in , , ,

MISRI INATAKIWA KUSHUKA MGONGONI MWA SALAH

Moja ya timu ambayo ilikuwa inapewa nafasi ya kufanya vizuri katika michuano hii ya kombe la dunia ni Misri.

Mwanzo wake umekuwa mwanzo wa mashaka baada ya kufungwa goli moja kwa bila na Uruguay.

Vipi kuna nafasi bado katika kikosi cha Misri?

Nafasi bado ipo kwa sababu katika kundi hili Uruguay na Russia wanaenda kukutana, matokeo ya hii mechi ndiyo yatatoa mwanga mzuri kwa Misri kupita kwenye hili. Mechi hii anatakiwa aombee mmoja kati ya Russia na Uruguay ashinde afu yeye (Misri) ashinde mechi zote mbili zilizobaki.

Kipi kiliwaangusha Misri?

Tatizo walilonalo Misri ni tatizo ambalo timu zote za Afrika zilizocheza katika michuano hii mpaka sasa wanalo. Timu zote hazina njia nzuri za kushambulia kiasi ambacho kinawapelekea washambuliaji wao kuonekana wapweke muda mwingi mwa mchezo.

Kwenye mechi ya Uruguay, Misri hawakuwa na njia mbadala ya kushambulia kupita ukuta mgumu wa Uruguay. Uruguay walikuwa wanabaki watano nyuma wakati wanajizuia, wakati Misri walikuwa wanabaki watatu mbele wakati wanashambulia hivo ilikuwa wachezaji watano wa Uruguay dhidi ya wachezaji watatu wa Misri ( 5 against 3), hivo ikawa ngumu kwa Misri kupata njia za kupenyeza mipira kule mbele.

Kipi walikosa?

Kabla hujamzungumzia Mohammed Salah, unatakiwa pia kuangalia aina ya viungo ambao walikuwa nao Misri. Viungo ambao wanajukumu la kutengeneza nafasi kwa washambuliaji. Hawakuwa na viungo wachezeshaji wazuri ambao wanalikuwa na uwezo wa kutengeneza nafasi nyingi za magoli kwa washambuliaji wao kitu ambacho kilionekana kuwa washambuliaji wao walikuwa wapweke sana kule mbele.

Kipi wanakihitaji ?

Kuna vitu viwili ambavyo vilikuwa vinakosekana katika kikosi cha Misri.

Cha kwanza ni kiungo mchezeshaji wa kutengeneza nafasi za magoli kwa washambuliaji wa timu husika. Misri hawana kiungo mchezajishaji ambaye ni mbunifu, kiungo ambaye atatumia ubunifu wake kutengeneza nafasi nyingi za magoli bila kujali aina ya ugumu wa beki ya timu husika.

Kitu cha pili ambacho Misri wanakihitaji ni kuwa na mchezaji ambaye anauwezo binafsi. Mchezaji ambaye anauwezo wa kuibeba timu nyakati ngumu. Ukiwa na mchezaji kama huyu basi atatumika kama mbinu ya ziada ya timu kupata ushindi.

Ndipo hapa umuhimu wa Mohammed Salah unapokuja, Mohammed Salah mpaka sasa hivi anajumla ya magoli thelathini na tatu (33) aliyoyafunga katika timu ya Taifa, wakati wachezaji wengine waliobaki kwenye timu ya taifa wamefunga jumla ya magoli thelathini na mbili (32) kwa pamoja. Hii inatoa taswira kuwa Mohammed Salah ndiye mtu muhimu katika kikosi cha Misri na ndiye mtu ambaye anaweza kutumika kama mtu wa ziada wa kuikomboa nyakati ngumu.

Upi ubora wa Misri?

Wana ukuta imara, ukuta ambao uliweza kuwadhibiti Luis Suarez na Edison Cavan wachezaji wa kiwango cha juu cha dunia.

Kipi wakifanye ili waweze kupita kwenye hii michuano ?

Kuweza kujilinda vizuri kitimu ni jambo la msingi, lakini ubora hukamilika kipindi pale timu inapokuwa inashambulia pia kwa pamoja. Misri wanatakiwa wabadilike, watimize majukumu yote kwa pamoja kuliko kuonekana timu inamhitaji mtu fulani ili iweze kupata ushindi.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

JOHN OBI MIKEL- ANAIKABA NIGERIA

Tanzania Sports

WALICHOKOSA UJERUMANI, KILIKUWEPO KWENYE BENCHI LA BRAZIL