in , , , ,

Majina ya siri katika usajili wa Arsenal

LICHA ya kutolewa katika hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya, klabu ya Arsenal inamaliza msimu ikiwa imepiga hatua kwenye mashindano hayo na kuvuna kitita kikubwa cha fedha kutokana na kufikia hatua nne bora (nusu fainali). Baada ya kukosa ubingwa wa EPL na UCL, klabu ya Arsenal imeonesha shauku ya kufanya vyema zaidi katika maandalii ya kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu England na mashindano ya Kimataifa. TANZANIASPORTS inafahamu kuwa mipango ya Arsenal imejielekeza kwenye nafasi ya ushambuliaji. Klabu hiyo imetajwa kusaka washambuliaji wawili ambao wana uwezo wa kufunga mabao zaidi ya 25 kwa msimu mmoja hali ambayo itaiweka kwenye mbio za ubingwa ikiwa na idadi kubwa ya mabao. 

Washambuliaji wawili

Arsenal wameweka mezani kwao majina mawili ya washambuliaji wanaofaa kusajiliwa msimu huu katika klabu yao. Majina hayo ni Benjamin Sesko na Viktor Gyokeres ambao ndiyo walengwa wakuu kati ya wachezaji ambao wanatarajiwa kuingizwa kikosini mwao. Dirisha lijalo la usajili limetajwa kwamba Arsenal wamekuwa makini na wameandaa mipango Madhubuti ya kuhakikisha wanasajili washambuliaji hao.  Washambuliaji hao wameonwa kama suluhisho la ukame wa mabao katika kikosi huku wakifuta matumaini ya kumsajili mshambuliaji namba moja wa Newcastle United, Alexander Isak baada ya klabu yake kukataa mpango wowote wa kumuuza nyota huyo Kwenda vilabu vingine. 

Majeruhi wengi

Tanzania Sports

Arsenal wamelazimika kupanga mpango wa kuingia sokoni wakiwa na hasira kutokana na kushindwa kuibuka na idadi kubwa ya mabao msimu unaomalizika. Kwa sasa katika kikosi chao kuna washambuliaji wachache ambapo Gabriel Jesus ndiye anategemewa zaidi, lakini amekuwa majeruhi wa goti tangu Januari mwaka 2025. Hali kadhalika Kai Harvetz naye amekuwa majeruhi tangu mwezi Februari mwaka 2025. Mjerumani huyo hata hivyo sio mshambuliaji kamili ambao anaweza kutegemewa, badala yake anafaa kucheza kama mshambuliaji wa pili yaani namba 10.

Kutokana na kukosekana kwa mshambuliaji, nafasi ya ushambuliaji amekuwa akicheza kiungo Mikel Merino ambaye amecheza mechi nyingi kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa na Ligi Kuu England.

Umri mdogo, nguvu za vijana

Tanzania Sports

Beenjamin Sesko ana umri wa miaka 21, na amefunga mabao 39 katika klabu yake ya Leipzig ya Ujerumani, tayari amecheza mechi 41 za Timu ya Taifa ya Slovenia akiwa amifungia mabao 16 na ana urefu wa futi 6 na inchi 5. Aina yake ya uchezaji inaendana na Arsenal na anatarajiwa kuingia kwenye mfumo kirahisi zaidi. 

Viktor Gyokeres ni nyota anayetikisa katika klabu ya Sporting Lisobn ya Ureno. Ili kumsajili nyota hao, huyo Arsenal watalazimika kulipa kiasi cha pauni Milioni 75 ili kupata huduma yao ama kinaweza kuwa kiasi kidogo zaidi. Ada hiyo hiyo ya uhamisho itakuwa inaendana na kiwango chao cha bajeti ya usajili msimu ujao.

Kipaumbele cha usajili cha Arsenal ni kuwachukua vijana na wenye umri mdogo ambao watajengwa na kutumikia klabu yao kwa muda mrefu zaidi. Arsenal wamekuwa wakimtegemea Gabriel Jesus tangu mwaka 2022 lakini sasa wamekubali kuwa nyota huyo wa Brazil hawezi kutosheleza mahitaji yao klabuni hapo. Ni sababu hiyo Arsenal wapo tayari kusajili nyota hao huku mkurugenzi mtendaji mpya Andrea Berta akiwa anasisitiza na kuweka mkazo katika usajili wa Gyokeres. Usajili wa Viktor Gyokeres mwenye umri wa miaka 26 na raia wa Sweden amepachika mabao 98 katika mechi 100 alizoichezea Sporting Lisbon ikiwemo 38 katika mechi 32 za Ligi kuu nchini Ureno.

Msako wa ziada

Asrenal hawajaishia kwa nyota hao wawili pekee, bali macho yao yameleekzwa kwenye majina ya washambuliaji wengine katika Ligi mbalimbali barani Ulaya. Miongoni mw ani nyota wa Atletic Bilbao, Nico Williams, mshambuliaji wa Wolves Matheu Cunha, Ollie Watkins wa Aston Villa na Joao Pedro. Nyota mwingine ni Hugo Ekitke wa Eintratcht Frankfurt ya Ujerumani. Klabu ya Arsenal ipo katika nafasi nzuri ya kupata faida kimapato kutokana na ushiriki wake kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa, na kwamba wanaingia kwenye dirisha la usajili wakiwa na akiba ya pauni milioni 100 za kufanya usajili.

Tanzania Sports

Ni Dhahiri kutokana na kushindwa kuibuka na taji, Arsenal imebaini idara ya ushambuliaji inahitaji kuongezewa nguvu na kuhakikisha upatikanaji wa mabao unakuwa wa uhakika kuliko hali ya sasa.

Je nani ataingia na mabao?

Usajili wa washambuliaji au wachezaji ni hatua moja, lakini kuleta matokeo ni hatua nyingine. Katika muktadha huo, Arsenal inahitaji washambuliaji ambao wataleta mabao mengi lakini pia wawe na mchango katika kuimarisha timu yao. Mshambuliaji gani anayeingia na nini anachoweza kukifanya kwa maslahi ya klabu ndicho kitu muhimu kinachoangaliwa na benchi la ufundi bila kuvuruga hali ya amani katika kikosi chao.

Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Yanga kufaidika na Ubingwa wa Simba CAF CC!

Tanzania Sports

Carlo Ancelotti kurudisha ufalme wa Brazil?