in , , ,

MBAO FC KUFUTA UTEJA DHIDI YA KLABU ZA DAR BAADA YA MIAKA 16 ?

Katika miaka 16 ni timu mbili pekee nje ya Dar es salaam zilizowahi kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa.
Mbao FC ya Mwanza, wanaitaji kushinda mechi ya fainali Kombe la FA dhidi ya Simba ili wajipatie tiketi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya kimataifa.

Mbao ilifanikiwa kutinga fainali ya michuano hiyo ya FA inayodhaminiwa na Azam baada ya kuifunga Yanga bao 1-0 kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Na endapo ikitokea Yanga wakateleza kwenye Ligi Kuu na kushindwa kutetea taji lao, Mbao Fc watakuwa wamepata tiketi ya kwenda michuano ya shirikisho Afrika hata kama wakipoteza mchezo wa fainali dhidi ya Simba.

Kwa miaka 16 sasa klabu za Dar es salaam Yanga, Azam, Simba ndizo zimekuwa zikiwakilisha nchi kwa kupokezana tu karibu kila mwaka, katika miaka hiyo 16, ni timu mbili pekee nje ya Dar es salaam zimefanikiwa kushiriki michuano ya kimataifa.
Kama ilivyo ada,makala hii inakuletea timu zilizowahi kuiwakilisha nchi mbali na Simba, Azam na Yanga kwa miaka 16 nyuma.

TANZANIA PRISONS

Prisons kutoka Mbeya ndiyo klabu ya mwisho kuiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa mbali na klabu za Azam, Simba na Yanga mwaka 2009.
Wameshiriki michuano hiyo mara tatu, klabu bingwa mara moja mwaka 1999 waliishia hatua ya awali kwa kuenguliwa na Ferroviario Maputo ya Angola, 2005, 2009 kombe la shirikisho na kuishia hatua za mwanzoni kwa kutolewa na USCA Foot 2005 na 2009 Khaleej Sirte.
MTIBWA SUGAR

Mara yao ya mwisho kwenye michuano ya Afrika ni mwaka 2004, Mtibwa walifanikiwa kuvuka raundi ya awali kwa kuwaondosha klabu ya Chemelil ya Kenya kwa jumla ya magoli 4 kwa 1 na kutinga hatua ya 32 bora.
Katika hatua 32 walipangiwa na Santos ya Afrika kusini na mchezo wa mwanzo Mtibwa Sugar walipoteza kwa magoli 3 kwa bila na katika mchezo wa marudiano Wakata miwa hao waliingia mitini hawakwenda kucheza mechi ya marudiano.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

JUVENTUS NA REAL MADRID WANA 60% YA KWENDA CARDIFF

Tanzania Sports

HATIMAYE ARSENE WENGER AVUNJA MWIKO