in ,

Messi: Pigo kwa EPL

Lionel Messi

Kuna watu watafurahika kutokana na Ligi Kuu ya England (EPL) kuponyokwa na nyota mwingine aliyekaribia kutua.

Huyo ni nahodha na mshambuliaji maarufu wa Barcelona na Timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi ambaye majuzi ametikisa kiberiti kutaka kuondoka Katalunya.

Ile tetesi kutokea tu, tayari baadhi ya klabu za EPL, hasa Manchester City, zikanyanyua macho, masikio na mikono, tayari kuvunja benki na kufanya usajili wa kihistoria, lakini iwapo ataamua kubaki Hispania, basi litakuwa pigo jingine.

Mlinzi wa Liverpool, Andy Robertson atakuwa mmoja wa wafurahiaji, kwani alitamka wazi kwamba hamtaki kokote karibu na EPL, beki huyo wa kushoto akionekana kuwa mkweli. “Simtaki kokote karibu na EPL,” akasema akiwa amekunja uso.

Itakumbukwa kwamba mwaka jana Liverpool walifungwa 3-0 na Barcelona wa Messi kwenye mechi ya nusu fainali mkondo wa kwanza, lakini wakaja kugeuza meza kwa kuwafunga Barcelona 4-3 kwenye mechi ya mkondo wa pili na kusonga mbele hadi kutwaa ubingwa wa Ulaya kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL).

Lionel Messi
Lionel Messi

Hapana ubishi juu ya makali ya Messi hata hivyo, japokuwa Robertson anadai haogopi ‘ubaya’ atakaofanya Messi kwa Liverpool bali kwa klabu nyingine za EPL. Huenda sasa tutakosa wasaa wa kumaizi jinsi Messi angezoea mazingira ya hapa England – baridi kali, upepo, unyevunyevu na mengineyo hasa kama akienda kule Stoke City au angefanya kipi akikutana na timu kama Burnley au Sheffield United, japokuwa tungeweza kuhisi.

Licha ya umri wake mkubwa wa miaka 33, Messi angekuwa kivutio kikubwa EPL, macho ya wengi ndani na nje ya nchi yakimwelekea anavyosakata gozi la ng’ombe, kukokota mpira vyema, kupiga chenga nyingi zikiwamo za maudhi na mwisho kabisa aina ya mabao anayotundika kambani.

Kwa namna yoyote ile, habari ya Messi kuja EPL ilionekana kubwa na ngumu kukubalika kuwa ya kweli, lakini Man City walikuwa wamepewa moyo mkuu kwamba mambo ni mazuri na wangempata ‘mtu wao’.

Hii ilitokana na Messi kukosana na waajiri wake, ikiwa ni pamoja na kocha aliyefukuzwa kazi muda mfupi baada ya Barcelona kuchabangwa 8-2 na Bayern Munich kwenye UCL, wakasonga hadi kutwaa kombe hilo mwaka huu. Messi alishadai tangu mwanzo kwamba kocha na uongozi wa klabu walikuwa wakiwapeleka siko, wakapoteza na ubingwa wa Hispania kwa mahasimu wao – Real Madrid.

Etihad watachukia kumkosa, lakini si habari za kushitua, kwani ni wachache waliofikia hata kufikiri tu, kwamba Messi angeondoka Barca. Huyu ni mchezaji kutoka ‘sayari’ nyingine, aliyejikita Katalunya, kupata heshima kubwa na kutwaa Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka – Ballon d’Or  mara sita.

Kw muda mrefu, kibinafsi na kitaaluma, ilionekana tangu kitambo kuwa ni vigumu kuvunja bondi iliyokuwapo baina ya Messi na Barcelona wenye makao makuu yao Camp Nou. Alipata kusema, hata hivyo, kwamba alikuwa makini akitaka kuondoka, kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine katika kazi yake na kumaliza akiwa juu kabisa kisoka.

EPL ilipata kuwa na nyota kama Cristiano Ronaldo, ambaye, Gary Neville anadai kwamba aliondoka kwa sababu ya hali ya hewa ya baridi kali, hasa kuanzia Novemba. Kwamba EPL ina mvuto mkubwa kwa wachezaji wengi kwa ushindani wake na umaarufu kama ligi kuu maarufu zaidi duniani, ila tatizo ni hali ya hewa.

Ronaldo aliwashangaza watu kwa kuondoka ghafla Real Madrid na kwenda Italia – Juventus, na hili la Messi lilipoanza kusanuka, watu wakaona kama ni mwelekeo ule ule. Rais wa Argentina alimwita Messi na kumtaka arudi nyumbani akamalizie soka yake kwenye klabu ya utineja wake ya Newell’s Old Boys.

Baadhi ya wachezaji wakubwa zaidi kusajiliwa na klabu za EPL ni Yaya Toure, Cesc Fabregas na Alexis Sanchez (ambao hawakuwa wakihitajika tena Barcelona), Angel Di Maria na Mesut Ozil (hawakuhitajika Real Madrid) na Sergio Aguero na David Silva ambao kule Atletico Madrid na Valencia mtawalia walikuwa wakitakiwa na Barca na Real.

Tanzania Sports
Messi akiwa uwanjani

Zlatan Ibrahimovic alijiunga na Manchester United kiangazi cha2016, lakini alikuwa na umri wa miaka 34. United pia walivunja rekodi kumsajili Paul Pogba kutoka Juventus 2016, lakini pia halikuwa dili lililokosesha watu usingizi kule Barcelona au Madrid au Turin, Italia kwa Juventus waliomtoa.

Wacheaji wawili wakali zaidi wa kizazi kilichopita – Zinedine Zidane na Ronalso ‘original’  hawakupata kuwa karibu na kujiunga na klabu yoyote ya EPL, kwa hiyo waliiponyoka, leo hii fursa ya EPL kumpata Messi na kuiongezea thamani nayo ni kama imekuwa ndoto ya alinacha.

Basi, bila Messi katika EPL, kuna vipaji vingine vya wachezaji wadogo vimekuja kama Ferran Torres wa Manchester City, Donny van de Beek wa Manchester United, Kai Havertz, Hakim Ziyech na Timo Werner wa Chelsea. Hawa ni wachezaji wanaoonekana wazi kwamba watastawi na kuwa wakubwa kwa muda mrefu ujao.

Messi angetikisa hapa, lakini ingekuwa kwa muda mfupi, kama miaka miwili hivi au sanasana mitatu na hakika walinzi wa timu pinzani na ambayo angejiunga, hawangependezwa kama alivyosema Robertson, kwani angewapa hali ngumu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Simba

VPL: Simba ni Moto, Yanga Yapooza..

VPL mechi za ufunguzi

VPL: Rekodi ya Sabiyanka haijavunjwa