Menu
in , , , , ,

Nyota wanaosaka klabu mpya msimu huu

Wachezaji watano wa Manchester United ni kati ya wale wa vilabu mbalimbali ambao wanatakiwa kutafuta klabu mpya kabla ya kumalizika kwa dirisha la usajili. Imebaki wiki moja kabla ya kufungwa rasmi kwa dirisha la usajili Ligi Kuu England, huku wachezaji mbalimbali wakiwa  wanahaha kupata timu mpya baada ya kuambiwa na vilabu vyao kuwa waondoke kwani hawapo katika mipango yao. Ligi Kuu England imeanza kwa kishindo huku ushindani ukiwa mkubwa kutoka klabu moja na nyingine. TANZANIASPORTS inakuleta orodha ya wachezaji ambao wanatakiwa kuhama kwenye klabu zao za sasa na kutafuta mpya ili kuendeleza vipaji vyao.

ALEXANDER ISAK

Tanzania Sports

Mshambuliaji huyu kutoka Sweden ameingia katika mgogoro na klabu yake ya Newcastle United kutokana na uamuzi wake wa kutaka kuhamadimba la St. James Park. Pande zote mbili zinapingana, Newcastle United wanataka mshambuliaji wao huyu arudi kwenye viwanja vya mazoezi ili kujumuika na wenzake kwenye maandalizi ya mechi zijazo za Ligi Kuu, lakini kambi ya Alexander Isak imekata kata kata kuona nyota huyo anakuwa sehemu ya kikosi cha Newcastle United. 

Isak anawindwa na Liverpool na amebainisha bayana kuwa anataka kuhama klabu ya Newcastle United ambayo alijiunga nayo mwaka 2022.kulingana na ripoti mbalimbali za kimichezo, Liverpool wameweka ofa ya pauni milioni 55 kumnunua mshambuliaji huyo, lakini Newcastle United wanataka pauni milioni 100 ili kumwachilia. Sakata hili limewagusa hadi mashabiki wa Newcastle ambapo katika mchezo wao uliopita dhidi ya Liverpool wanamwita nyota huyo kuwa ni panya au msaliti kwao. Msimamo wa Isak umebaki palepale kuondoka ikiwa na maana anatakiwa kutafuta timu ndani ya siku 7 kabla ya dirisha kufungtwa.

GIANLUIGI DONNARUMA

Golikipa huyu wa mabingwa wa soka Ulaya, PSG amejikuta katika wakati mgumu baada ya kutemwa katika kikosi cha timu hiyo. Huyu ndiye golikipa wao namba moja, lakini alikataa kusaini mkataba mpya kwa sababu ya kudai mshahara mkubwa. Akiwa na umri wa miaka 26 Donnaruma amejikuta katika wakati mgumu kutokana na uamuzi wa ghafla wa PSG kumwondoa katika orodha ya wachezaji wake wa msimu ujao. PSG iliamua kumtema kutokana na uamuzi wa Donnaruma kutaka kutumikia mkataba wake hadi mwisho kisha kuondoka bure. 

Lakini PSG hawataki kukosa fedha, hivyo wanataka kumuuza nyota huyo ili wapate kiasi cha fedha kuliko kumruhusu kuondoka bure. Ikumbukwe Donnaruma amewahi kuifanyia vitimbi AC Milan ambako alikataa kusaini mkataba mpya na badala yake akaendelea kuitumikia hadi ulipofika mwisho na kuhamia PSG bure. Kwa upande wa PSG hawataki mambo ya nyota wao huyo kuondoka bure kama alivyofanya kwa AC Milan, na hivyo kama hataki kuondoka msimu huu na wao hamhitaji kwenye kikosi chao. Manchester City imetajwa kutaka saini ya golikipa huyo lakini wanatakiwa kuhakikisha wanamuuza golikipa wao Ederson kwenda klabu nyingine ili kupaa nafasi ya kumsajili Donnaruma.

ALEJANDRO GARNACHO

Huyu ni kinda aliyekulia katika klabu ya Manchester United na akapanda ngazi kutoka timu ya vijana hadi kikosi cha kwanza. Amekuwa nyota ambaye anatakiwa kuondoka Old Traford ili kulinda kipaji chake. Dalili za Garnacho kuhama Man United zilijitokeza baada ya fainali ya Europa League baada ya kuwekwa benchi na kocha wake Ruben Amorim. Inaelezwa kuwa Garnacho aliambiwa na kocha wake kuwa anatakiwa kusali ili kupata timu mpya. Kauli hiyo aliambiwa akiwa na wachezaji wenzake. Hata hivyo ripoti zinasema kuwa Chelsea wanafikiria kutuma ofa ya kumsjaili nyota huyo kutoka Argentina.

