Menu
in , , , ,

Mikel Arteta ni ubingwa au kuondoka Arsenal

LIGI Kuu England inafika tamati ya dirisha la usajili kwa timu zake zote. Saa chache zimesalia kwa timu kukamilisha usajili wao wenye madhumuni ya kuimarisha vikosi vyao. Arsenal ni miongoni mwa timu ambazo zimefanya vyema katika soko la usajili.  Na bila shaka bajeti kubwa imetokana na kufanya vizuri kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambako fedha zimetunisha akaunti ya klabu. Pamoja na usajili huo, TANZANIASPORTS katika tathmini yake inaonesha kuwa kocha wa Arsenal, Mikel Arteta anakabiliwa na kibarua kigumu cha kubaki klabuni hapo endapo mambo ya yataenda kombo mwisho wa msimu.

Je kwanini nafasi ya Arteta ipo hatarini?

Mikel Arteta bado anadaiwa na Arsene Wenger
Mikel Arteta bado anadaiwa na Arsene Wenger

Kwa muda mrefu klabu ya Arsenal hakuingia sokoni kwa fujo kama ambavyo ikmefanya katika dirisha hili. Wachezaji wapya wamesajiliwa ili kuimarisha kikosi, ushindani na kuhakikisha  wanafanya vizuri kuliko msimu uliopita. Msimu uliopita safari ya Arsenal ilikomea katika hatua ya nusu fainali baada ya kuchapwa na PSG ambao wlaikuja kuwa mabingwa wa Ulaya. Arsenal ilicheza soka la kusisimua na ushindani mkali dhidi ya waliokuwa mabingwa watetezi Real Madrid ambapo waliibuka na ushindi wa jumla wa mabao 3-1. 

Msimu huu na kwa usajili waliofanya ni dhahiri kuwa kocha Mikel Arteta ndiye yupo hatarini. Malengo ya Arsenal ni kuchukua ubingwa wa EPL na mengine yote. Endapo Arsenal itamaliza msimu bila kombe lolote maana yake nafasi ya kocha itakuwa shakani. Mabosi wa Arsenal wamefanya kila kitu muhimu kumpatia zana za kazi ili kuleta ubingwa, na matumaini yao msimu huu lazima wachukue. 

Aina ya usajili wa nguvu uliofanywa na mabosi wa Arsenal unaonesha dalili zote za kuwambia kocha wao “zana hizo hapa, leta ubingwa”. Kwa maana hiyo msimu huu Arsenal watakuwa kwenye mapambano makali ya ubingwa kuliko ilivyowahi kutokea huko nyuma. Mara kadhaa Arsenal walikosa ubingwa dakika za lala salama dhidi ya Manchester City. Mawinga, viungo washambuliaji na washambuliaji ni maeneo ambayo Arsenal imetumia fedha nyingi kuhakikisha ananunua wachezaji wenye viwango. Kazi inayobaki ni kuhakikisha kombe linatua katika kiwanja chao.

Je mashabiki watakubali Arteta kung’atuka?

Kuna wakati kulikuwa na kelele nyingi kuhusiana na kocha Mikel kutoka kwa mashabiki wa Arsenal. Ripoti kutoka vyombo vya habari zilionesha kuwa mashabiki hawakuwa na furaha kutokana na kukosa mataji mara kwa mara. Upo wakati Arsenal ilikuwa inakaribia kutangazwa bingwa wa England lakini ikaajikuta inateleza na kuliacha kombe lipotelee kwa wapinzani. Hata hivyo zipo nyakati ambazo mashabiki wa Arsenal walikuwa na furaha, waliimba kwa shangwe kutokana na kazi nzuri ya kocha huyo. Zipo nyakati ambazo walijikuta wakimpenda Mikel Arteta kwa kuwapa furaha katika mechi mbalimbali. 

Mashabiki na mabosi wa klabu waliamini chini ya Mikel Arteta kila kitu kinawezekana na hivyo wangeweza kunyakua taji lolote. Matumaini yao hayajatimia lakini tathmini inaonesha si rahisi kwa kocha huyo kuchokwa na mashabiki, ingawa msimu huu una dalili zote za kumfungulia mlango wa kutokea.

Je wachezaji watamfukuzisha Arteta?

Usajili uliofanyika unaimarisha kikosi chao, lakini jukumu kubwa la kucheza ni la wachezaji. Ni wachezaji hawa ndiyo wanatakiwa kumtumikia Mikel Arteta na kuhakikisha wanalinda kibarua chake. Kuanzia langoni, mabeki kati na pembeni, viungo, washambuliaji na mawinga wanatakiwa kulinda kibarua cha Arteta. Endapo wachezaji wa Arsenal watapoteana maana yake kazi ya Arteta itakuwa ngumu na kusababisha wamfukuzishe. 

Arteta kumaliza ukame?

Baada ya usajili wa nguvu maana yake klabu inahitaji kombe. Arsenal haijatwaa taji la Ligi Kuu England tangu lilipofanya hivyo mwaka 2002. Chini ya Arsene Wenger Arsenal walikuwa moto wa kutoea mbali na walimaliza msimu bila kufungwa. Hata hivyo kijana wa Arsene Wenger, Mikel Arteta anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuondokana na ukame wa kombe la EPL. 

Mikel anatazamwa kama kocha ambaye anaweza kuibuka shujaa au kusambaratika kabisa ikiwa hatachukua ubingwa wa EPL. Mbaya zaidi itakuwa pale ambapo timu hiyo ikimaliza bila kombe lolote, basi kisu kikali kitapita kwa kocha wa timu na benchi lake lote. Ni rahisi kubaini kuwa endapo watamaliza bila ubingwa ni dhahiri Arsenal watataka fikra mpya kuhakikisha wanalitwaa kombe la EPL. Kazi kubwa itabaki kwa Arteta kupigania kibarua chake kabla hajakutana na rungu.

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

Leave a Reply

Exit mobile version