in

Ronaldo kurudi Real Madrid?

Cristiano Ronaldo

Mchezaji kurudi timu aliyohama ni jambo la kawaida katika mchezo wa soka. Wapo wachezaji ambao waliwahi kuhama timu zao na baadaye kurejea tena. Mathew Flamini alihama Arsenal na kwenda AC Milan, lakini miaka michache baadaye alirejea mikononi mwa Arsene Wenger.

Ibrahim Ajibu alihama Simba na kwenda Yanga, kabla ya miaka michache baadaye kuondoka Yanga na kurejea Simba. Zlatan Ibrahimovic alihama AC Milan na kwenda PSG lakini miaka michache baadaye amerejea AC Milan.

Kwa mazingira hayo ndiyo yanayomkuta nyota wa Juventus Cristiano Ronaldo ambaye ametajwa kufanya mipango ya kurejea Real Madrid. Ronaldo alijiunga na Real Madrid mwaka 2009 sambamba na nyota mwingine Karim Benzema ambapo walicheza kwa mafanikio zaidi.

Taarifa za Ronaldo kutaka kurudi Real Madrid zimethibitishwa kwa mkutano uliofanywa kati ya wakala wake Jorge Mendes na bodi ya wakurugenzi ya Real Madrid juu ya uwezekano wa mteja wake kurejea Santiago Bernabeu.

Tanzania Sports
Cristiano Ronaldo

Kimsingi Ronaldo tangu aondoke Real Madrid julai 2018 miezi miwili baada ya kocha Zinedine Zidane kujiuzulu hajapata mafanikio yoyote kisoka. Tangu 2018 hajacheza kwa mafanikio na sasa imedhihirika kuwa Ronaldo anaimisi Real Madrid kuliko wakati wowote ule.

Vilevile Real Madrid nayo inammisi nyota huyo ambaye alikuwa nguzo ya ushindi wao katika Ligi ya Mabingwa Ulaya ambako walifaniiwa kitwaa taji hilo mara tatu mfululizo.

Matamanio ya Ronaldo yanatokana na kushuhudia klabu yake ya Juventus ikishindwa kufurukuta mbele ya FC Porto ya Ureno katika hatua ya mtoano Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ndoto za Ronaldo kutwaa taji la UEFA akiwa na uventus Turin zilikatizwa na Porto ambayo ilikata tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali.

Wakala wa Ronaldo Jorge Mendes anathibitisha kuzungumza na Real Madrid ni kitendo cha kuonesha nyota huyo yupo tayari kurejea maskani yake ya zamani alikopata mafanikio makubwa kwenye soka.

Taarifa za Ronaldo kutaka kuondoka Juventus zilianza kufichuliwa na wachezaji wa Real Madrid katika kipindi ambacho nyota alienda kutazama mechi ya El Clasico ndani ya dimba la Santiago Bernabeu msimu uliopita.

Hayo ni matakwa ya Ronaldo mwenyewe baada kuona hakuna dalili za yeye kupata mafanikio mengine akiwa na Juventus. Kutolewa mashindanoni Ulaya imekuwa kama chachu yay eye kuamua kuondoka Italia.

Kwa upande wao klabu ya Juventus Turin wapo tayari kumuuza Ronaldo kwa dau la pauni milioni 25. Uamuzi wao unaotaojana na hali mbali ya kifedha waliyonayo pamoja na matokeo mabovu yaliyopo uwanjani.

Juventus Turin ndani ya uwnaja wameachwa mbali na vinara wa Ligi hiyo Inter Milan kwa tofauti ya pointi 10, huku wakiwa na mechi moja mkononi.

Aidha, mshahara mkubwa ni sababu nyingine ambayo Juventus inataka kuachana na Ronaldo. Nyota huyo analipwa kiasi cha pauni milioni 28 kwa mwaka ambao ni mkubwa huku wakikabiliwa na mdororo wa uchumi klabuni hapo. Mkataba wa Ronaldo na Juventus unamalizika mwaka 2022, ambapo sasa ana umri wa miaka 36 angali anadai kucheza angalau misimu mitatu mingine.

