in

Refa ameharibu ushindi wa Real Madrid

Ferland Mendy celebrates his strike

Hivi karibuni wachezaji wa klabu ya Gor Mahia ya Kenya walizusha vurugu baada ya mchezo wao dhidi ya Napsa ya Nigeria. Wachezaji wa Gor Mahia waliona refa wa mchezo huo alikuwa amekosea kutoa adhabu ya penalti dakika za nyongeza iliyowawezesha Napsa kusawazisha bao hivyo mchzo kumalizika kwa sare 2-2 haikuwa sahihi.

Gor Mahia waliamini wangemaliza mchezo huo kwa ushindi wa bao 2-1. Mambo hayakuwa hivyo, ndipo hasira zao zikaibuka kumshambulia mwamuzi wa mchezo.

Ligi ya Mabingwa Ulaya imeendelea jumanne na jumatano wiki hii, ambako Real Madrid walisafiri hadi nchini Italia kumenyana na wenyeji wao Atalanta. Katika mchezo huo Real Madrid ilikuwa kwenye kipimo kwani haijawa na matokeo mazuri msimu huu kwenye Ligi ya Mabingwa.

Kipimo hicho kilikuwa na maana Real Madrid ilipaswa kucheza bila nyota wao 9 wa kikosi cha kwanza. Ndiyo maana haikushangaza kuona kocha Zinedine Zidane akipanga wachezaji katika nafasi ambazo sio zao lakini hakukuwa na namna nyingine.

Isco Alcaron alicheza nafasi ya mshambuliaji yaani namba 9, kisha Lucas Vazquez akacheza nafasi ya beki wa kulia. Kiasili Isco ni kiungo mshambuliaji,mshambuliaji namba mbili na anaweza kucheza wing azote mbili kulia au kushoto.

Luvas Vzquez ni winga wa kulia au kushoto, lakini mara kadhaa amekuwa akitumika kama beki wa kulia na mshambuliaji namba mbili. Kwenye benchi alikuwepo mshambuliaji mmoja tu, Mariano Diaz ambayo hucheza nambari. Hadi hapo tunaona Zidane aliunga unga timu yake ili icheze dhidi ya wakali Atalanta lakini alipata matokeo mazuri.

NAMNA REFA ALIVYOHARIBU

Tukio lililotokea katika dakika 17 ya mchezo baada ya mchezajiwa Atalanta Remo Freuler kulimwa kadi nyekundu kwa madai ya kumchezea madhambi beki wa kushoto wa Real Madrid, Ferland Mendy wakati akielekea  eneo la hatari la Atalanta.

Mwamuzi wa mchezo huo Tobias Stieler alitoa kadi nyekundu ambayo ilikuwa adhabu kubwa zaidi kwa Atalanta. Wachambuzi wa soka wanasema uamuzi wa refa huyo ulikuwa mkubwa kulinganisha na tukio halisi.

Kimsingi mwamuzi angeweza kutoa adhabu ya kadi ya njano lakini sio kumlima nyekundu. Hapo ndipo refa aliharibu mchezo kwani ukawa wa upande mmoja ambako Real Madrid walishambulia lango la Atalanta kama nyuki ambao nao walikuwa wamejaa eneo lao la 18 kulinda lango lao.

Kucheza dhidi ya timu inayojilinda kwa asilimia 100 ni changamoto kwa timu pinzani na inasababisha mchezo kuwa wa kubana zaidi badala ya uwazi. Wengi walitarajia Atalanta ingekuwa moto kuotea mbali lakini hawakuwa na madhara ndani ya dakika 17 za mchezo kabla ya Remo kulimwa kadi nyekundu.

