in , ,

Manchester United waamka

*Burnley wa kwanza kushuka daraja

Baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo, hatimaye Manchester United wameamka na kupata ushindi mwembamba dhidi ya Crystal Palace, huku Burnley wakiwa timu ya kwanza kushuka daraja msimu huu.

United walianza kufunga kwa penati ya Juan Mata kabla ya Jason Puncheon kusawazisha kwa mpira wa kuparaza katika kipindi cha pili. Marouane Fellaini aliyerudi kwenye kiwango tangu aaminiwe na kocha Louis van Gaal alifunga bao la ushindi.

Man U sasa wamesogea karibu na kufuzu kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) msimu ujao. Penati ilitolewa kutokana na Scott Dann kushika mpira uliokuwa umepigwa na Ashley Young, ambaye pia alitoa pasi ya bao la pili.

Palace hawakukubali kufungwa kirahisi, ambapo kama si uhodari wa golikipa David De Gea si ajabu United wangepoteza pointi zote tatu. Man U wanashika anfasi ya nne wakiwa na pointi 68, mbili nyuma ya Arsenal na Manchester City.

Timu inayomaliza ligi wakiwa nafasi ya nne huingia kwenye hatua ya kwanza ya mtoano kwa ajili ya kufuzu kwa UCL na wanaweza kuwa Man U, Man City au Arsenal. Tayari Chelsea wametwaa ubingwa wa England, na walipewa siku nne za kupumzika wiki iliyopita kabla ya pambano lao la Jumapili hii dhidi ya Liverpool.

Liverpool wanashika nafasi ya tano wakiwa na pointi 61, hivyo kufanya uwezekano wa kuwafikia United kuwa mdogo. Southampton wanaoshika nafasi ya saba walizidi kupoteza mwelekeo baada ya kulazwa 2-0 na Leicester wanaopigana kuepuka kushuka daraja.

Katika matokeo mengine, Aston Villa waliwazidi nguvu West Ham kwa 1-0, Hull wakafungwa 1-0 na Burnley, wakati Tottenham Hotspur wanaoshika nafasi ya sita walipigwa 3-0 na Stoke katika matokeo ya kushangaza. Newcastle wamemaliza mfululizo wakufungwa mechi nane kwa kwenda 1-1 na West Bromwich Albion.

Burnley wameshuka daraja kutokana na matokeo ya timu nyingine.
Burnley wameshuka daraja kutokana na matokeo ya timu nyingine.

Burnley wameshuka daraja kutokana na matokeo ya timu nyingine, licha ya wao kushinda kwa bao la mfungaji wao bora, Danny Ings. Hilo lilikuwa bao la kwanza kwa Burnley katika saa 10 za mechi walizocheza, ukiwa ni ukame mkali.

Kilichowahakikishia kushuka daraja ni ushindi wa Sunderland, Leicester na Aston Villa pamoja na pointi moja muhimu waliyojinyakulia Newcastle.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Benteke kumbadili Sturridge Liverpool?

Fununu za usajili majuu