*Vigogo wa Madrid waingiwa wasiwasi
*Wilshere amfuata Pellegrini West Ham
*Arsenal nao waendelea kuunda kikosi
WAKATI fainali za Kombe la Dunia zikiendelea Urusi, kuna taarifa Hispania na Italia kwamba nyota wa Ureno, Cristiano Ronaldo anakwenda Juventus.
Taarifa zimesambaa kiasi cha kuwafanya mabosi wa Madrid kuwa na wasiwasi na kumtaka nyota huyo aweke wazi msimamo wake na awaambie washabiki kwamba klabu hawakuhusika kumwingiza wkenye sakata hilo.
Inadaiwa kwamba Juventus wanataka kujiimarisha kwa kumchukua mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United kwa pauni milioni 88 na kumpa mshahara mkubwa kuliko anapata Madrid, wakati huu ikisemwa amechoka kukaa Santiago Bernabeu na anataka kukabiliana na changamoto za sehemu nyingine.
Wakala wa mchezaji huyo, Jorge Mendez anasema mteja wake anaweza kuondoka Madrid huku Rais Florentino Perez wa Real Madrid akihofia kwamba kuondoka kwake, kama ikiwa, kutawachefua washabiki wanaoweza kuushukia uongozi wake. Magazeti ya Hispania na Italia yanazungumzia uhamisho huo huku taarifa nyingine zikisema angeweza hata kutambulishwa wikiendi hii.
Mambo yamebadilika ghafla, ambapo inadaiwa anaweza kuachiwa kuondoka kwa pauni hizo milioni 88 wakati mkataba wake una kifungu kinachotaka pauni bilioni moja kutoka klabu yoyote inayotaka mazungumzo ya kumchukua. Kwa miezi 12 iliyopita kambi ya Ronaldo, 33, imekuwa ikieleza kutofurahishwa kwa mchezaji huyo anayejiona kwamba amesalitiwa kwa kutopewa mkataba mpya wneye maslahi zaidi mwanzoni mwa msimu uliomalizika.
Manchester United wanadaiwa kuulizia juu yauwezekano wa kumpata Ronaldo kwa ajili ya kumrejesha Old Trafford, lakini ‘Bibi Kizee wa Torino’ anaonekana kujizatiti kumchukua, huku Real Madrid wakifikiria kuuza ili wanunue ama Kylian Mbappe au Neymar.
Paris Saint-Germain (PSG) wapo tayari kutoa pauni zaidi ya £100m kumnyakua kiungo wa Chelsea na Ufaransa, N’Golo Kante, 27.
West Ham wanaofundishwa na Manueli Pellegrini wanafikia makubaliano ya kumchukua Jack Wilshere, 26, wa Arsenal kwa mkataba wa miaka mitatu na kitita cha pauni milioni tano na kumrejesha kiungo wake wa zamani aliyekwenda Marseille, Mfaransa Dimitri Payet lakini atatakiwa akubali kupunguziwa mshahara.
Jack Wilshere has started a medical at West Ham as the Hammers look to sign the 26-year-old midfielder on a free transfer from Arsenal on a three-year contract and a package worth £5m. (Times – subscription required)
Winga wa Crystal Palace, Wilfried Zaha amekataa mpakata mpya wa £120,000 wakati huu ambapo Tottenham, Everton na Borussia wakitaka kumchukua jamaa huyu wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 25.
Arsenal wapo kwenye mazungumzo na Sevilla na kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, Steven N’Zonzi, 29, kwa ajili ya kumpeleka Emirates kiangazi hiki. Arsenal pia wanaendelea na mazungumzo kwa ajili ya kumchukua kiungo wa kimataifa wa Uruguay, Lucas Torreira, 22, kutoka Sampdoria kwa pauni milioni 26 na anaweza kutangazwa wakati wowote, ikitegemea ikiwa ataruka kuja London moja kwa moja kutoka Urusi au atakwenda kwanza nyumbani na wenzake.
Washika Bunduki wa London hao wamefanya mazungumzo na Boca Juniuors wa Argentina kwa ajili ya kuwauzia golikipa wao, David Ospina aliyesajiliwa London Kaskazini baada ya fainali za Kombe la Dunia 2014 alikowika sana, lakini hakuonesha makeke Arsenal na sasa nafasi yake inachukuliwa na Bernd Leno kutoka Bayer Leverkusen.
Kocha mpya wa Arsenal, Unai Emery anatengeneza kikosi chake na ndiye alimwambia Wilshere kwamba hawezi kumhakikishia anfasi kwenye kikosi chake cha kwanza kila wakati. Tayari amesajili mchezaji huru kwenye nafasi ya ulinzi, Stephan Lichtsteiner akitoka Juventus, na mlinzi wa kati, Sokratis kutoka Borussia Dortmund.