ya wachezaji watashindwa kulinda
mwendelezo wa viwango vyao vya mpira hii inamanisha katika mechi hii
watakuwa out of form .

Kipi wakifanye na je urejeo wa Mane Unaweza ukawa na faida kwao?

Aina yao ya uchezaji wa kushambulia kwa kasi ilikuwa inawasaidia sana
kwa namna zifuatazo.

Moja, unaposhambulia kwa kasi na nguvu unakuwa na uhakika wa
kutengeneza nafasi nyingi za magoli kutokana na presha unayotengeneza
kupitia kushambulia kwa kasi.

Pili, unaposhambulia kwa kasi hii inakupa faida kubwa ya wewe kuwa na
mpira muda wote, hivo unapokuwa na mpira muda wote unakuwa
unajihakikishia kuziba madhaifu ya maeneo mengine ya timu kama eneo la
ulinzi.

Ujio wa Mane, utakuwa na faida kubwa sana kwa Liverpool. Kwanini nasema hivo?

Tumeshuhudia mechi zilizopita ambavyo Liverpool wamekuwa wakipata
shida sana jinsi ya kuliziba pengo lake kwa kuwaweka watu ambao
hawakuwa na kasi na uwezo wa kulazimisha mashambulizi kama ilivyo kwa
Mane.

SABABU KWANINI CHELSEA WATAIFUNGA LIVERPOOL.

Chelsea

Mechi 19 zilizopita wameshinda mechi 18, mpaka sasa wakiwa na Clean
sheets 13 katika michezo 22 ya ligi kuu ambayo wameruhusu magoli 15
tu. Hii inaonesha wanaukuta mzuri wa ulinzi kuliko wa Liverpool ambao
umeruhusu magoli 27 katika mechi 22 za ligi kuu.

Safu bora ya ulinzi inaweza ikawa faida kwao?

Ndiyo, siku zote ukitaka kuchukua ubingwa au kushinda mechi kubwa
kama hizi unatakiwa uwe na kipa bora ambaye tayari wanaye, uwe na
walinzi bora ambao tayari wanao.

Yupi mchezaji anayeweza kuibeba Chelsea?

Nimemtaja Philipe Countinho kama mchezaji ambaye anaweza kuibeba
Liverpool kama akiwa katika kiwango kizuri.

Eden Hazard ndiye nampa nafasi ya kuibeba Chelsea kama atakuwa kwenye
kiwango chake kizuri.

Ubora wa Chelsea uko wapi?

Binafsi, ubora wa Chelsea nauona zaidi pembeni ambapo wanacheza kina
Marcos Alonso na Moses.

Hawa ndiyo wanaozalisha mashambulizi ya timu hii, hata flow nzima ya
timu hufanyika kupitia hapa.

Ukiwabana Moses na Alonso, unakuwa na uhakika wa kupunguza asilimia
kubwa ya mashambulizi ya timu ya Chelsea.

Lakini unawezaje kuwabana Moses na Alonso?

Kuna njia mbili za kuwabana Moses na Alonso.

Njia ya kwanza ambayo Liverpool wanatakiwa waitumie sana ni
kuhakikisha Matic na Kante hawatoi huduma kwa Alonso na Moses.

Matic na Kante kwa kiasi kikubwa ndiyo huwa wanasambaza mipira mingi
kwa hawa watu, hivyo kuwabana Matic na Kante inakuwa na maana kuwa
umebana kwa asilimia usambazaji wa mipira kwa kina Alonso na Matic.

Njia ya pili ya kuwazuia Alonso na Moses. Ni kuwafanya wasipande zaidi.

Sasa utawezaje kuwazuia wasipande zaidi?

Moja, kupitia washambuliaji wa pembeni wa Liverpool, washambuliaji wa
pembeni wa Liverpool wana kasi kubwa, hivo kasi yao itakuwa inawapa
hofu Moses na Alonso kupada mara kwa mara na kubaki nyuma wakiwalinda.

Pili, Mabeki wa pembeni wa Liverpool wanatakiwa wasipande kwa
asilimia kubwa mbele, wajihadhari sana na mashambulizi ya kushtukiza
ya kina Moses na Alonso.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

NILICHOKIONA KWENYE MECHI YA AZAM NA SIMBA

Tanzania Sports

Chelsea safi, Arsenal mh!