in ,

MZUNGUKO WA TATU LIGI KUU BARA

 

*YANGA, SIMBA, AZAM HAKUNA KUTELEZA*

 

Ligi Kuu Tanzania Bara iliendelea kushika kasi kwenye michezo ya jana na juzi ambapo hakuna iliyokubali kupoteza alama kati ya Azam, Yanga na Simba ambazo ndizo timu tishio kwenye ligi hiyo.

YANGA 4 – JKT RUVU 1

Yanga ambao walicheza mchezo wao hapo juzi waliwatandika JKT Ruvu 4-1
Yanga ambao walicheza mchezo wao hapo juzi waliwatandika JKT Ruvu 4-1

Yanga ambao walicheza mchezo wao hapo juzi waliwatandika JKT Ruvu 4-1. Mabao ya Yanga yalifungwa na Amis Tambwe aliyefunga mawili pamoja na Donald Ngoma na Thabani Kamusoko huku bao la JKT likifungwa na Michael Aidan.

Mshambuliaji Donald Ngoma alianza kuonyesha makeke mapema kwenye dakika ya pili ambapo aliwasumbua walinzi na kupiga krosi iliyookolewa na kuzaa kona. Ndani ya dakika ya 33 ya mchezo mshambuliaji huyo akaipatia Yanga bao la kwanza baada ya kushirikiana vyema na Haji Mwinyi pamoja na Amis Tambwe aliyetoa pasi ya bao.

Ngoma aliendelea kuonyesha makeke yake lakini wachezaji wa JKT walionekana kumkamia hivyo hakuweza kuleta madhara tena mbaka kipenga cha mapumziko kikapulizwa matokeo yakiwa 1-0.

Dakika tatu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili Amis Tambwe akafunga bao rahisi na kuifanya Yanga kuwa mbele kwa mabao mawili baada ya golikipa Tony Kavishe wa JKT kushindwa kuiondosha krosi ya Deusi Kaseke kwenye eneo la hatari.

Hazikupita dakika mbili vijana wa Fredy Minziro wakajibu mapigo kupitia kwa Michael Aidan aliyeutumia mwanya wa golikipa Ally Mustapha kuwa mbele ya lango na kuacha nafasi nyuma yake. Aidan alifunga bao hilo kupitia shuti la mbali.

Kwenye dakika ya 62 Amis Tambwe akaunganisha krosi ya Simon Msuva na kuipatia Yanga bao la tatu kabla ya Thabani Kamusoko kuongeza la nne zikiwa zimesalia dakika mbili kabla ya mchezo kumalizika.

SIMBA 3- KAGERA SUGAR 1

Simba waliwaadhibu Kagera 3-1
Simba waliwaadhibu Kagera 3-1

 

Simba nao waliendeleza rekodi yao ya asilimia mia moja msimu huu huku mshambuliaji wao Hamis Kiiza akifunga hat-trick dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar-es-salaam hapo jana Jumapili.

Kiiza aliifungia Simba bao la kwanza kwa kichwa kwenye dakika ya 30 ya mchezo baada ya kukutana na krosi ya Awadhi Juma. Bao hilo lilidumu mbaka kipindi cha  mapumziko kilipofika.

Punde baada ya kipindi cha pili kuanza Kiiza akaifungia Simba bao la pili kwa kichwa kutoka kwenye mpira wa adhabu uliopigwa na Mohammed Hussein. Dakika nne baadae Kagera Sugar wakapata bao lao la kufutia machozi kupitia kwa Mbaraka Yusuph ambaye aliwachambua walinzi wa Simba na kufunga bao rahisi.

Hamis Kiiza akakamilisha hat-trick yake kwa shuti kali kwenye dakika za 90+3 baada ya kupokea pasi ya Kazimoto. Sasa Kiiza anaongoza kwenye orodha ya wafungaji akiwa na na mabao matano kwenye michezo mitatu. Washabiki wa Simba wamedai kuwa hizo ni salamu ambazo wanatumiwa Yanga watakaokutana nao Jumamosi hii kwenye mchezo wa mzunguko wa nne.

MWADUI FC 0 – AZAM FC 1

John Bocco katika dakika ya 48 , akitupia bao pekee.
John Bocco katika dakika ya 48 , akitupia bao pekee.

 

Azam FC nao hapo jana walifanikiwa kuokoa alama tatu muhimu kupitia bao la nahodha John Bocco dhidi ya Mwadui FC kwenye mchezo uliopigwa ndani ya dimba la Mwadui jijini Shinyanga.

Azam walibakia 10 uwanjani baada ya mlinzi Aggrey Morris kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye dakika ya 60 ya mchezo baada ya kumchezea madhambi Rashid Mandawa. Nyekundu hiyo iliandamana na penati ambayo golikipa Aishi Manula aliipangua.

Kwa matokeo haya Yanga wanaendelea kubaki kileleni kwa tofauti ya mabao huku wakifukuzwa kwa karibu na Azam na Simba ambazo pia kila moja ina alama 9 sawa na Yanga.

Report

Written by Kassim

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

JANUARI NI MBALI MNO KWA FC BARCELONA

Tanzania Sports

TIMU YA WIKI EPL