in , ,

Miaka 80 bila kitu, Yanga ikodishwe?

KWA umri wake, Klabu ya yanga inayo miaka 80 yangu ilipoanzishwa miaka ya 1930. Kwa miaka hiyo ilitakiwa iwe klabu iliyopiga hatua kubwa na yenye misingi ya maendeleo yake.

Tunaposema maendeleo hatuongelei tu kushiriki michuano ya kimataifa, bali tunaongelea namna klabu yenyewe inavyoweza kutwaa makombe, kuwa na rasilimali zake pamoja na mambo yote yanayosisitizwa katika maendeleo.

Kwa mfano, Yanga kwa umri wake haitakiwi kutegemea hisani au ufadhili wa mtu kutoa fedha zake mfukobni, badala yake inatakiwa kuwa klabu inayojiendesha kisasa, iwe na uwanja wake, rasilimali zake na utajiri wa kutosha.

Lakini Yanga hii imebaki kwa muda mrefu ikitegemea fedha za akina Abbas Gulamali, Tarimba Abbasi, Francis Kifukwe, Yusuf Manji, Reginald Mengi na wengine.

Kwahiyo tunaona Yanga inakuwa klabu isiyokuwa na msingi licha ya miaka mingi waliyonayo katika dimba la soka. Miaka 15 iliyopita Yanga ilikataa wazo la akina George Mpondela, Francis Kifukwe na Tarimba Abbas la kubadilisha mfumo wa klabu hiyo na kuwa kampuni.

Miaka imepita na sasa Yanga inaelekea kutaka kubadilisha utaratibu wake kutoka kuendeshwa kwa mfumo wa uanachama hadi kukodishwa na siyo kampuni ya kuendesha.

Timu ikiendeshwa kwa pesa kutoka mfukoni mwa Yusuph Manji na wanachama wachache wenye uwezo kwa zaidi ya miaka kumi sasa,ni jambo la kushangaza kwa timu yenye mamilioni ya mashabiki kuwa tegemezi kwa watu wachache miaka nenda rudi.

Ilipofika Manji hata angejikabidhi timu 100% kimyakimya hamna tofauti na kilichokuwa kinaendelea.

USAJILI WA MAMILIONI

Yanga imesajili nyota kadhaa msimu uliopita na msimu huu. Ni suala la kawaida kusajili wachezaji nyota, lakini je wamerudisha faida? Jibu hapa bado laweza kuwa ndiyo ama hapana.

Kwa mfano kama Yusuf Manji aliwaambia washabiki wa Yanga 40,000 waiingie bure kwenye mechi yao dhidi ya TP Mazembe wkenye Ligi ya Mabingwa, maana yake Yanga ilikosa fedha nyingi za milangoni ambazo wamekuwa wakizitegemea.

Kwahiyo washabiki wa Yanga waliingia uwanja bure kuwaona Donald Ngoma,Obren Chirwa,Thabani Kamusoko ambao bei yao ni zaidi ya milioni 600 mbali ya mishahara wanayolipwa.

Yanga haina mapato ya kumudu gharama hizo, kuanzia maandalizi ya Ligi ya Mabingwa Afrika hadi Kombe la Shirikisho ambako gharama ni zaidi ya bilioni 1, Yanga haina vyanzo vya mapato kupata hiyo pesa.

KUGOMEA FEDHA

1.Yanga imegomea kusaini mkataba wa udhamini wa Ligi Kuu wa Azam Tv ambayo ina haki ya kuonyesha mechi zote za Ligi Kuu Tanzania Bara. Awali Yanga ilidai fedha zilizotolewa na Azam yaani shilingi miliono 100 zilikuwa ndogo. Lakini udhamini wa Azam msimu huu umeongezeka na sasa imeweka kitita cha shilingi bilioni 2, lakini Yanga siyo sehemu ya klabu zinazochukua mgawo wao.

2. uhusiano wa wadhamini wa Yanga yaani TBL haupo kama zamani kwakuwa mechi kadhaa za Kombe la shirikisho walivaa jezi zenye nembo ya QUALITY GROUP. Hii ikiwa na maana TBL wameondoa fedha zao kwa Yanga.

3. Uhusiano wa klabu ya Yanga na shirikisho la soka hapa nchini TFF siyo mzuri kwa namna Fulani. TFF imewaona viongozi wa Yanga kama wasumbufu na wavunjaji wa katiba, lakini vilevuile viongozi wa Yanga wanaliona shirikisho la soka TFF kama linakwanza maendeleo au kuikandamiza klabu yao.

YANGA IKODISHWE?

Hebu tuanze kusema maana ya kukodisha. Ni kwamba hakuna tofauti ya kilichokuwa kikifanyika chini ya uongozi wa Manji kama siyo kukodishwa. Manji ni mwenyekiti, lakini kuamuru washabiki waingie bure maana yake ilikuwa yeye ndiye mwenye uamuzi wa mwisho wa chochote cha kufanya klabuni hapo.

Suala jingine ni namna uchaguzi wa mwenyekiti ulivyofanyika huku wakilumbana na TFF ambayo ilisisitiza kuwa kulikiukwa katiba ya klabu wakati wa uchaguzi huo.

Kinachoendelea sasa Yanga,gharama za uendeshaji wa timu zilikuwa zinatolewa na Yusuf Manji kwa kiasi kikubwa, ina maana kwamba sasa anapewa mamlaka ya yeye kujiongeza zaidi kwa kusaka vyanzo vya mapato kwa kuitangaza vema vema klabu, kufungua vitega uchumi, kubadili sura ya klabu kama kukosa kiwanja, na kushindwa kuuza vifaa vyake.

Kumekuwa na taarifa kuwa Yanga inaendeshwa kihasara. Kwamba Yanga itatumia gharama kubwa kuliko faida inayoingizwa klabuni. Hivyo basi uamuzi wa Yanga kumpa 75% Yusuf Manji ni sawa na ksuema wanachama watapata asilimia 25 tu ya mapato ya klabu.

NI MWENYEKITI AU MWEKEZAJI?

Jambo linaloshangaza hadi sasa ni namna Yanga inavyoendesha mambo yake. Ukweli ni kwamba anayeomba kukodishwa timu hiyo ni Yusuf Manji ambaye ni mwenyekiti wa klabu ya Yanga.

Kwa maana hiyo inaleta mgogoro wa kimaslahi baina ya Mwenyekiti na Mwekezaji anayetaka asilimia 75 za kukodishwa. Njia rahisi ilitakiwa kuachia uaenyekiti kwanza kabla ya kuomba kukodi klabu hiyo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Naziangalia timu za EPL kwa ufupi..

Tanzania Sports

SIMBA ina thamani ya Bilioni 20?