NICOLAS JACKSON

Chelsea wapo mbioni kumpiga bei mshambuliaji wao Nicolas Jackson ili kukusanya fedha za kumsajili Alejandro Garnacho. Ripoti za michezo zinasema Nicolas Jackson aliiambia Chelsea anataka kuondoka klabuni hapo. Klabu mbalimbali zinamtupia jicho ili kupata huduma yake zikiwemo za EPL na miamba ya Bundesliga, Bayern Munich.

ROSMUS HOJLUND

Ni sahihi kusema mshambuliaji huyu ameshindwa kukidhi matarajio licha ya kusajiliwa kwa bei ya kutupa ya pauni milioni 72 mwaka 2023. Hojlund alibebeshwa mzigo mzito wa kuleta mafanikio Man United akiwa na umri mdogo wa miaka 22 lakini ameshindwa kutimiza malengo ya klabu hiyo. Napoli inatajwa kutamani kumsajili nyota huyo na klabu ya Man United ipo tayari kumuuza kwa bei pungufu ili aondoke Old Traford.

KOBBIE MAINOO

Ana akipaji kikubwa, mtulivu, anacheza vizuri na kufanya mchezo wa soka uonekane ni rahisi zaidi. Aliyekuwa kiungo wa Man United, Paul Scholes anaamini Kobbie Mainoo ana kipaji kikubwa kuliko yeye katika umri wake, anasema wakati akiwa na miaka kama ya kinda huyo hakuweza kuwa na utulivu, ubora na ufundi kumzidi kijana huyo. 

Kobbie Mainoo miezi 18 iliyopita dunia ilikuwa miguuni mwake, lakini mambo yamebadilika kwa kasi mno na hivyo nafasi yake ya kubaki Manchester United ni ndogo tangu ujio wa kocha mpya Ruben Amorim kwa sababu hajapata nafasi ya kutosha kucheza mechi. Ili kuokoa kipaji chake njia mwafaka ni kuhama Man United, huku klabu za Real Madrid na Atletico Madrid zinatajwa kuwinda saini ya nyota huyo.

MARC GUEHI

Crytal Palace na Marc Guehi wamekuwa katika uhusiano mbaya kikazi licha yanyota huyo kuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha timu ya Taifa England ilipokuwa chini ya kocha Gareth Southgate. Guehi amekuwa mchezaji mwenye mwendelezo katika kikosi cha Crystal Palace na kuwafanya mashabiki wanaojazana kwenye dimba la Selhurst Park kufurahia kiwango chake, lakini kwa sasa anaelekea ukingoni. Guehi anawindwa na Newcastle United.

CHRISTOPHER NKUNKU

Alisajiliwa kama mchezaji mwenye kiwango bora na kipaji kisicho na wasiwasi, lakini hali ya mambo imekuwa vigumu kwani amekuwa akipata majeraha mara kwa mara. Sababu nyingine ya kuondoka ni kutokana na kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza chini ya kocha Enzo Maresca. Akiwa na miaka 27 nyota huyo anawinda na klabu ya Bayern Munich na klabu yake ya zamani ya RB Leipzig.

YOANE WISSA

Ulikuwa msimu mgumu kwa nyota huyu ndani ya klabu ya Brendford ambayo imempoteza kocha wao Thomas Frank aliyejiunga na Tottenham Hotspurs. Kocha huyo alidumu Brendford kwa miaka 7 lakini msimu huu anakiongoza kikosi cha Spurs, wakati nahodha wao Christian Norgaad na mfungaji bora wa msimu uliopita katika klabu hiyo Bryan Mbeumo wameondoka na kujiunga na vilabu vingine. Yoane Wissa anawindwa na klabu ya Newcastle United kama mchezaji mbadala wa Alexander Isak.

XAVI SIMONS

Chelsea wanafukuzia saini ya nyota huyu kutoka RB Leipzig ambaye anatakiwa kutafuta changamoto mpya. Nyota huyo anatamani kuondoka RB  Leipzig na kujiunga na klabu mpya ambayo ni Chelsea. Maisha yake katika klabu ya RB yanatajwa kufika mwisho, na hivyo hana chaguo lingine zaidi ya kuhama.

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

Leave a Reply

Exit mobile version