Wakati Ronaldo na Zidane walipoandoka Real Madrid kulikuwa na hali ya sintofahamu hivyo kusababisha baaaye iwe inafanya kazi ya kubadili makocha kuziba pengo la Zidane.

Awali Real Madrid ilimchukua Julen Lopetegui lakini akaaishia kufkuzwa kutokana na matokeo mabovu. Santiago Solari alikabidhiwa timu akitokea kikosi cha pili Castilla.

Hata hivyo Solari alishuhudia mabingwa hao wa Ulaya wa zamani wakitetemeshwa nyumbani kwa mabao 4-1 hali ambayo ilichangia kuondolewa kocha huyo.

Chini ya Zidane klabu ya Real Madrid na Ronaldo walifanikiwa kutwaa mataji ya La Liga,Super cup na UEFA. Uhisiano kati ya Zidane na Ronaldo umekuwa mzuri na hivyo kuwa kete muhimu kwa nyota hao kuungana tena kufanya kazi pamoja.

Kwa sasa Zidane ameituliza timu baada ya kutokea kimbunga kibaya misimu kadhaa iliyopita. Kwa sasa wapo nyota wengine vijana ambao wanaweza kujifunza kutoka kwa Ronaldo, mfano Rodrygo Goes, Vinicius Junior,Hugo Duro,Blanco,Lunin, Odriozola na wengineo.

Kimsingi Real Madrid ipo kwenye mchakato wa kubadili timu timu kutoika kikosi cha dhahabu kilichotwaa mataji mengi kwenda kizazi kingine. Wachezaji wengi wana umri wa juu za 30 kama Marcelo,Lucas Vazquez,Sergio Ramos,Luka Modric,Toni Kroos,Karim Benzema ambao walikuwa uti wa mgongo wa tiomu hiyo.

Ingizo la vijana Ferland Mendy, Lunin,Rodrygo Goes, Vinicius Junior,Luka Jovic,Marvin,Hugo Duro, Martin Odegaard,Borja Mayoral,Reinier,Eder Militao,Sergio Arribas, Diego Attube, Blanco, Fran Garcia na wengineo.

Tanzania Sports
Eden Hazard

Real Madrid kufikiria kumrudisha Ronaldo ni ujumbe mbaya kwa nyota wake Eden Hazard ambaye tangu amejiunga amekumbwa majeruhi ya maeneo mbalimbali mwilini mwake.

Hazard ametajwa na baadhi ya mashabiki kama mcheaji aliyekuja kula pensheni ya kustaafu ya soka kwa kile ambacho kinatajwa hajafanya la maana kumzidi hata Lucas Vazquez.

Takwimu zao ziko wazi kimafanikio Hazard hajafikia hata robo ya kile alichoshinda Lucas Vazquez ambaye anachezeshwa namba tofauti beki wa kulia, winga na mshambuliaji wa pili.

Kwahiyo ikiwa Ronaldo atatua Real Madrid maana yake Eden Hazard atakuwa kwenye wakati mgumu zaidi ikiwa ataendelea kuwa na hali hiyo, huku chipukizi Rodrygo,Vinicius na Marvin wakitishia nafasi yake. Ni lini Ronaldo atarejea Real Madrid? Hilo ni litakuwa suala la muda tu. Tusubiri na kuona.

Report

Written by Mark Mpangala

*Markus Mpangala ni Mhariri, Mwandishi wa Makala Maalumu, Mwanahabari,Mwanablogu,Mwanafasihi na Mwanasafu, ambapo kwa kipindi cha miaka 12 amefanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali vikubwa na vidogo nchini Tanzania katika Michezo, Siasa, Elimu na utalii. Pia ni mchambuzi mchangiaji wa masuala ya siasa na utawala bora katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC SWAHILI). Ni mhariri na mhamasishaji wa usomaji wa vitabu*

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Nuno Espírito Santo

TUTENGENEZE AKINA MOURINHO NA NUNO SANTO WETU!

Jamie Vardy

JAMIE VARDY NI MFANO WA KUIGWA KWA WACHEZAJI WA “NDONDO”