in , , ,

Nyota wapya Simba wana zigo zito

Leandre Willy Essomba Onana

Hakuna shabiki wa Simba mwenye kupenda unyonge kwahiyo ni jukumu viongozi kuepuka usajili wa mizuka ambao unagjarimu timu kwa ujumla wake….

VYOVYOTE umavyoweza kudhani lakini klabu ya Simba inaelekea kuwatwisha zigo zito sana wachezaji wake wapya. Simba ni klabu maarufu barani Afrika na ndiyo timu pekee inayopeperusha bendera ya ukanda wa Afrika Mashariki kwenye mashindano ya Super League barani Afrika. 

Kuwa katika hadhi hiyo ina maana uongozi wa Simba unatakiwa kusajili wachezaji wenye viwango vya juu. Ilipofikia Simba inawindwa na nyota wengi, mawakala wengi na makocha pia. Ni wakati ambao uongozi unatakiwa kuepuka usajili wa wachezaji ambao ni magalasa. 

Hawa ni wachezaji wanaokaa msimu mzima bila kucheza, maana yake hawana ushindani wala utimamu wa miili yao. Hii Ina maana Simba wanaleta wachezaji ambao watabeba mzigo mzito. Washabiki wa Simba hawataki unyonge katika msimu wa tatu mfululizo, kwani walizoea raha na ndicho wanapaswa kupewa na uongozi wao. 

Hivi karibuni klabu ya Simba imetangaza kukamilisha usajili wa winga wa Kimataifa wa Cameroon , Leandre Willy Essomba Onana kama mchezaji huru akitokea Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda kwa Mkataba wa Miaka miwili.

Kwa umri Onana wa Miaka 23,  msimu uliopita alifanikiwa kuwa Mchezaji na Mfungaji bora wa Ligi Kuu Nchini Rwanda akifunga magoli 15 na kutoa asisti 10 kwenye michezo 20 ya Ligi hiyo. Nyota huyo anasifika kwa kasi, chenga na stamina akiwa na mpira huku wakimfananisha na Cristiano Ronaldo kiuchezaji. 

Usajili huu una maana moja kubwa Simba wanao mzigo mzito wa kuhakikisha wanalinda “brand” Yao katika mashindano ya CAF. Vilevile Simba ndiyo sehemu ambayo Nyota wengi wamepita na kufanikiwa kucheza klabu nyingine kubwa Afrika ikiwemo Al Ahly. 

Simba wanatakiwa kusajili wachezaji ambao watawatoa udenda timu pinzani kama Al Ahly walivyofanya kwa Luis Miquissone. Simba wanatakiwa kuwa na wachezaji ambao wamejaa uwezo mzuri na kutamaniwa na vilabu vikubwa. Usajili wao unapaswa kulenga kuinua na kuendeleza hadhi yao sio wachezaji wa kukaa benchi. Ifike mahali Simba wawe na wachezaji wa kigeni wenye viwango vinavyostahili kuvaa jezi za timu hiyo.

Ni wakati mzuri kuhakikisha wachezaji wanaosajiliwa wanakuja kutekeleza majukumu yao kwa ustadi na ufanisi wa hali ya juu. 

Katika mashindano ya Super League, Simba ni klabu inaogopeka kutoka ukanda wa Afrika Mashariki, hivyo hofu ya vigogo inatakiwa kuonekana kupitia usajili unaofanyika. 

Kwa mfano usajili wa Onana ulete tija kwa kuwapa furaha Simba. Vilevile viongozi waepuke usajili wa mizuka kwa sababu imelazimika kuwaacha wachezaji wa kigeni waliosajiliwa kwa mizuka ya Mechi moja au mbili. Ni muhimu idara ya uchunguzi wa vipaji kuimarisha ubora wao kwa kuhakikisha wanapendekeza wachezaji wenye uwezo wa kuing’arisha Simba na sio vinginevyo. 

Hakuna shabiki wa Simba mwenye kupenda unyonge kwahiyo ni jukumu viongozi kuepuka usajili wa mizuka ambao unagjarimu timu kwa ujumla wake.

Simba sio timu ya kufikiria kuishia nusu fainali tena, bali ipandishe viwango kwa kulileta Kombe katika ardhi ya Tanzania. Nina Imani Simba wanayo fursa ya kubaki katika ubora na tishio Afrika lakini ni wakati pia viongozi wafikirie mataji ya CAF kuliko kuishia robo au nusu fainali. Hivyo basi mzigo wa kwanza uwe kwa Nyota wapya wanaosajiliwa ili waipeleke Simba katika ngazi za juu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Hannah Dingley

MWANAMKE WA KWANZA KUWA KOCHA WA TIMU YA WANAUME

Kila msimu Azam Fc wamekuwa na hekaheka nyingi lakini ufanisi wao bado hauridhishi kabisa.

Azam FC na hekaheka, bila wivu kwa Yanga, Simba