Pengine ukiwa shabiki unaweza kuunga mkono hatua ya wachezaji wa Gor Mahia waliomvamia refa kutokana na kukasirishwa na uamuzi mbovu. Lakini kwenye soka la Ulaya mambo hayaendi hivyo. Wachezaji wanaweza kumzunguka mwamuzi na kumhoji lakini si kumshambulia kwa makonde kama ilivyotokea kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

USHINDI WA MECHI 5

Real Madrid wameandika nchini Italia. Bao la Ferland Mendy lilishusha presha kubwa waliyokuwa nayo wachezaji na benchi la ufundi. Ni timu chache sana zinazoweza kumudu kucheza bila kuyumbishwa na presha waliyonayo, kwa Real Madrid kila kitu kinawezekana.

Aghalabu hali ya presha inapotokea, wengi wanageuka na kumtazama kocha wao Zinedine Zidane na wachezaji wake wanafanya nini ili kujiondoa kwenye hali hiyo.

Katika mchezo wao dhidi ya Atalanta wameonesha kuwa wanaweza kumudu kupambana na timu yoyote,kuonesha namna wanavyoweza kupambana na uwezo wa kutwaa ubingwa. Mara nyingi timu inapokuwa kwenye presha kubwa imeonesha namna wanavyocheza kwa utulivu na kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

Tanzaniasports imekusanya takwimu za timu hiyo ambazo zinasema; mwezi Januari mwaka huu Real Madrid walikuwa kwenye hali mbaya kuanzia Ligi Kuu La Liga, kisha wakatupwa nje ya mashindano ya Copa del rey na Supercopa  de Espana.

Tayari mataji mawili yalikuwa aymeota mbawa mikononi mwao. Lakini kila mara wamekuwa wakirekebisha makosa yao na kuendelea kupata matokeo mazuri. Kwa sasa wamebakiwa na mataji mawili; Ligi ya Mabingwa na La Liga.

Ushindi wao dhidi ya Atalanta ni watano mfululizo. Ni dhahiri ushindi huo utawapa motisha ya kusaka mataji yote mawili. Lakini ushindi wao mara nyingi unakuja pale wanapokuwa na upungufu wa wachezaji sababu ya majeruhi.

Kwenye mchezo wao dhidi ya Atalanta waliwakosa wachezaji nane hadi tisa kutokana na kuumia. Karim Benzema, Sergio Ramos,Dani Carvajal,Fede Valverde,Rodrygo Goes,Eden Hazard na Marcelo.

Kuumia kwa nyota hao ndiko kumewapa nafasi wachezaji chipukizi Sergio Arribas, Chust na Hugo Duro kupewa dakika 20 za mchezo dhidi ya Atalanta. Kwa chipukizi ni hatua kubwa hususani kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

MATAJI MAWILI

Baada ya kupoteza mataji mawili Copa del rey na Supercopa de Espana, sasa Real Madrid wamebakiwa na mataji mawili tu; Ligi ya Mabingwa na La Liga. Real Madrid anatarajiwa kukutana na vibara wa La Liga Atletico Madrid Machi 7.

Awali pengo la alama lilikuwa 10 lakini sasa zimepaki tatu. Hii ina maana ushindi watakaopata Real Madrid utaondoa pengo la alama, pia ikiwa Atletico watashinda wataongeza pengo la alama.

Endapo wachezaji majeruhi wote watarejea maana yake timu hiyo itakuwa imara zaidi na kocha atapunguza kuunga unga kikosi chake.  Lakini hilo haliwezi kuwahakikishia kuwa watatwa taji la Ligi ya Mabingwa au La Liga. Mechi bado.

Report

Written by Mark Mpangala

*Markus Mpangala ni Mhariri, Mwandishi wa Makala Maalumu, Mwanahabari,Mwanablogu,Mwanafasihi na Mwanasafu, ambapo kwa kipindi cha miaka 12 amefanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali vikubwa na vidogo nchini Tanzania katika Michezo, Siasa, Elimu na utalii. Pia ni mchambuzi mchangiaji wa masuala ya siasa na utawala bora katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC SWAHILI). Ni mhariri na mhamasishaji wa usomaji wa vitabu*

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Mpambano wa nguvu

Al Ahly ni kibonde wa Simba

Namungo FC

Namungo FC kuwatikisa Raja Casablanca?