in , , ,

Rooney, RVP hawaelewani?


*Wapasiana mara sita tu mechi nzima

*Ndio tegemeo lililobaki kwa Moyes

Washambuliaji wawili nyota wa Manchester United, Wayne Rooney na Robin van Persie (RVP) wanaelekea kutofautiana.

Hawa ndio tegemeo lililobaki kwa Kocha David Moyes aliye matatani, lakini katika mechi ya Jumapili hii dhidi ya Fulham walicheza kama wageni, mechi ikaishia kwa sare ya 2-2.

Pengine kila mmoja anataka kuonekana zaidi, lakini athari inakuwa kwa timu, ambapo katika dakika zote 90 walipasiana mara sita tu.

Mbaya zaidi, ni kwamba mara mbili kati ya hizo sita ni pale walipokuwa wakianza mchezo wakati ukichanganya na Juan Mata walipata kuitwa utatu hatari kwa timu pinzani.

Hivi sasa United wamelala pointi tisa nyuma ya Liverpool wanaoshikilia nafasi ya nne huku shinikizo likizidi kwa Moyes anayeonekana kushindwa kujieneza kwenye viatu vya Sir Alex Ferguson aliyeng’atuka.

Rooney na RVP walionekana kama wenye kuonena haya uwanjani na inashangaza kwamba hawakupatiana mipira licha ya fursa kujitokeza mara kwa mara na kuwa kana kwamba wamekata tamaa.

Rooney alipata kuomba zaidi ya mara moja ahame United chini ya Fergie na pia chini ya Moyes akakataliwa, akaanza kucheza kwa makeke lakini kadiri muda unavyokwenda makali yanapungua akiishia kupaisha mipira tu.

RVP naye alikumbwa na majeraha kabla ya kupona na pamekuwapo tetesi hivi karibuni kwamba alikuwa akifikiria ama kurudi Arsenal au kwenda klabu nyingine majira yajayo ya kiangazi, kwani anaona mambo hayaendi Old Trafford.

Mashetani Wekundu walitokwa jasho hasa Jumapili kwenye mechi dhidi ya timu inayoshika nafasi ya mwisho kati ya 20 za Ligi Kuu, huku United wakiwa ya saba.

Walianza kufungwa, wakasawazisha na kupachika bao la pili dakika mbili tu baadaye, na wakati Moyes akishangilia akijua ameokoa pointi zote tatu, Fulham walirudisha bao na kumfanya Mskochi huyo abaki akilaani bahati yake mbaya na zama safi alizokuwa nazo Fergie.

United walikuwa na jumla ya pasi 649 lakini wawili hao walishindwa hata kukamilisha asilimia moja ya hizo pasi.

Jumatano hii Manchester United wanafunga safari kuja London kucheza na Arsenal ambao nao walijeruhiwa Jumamosi kwa kufungwa mabao 5-1 na Liverpool.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Man Utd hakijaeleweka

Nahodha wa England ni msagaji