in , ,

Qatar kupokwa uenyeji Kombe la Dunia?


*Platini asema halichezeki kwenye joto

*Sepp Blatter: Huenda kura ikarudiwa

 

Hofu imeanza kutanda, baada ya kuchomoza tetesi kwamba huenda Qatar wakapokonywa uenyeji wa michuano ya soka ya Kombe la Dunia 2022.

Hali ni tete, kwa sababu watu wameanza kujivua magamba na kueleza ukweli kwamba haitakuwa rahisi taifa hilo kuendesha michuano wakati hali ya hewa itakuwa ya joto kali.

Zipo habari kwamba Shirikisho la Soka la Qatar linafikiria kuomba kubadilisha tarehe ili mashindano yawe wakati wa baridi.

Hata hivyo Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Sepp Blatter anasema hajapata ombi hilo, lakini Qatar wakithubutu kulitoa, huenda ikanyang’anywa kabisa nafasi hiyo waliyopigania kwa nguvu kubwa.

Ulimwengu wa soka ulishangazwa Qatar walipopewa uenyeji huo na kuachwa kwa waombaji wengine kama Marekani, Australia, Korea Kusini na Japan.

Hamaki hiyo hivi karibuni imehusishwa pia na tetesi za kwamba mlungula ulitembea kutoka kampuni kubwa za taifa hilo lenye utajiri wa mafuta, yanayomiliki klabu kadhaa za soka duniani.

Lakini sintofahamu kubwa zaidi ni kwamba tarehe za mashindano hayo zinaangukia wakati joto la Qatar litakuwa limefika hadi nyuzijoto 50!

Rais wa UEFA, Michel Platini amesema wazi kwamba haiwezekani wanasoka wakacheza kwenye hali ya hewa ya joto kiasi hicho na akataka mashindano hayo yahamishiwe majira ya baridi.

“Ili ratiba ibadilishwe kwenda majira ya baridi lazima Qatar walete ombi. Hawajafanya hivyo hadi sasa, na wanajua wakijaribu tu, kuna hatari ya kupokonywa uenyeji, maana nchi nyingine zitaweka pingamizi na kura itarudiwa upya,” Blatter ametoa angalizo.

Wazo la kubadili ratiba hiyo tayari lina utata, kwa sababu ligi zote kubwa na zenye faida zaidi za Ulaya zimeweka msimamo wa kutumia nguvu zote kuhakikisha mashindano yanafanyika katika muda wake wa kawaida.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sir Dave Richards amesema kombe hilo haliwezi kuchezwa hapo Qatar wakati wa joto.

“Haiwezekani hata kidogo, sasa inaonekana wazi kwamba wachezaji hawatamudu joto hilo…waandaaji walisema eti wataweka viyoyozi uwanjani, je itakuwaje kwa washabiki na wadau wengine?” akahoji.

Maoni ya Blatter, Platini na Richards yanaonesha kwamba kuna kitu nyuma ya pazia kinakuja, tena si muda mrefu kutoka sasa, tena pakiwa na shinikizo la kisiasa pia.

Kwa hali ilivyo, uenyeji wa Kombe la Dunia 2022 unaelekea kuwaponyoka Qatar, maana kila hesabu inaelekea kugoma, labda kama watakuja na nyingine mpya kuliko wanavyofikiria vigogo hao na wadau wengine.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

*SERIKALI YARIDHIA MCHAKATO WA UCHAGUZI TFF*

Uwanja wa Azam kuwa miongoni mwa viwanja vilivyothibitishwa na FIFA kwa Ubora wake.