in , ,

Pierre- Emerick Aubameyang: alikaribia kutua Newcastle Utd

Kuna habari ambazo kwenye mpira huwa zinauma sana kila unapopata nafasi ya kusimuliwa au kuzikumba.
Moja ya habari ambazo mashabiki wengi wa Arsenal huchukia kuzisikia ni wao kuwakosa wachezaji nyota katika sajili mbalimbali.
Wengi huwa wanafikiria kikosi chao kingekuwaje kama Zlatan Ibrahimovic angefanikiwa kuwepo ndani ya kikosi cha Arsenal akiwa na wachezaji kama Buffon, Pique, Roberto Carlos, Didier Drogba, Ronaldinho, Messi na wengine wengi.

Picha inayokuja hapa ni kuiona Arsenal yenye mafanikio makubwa, Arsenal yenye majina makubwa yenye vipaji vikubwa.
Lakini cha kusikitisha majina haya yote hayakufanikiwa kusajiliwa na Arsenal ila baadaye yakaja kuwa majina makubwa tofauti na kipindi ambacho Arsenal walitaka kuwasajili.

Hii hutokea unaweza kushindwa kumsajili mchezaji na akaenda sehemu nyingine akawa nyota.
Manchester United mwaka 1993 walishindwa kumsajili Allan Shearer ambaye alienda Blackburn Rovers, hawakukata tamaa mwaka 1996 walitaka tena kumsajili lakini Allan Shearer alienda Newcastle United.

Newcastle United, sehemu ambayo ingekuwa moja ya sehemu ambayo Pierre- Emerick Aubameyang angekuwa amepita.
Mwaka 2013 kulikuwa na msafara mkubwa sana kutoka St. James Park uliokuwa unaelekea Ufaransa.
Aliyewahi kuwa skauti mkuu wa Newcastle United Graham Carr aliamua kwenda nchini Ufaransa ili kuleta wachezaji wapya ndani ya kikosi chao.

Mmiliki wa Newcastle United alitoa pesa ambazo Graham Carr zilimwezesha kuleta wachezaji wapya kutoka Ufaransa.
Ndiyo ulikuwa wakati ambao Mathieu Debuchy, Mapou Yanga-Mbiwa , Yoan Gouffran, Massadio Haidaea na Moussa Sissoko.
Newcastle walifanya usajili ambao uliifanya timu ionekane ni timu ya Wafaransa, lakini hawakujali hayo maneno , kitu pekee walichokihitaji ni wao kuona timu yao inafanya vizuri ikiwa na wachezaji ambao ni bora.

Mahitaji yao hayakuishia pale tu walipowaleta hao wachezaji watano, walibakiwa na hitaji moja la muhimu na la msingi kwao, nalo ni kumleta mshambuliaji mmoja wa kati mwenye kasi, kijana na mwenye uwezo wa kufunga magoli mengi.
Kwa wakati huo walikuwa na Demba Ba ambaye alikuwa anahitajika sana na vilabu vingi barani ulaya ambapo mwisho wa siku alienda Chelsea.

Akiwa amesajiliwa kutoka Westham United mwaka 2011 na kufanikiwa kufunga magoli 16 katika msimu wake wa kwanza katika ligi kuu ya England , Demba Ba alionekana ƙlulu kwa vilabu vikubwa.
Mwisho wa siku aliondoka na kwenda Chelsea huku nyuma akimwacha Papiss Cisse ambaye hakufanikiwa kuipatia Newcastle United magoli mengi

Hivo hitaji la timu likawa kumtaka mshambuliaji mwingine mwenye kasi na uwezo mkubwa wa kufunga magoli.
Macho ya mabosi wa Newcastle United yalitua tena nchini Ufaransa katika klabu ya Saint- Etienne ambapo walikuwa na Pierre-Emirick Aubameyang.

Mshambuliaji ambaye alionekana mtu sahihi ambaye atakuja kukidhi mahitaji ya Newcastle United kwa wakati huo.
Graham Carr alihangaika muda mrefu katika nchi ya Ufaransa ili apate kumsajili Pierre- Emirick Aubameyang.
Msimu ambao Newcastle United ilifanikiwa kufika robo fainali ya kombe la UEFA Europa League na kushika nafasi ya kumi na sita kwenye ligi kuu.

Kushika kwao nafasi ya kumi na sita kwenye ligi kuu ya England ndicho kilichoua matamanio ya mashabiki wa Newcastle United kumuona Pierre- Emerick Aubameyang katika klabu yao.

Matokeo ya timu yalikuwa mabaya, matokeo ambayo hayakuwa na ushawishi kwa mchezaji yoyote mwenye ndoto za kufanikiwa katika ngazi ya juu ya mpira kwenda Newcastle United.
Nafasi ya kumi na sita (16) kwenye ligi, nafasi ambayo ilikuwa haimpi nafasi hata kidogo Newcastle ya kushiriki katika mashindano yoyote makubwa barani ulaya.

Mashindano ambayo yamebeba matamanio ya wachezaji wengi duniani.
Wachezaji wengi duniani hutamani kuwepo kwenye timu ambayo inauwezo wa kushiriki mashindano ya ulaya mara kwa mara ( Uefa Champions league na Uefa Europa League).

Ndiyo maana Borrusia Dortmund walipokuja kumtaka Pierre-Emirck Aubameyang haikuwa kazi ngumu kwa baba yake Pierre ambaye na yeye anaitwa Pierre kumruhusu mwanaye aende kucheza Borrusia Dortmund.
Timu ambayo ilitoka kushinda kombe la ligi kuu ya Ujerumani (Bundesliga) na kufika fainali ya kombe la klabu bingwa barani ulaya.

Mafaniko haya yalimshawishi baba yake Pierre kuwa mwanaye atakuwa na wakati sahihi wa kukuza kipaji chake akiwa Borussia Dortmund kuliko Newcastle United.

Leo hii tunawaona Arsenal wakihangaika kutaka kumsajili Pierre- Emerick Aubameyang kutoka Borussia Dortmund, kuna dalili ambazo zinaonesha anaweza asifanikiwe/au afanikiwe kwenda Arsenal.
Kushindwa kwake kwenda Arsenal itakuwa mara ya pili kwake kushindwa kwenda England.japo dalili zinaonyesha atafanikiwa kipindi hiki.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

BUSARA YA MATUMIZI IMEWAWEKA MAN CITY MAHALA WALIPO

Tanzania Sports

KWANINI SPURS WALIIFUNGA MANCHESTER UNITED?