in , ,

SIMBA ina thamani ya Bilioni 20?

MABINGWA wa zamani wa Soka nchini, klabu ya Simba ipo kwenye mchakato wa kupata mwekezaji mpya, Mohammed Dewji au maarufu kama MO Dewji.

Katika msimu wa mwaka 2003 Mo Dewji akiwa mdhamini wa klabu ya Simba ilifanya vema kwenye mashindano ya kimataifa ikiwemo kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ilikuwa hatua nzuri kwa klabu ya Simba ambayo inazo rekodi mbalimbali za kufanya vizuri kimataifa. Vilevile Mo Dewji ni mdau mkubwa wa soka hapa nchini akianzia klabu ya Singida United, na baadaye African Lyon ambayo aliinunua kutoka Mbagala Market.

Hata hivyo hakufanikiwa kutamba nazo hizo timu. Hivyo alijiweka kando kwenye masuala la soka na badala yake akajielekeza kwenye masuala la ubunge ambapo alichaguliwa kuwa mbunge wa Singida Mjini kwa kipindi cha miaka mitano(2010-2015).

THAMANI YA SIMBA

Mo-Simba sports
Mo-Simba sports

Hata hivyo suala la klabu ya Simba kuuza hisa zake ndilo linaloleta mjadala. Simba inao mpango wa kuuza hisa au kumuuzia Mo Dewji kwa shilingi bilioni 20.

Mpaka sasa suala kubwa linalotakiwa kupatiwa ufafanuzi ni jinsi ambavyo thamani ya klabu ya Simba inaweza kufanyiwa ili kuona kama inastahili kuuzwa kwa bilioni 20.

Ni dhahiri hadi leo Simba haijawahi kufanya tathmini juu ya thamani yake. Hapakuwahi kufanywa tathmini ya thamani ya klabu hivyo kukadiria bilioni 20 za Mo Dewji ina maana kwamba wanachama hawajui thamani halisi ya timu yao.

Tuchukue mfano huu timu ina wanachama takribani milioni 1 tu. Ada ya uanachama wa Simba iwe shilingi 10,000 kwa mwaka. Halafu mapato janakuja kupatikana au kuwa sawa na shilingi 10,000,000,000 yaani bilioni 10 kwa mwaka.

Hizo ni hesabu rahisi tu. Klabu imetumia nguvu gani kuwafikia wanachama wake kiasi cha kusema thamani ya hisa zao 51% ni bilioni 20? Ni lini viongozi wa Simba walitumia ya kuwabadili mashabiki kuwa wanachama hai na wenye kuichangia timu kupitia fedha zao moja kwa moja kwa kununua kadi?

Pengine tuseme siyo jambo baya kwa Mo Dewji kuuziwa timu lakini sio kwa yeye kujipangia bei ya shilingi bilioni 20 na kuhitimisha kuwa ndiyo thamani ya Simba katika hasia 51%

Kla ya Simba inatakiwa kufanya mchakato wa tathmini ya thamani yake halisi iwapo itaendeshwa kama kampuni basi watu wanunue hisa au ijitathmini thamani yake halisi kisha masuala ya kuingia mkataba wa kuuza hisa zake yaanze.

Vilevile Simba wanatakiwa kutangazwa zabuni ili watu washindane lakini kuendelea kusubiri uamuzi wa bei ya Mo Dewji na kwamba ndiyo kiini chao cha kuuza hisa ni kujinyima thamani halisi ya klabu yao.

Kwa mfano Simba inao wanachama wanaolipia uanachama kwa shilingi 1,000 hata ukiwauliza thamani ya uanachama huo katika timu imeleta vipi ufanisi utasikia mashabiki ni muhimu.

Ni lazima washabiki wa Simba wawe chachu ya ufanisi kabla ya kufikiria kuuza hisa. Mwisho niwakumbushe, ni lazima Simba ijiwekee kiwango cha tahamani ambacho Mo Dewji atatakiwa kukinunua sio Mo Dewji kuwawekea wao bei yake ya bilioni 20 huku wenye timu wakiaanza kutetemeka.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Miaka 80 bila kitu, Yanga ikodishwe?

Tanzania Sports

Arsene Wenger : Maswali magumu