Mabosi wa soka wametuma ujumbe mzito serikalini kupitia kikao kati ya wasimamizi wa Ligi Kuu England, chama cha soka FA na wadau wa Ligi Kuu walipokutana na Waziri wa mambo ndani,habari,utamaduni na michezo mapema jumatano wiki hii, Oliver Dowden, kuomba kibali mashabiki waruhusiwe kuingia viwanjani haraka iwezekanavyo kabla ya mambo hayajaenda kombo kwa vilabu na wadau wa ligi hiyo.
Timu za Ligi Kuu zimecheza mechi bila mashabiki wao tangu mwezi Juni mwaka huu zikiwa na matumaini kuwa angalau robo ya mashabiki wao watarejea viwanjani kuanzia tarehe 1 mwezi Oktoba, lakini mipango yote imeenda kombo baada ya wiki iliyopita waziri mkuu Boris Johnson kutoa ripoti ya mrejesho juu ya hali ya mambukizi ya ugonjwa wa corona nchini England na kusisitiza kuwa watu wanatakiwa kuendelea kuzingatia kanuni ya kuepuka mikusanyiko mahala popote wanapokutana.
Waziri Johnson alisema hayo baada ya matokeo ya vipimo kuonesha hali ya maambukizi imefika kwa watu 1000 tangu ulipoanza mwezi Spetemba mwaka huu. Waziri huyo ameonesha hofu juu ya mkusanyiko na kusisitiza uwezekano wa kuwaruhusu angalau mashabiki 10,000 viwanjani huenda ukachochea maambukizi zaidi.
“Tunatakiwa kuwaruhusu mashabiki waingie viwanjani au klabu ziingie kwenye matatizoni. Ni rahisi kuelewa, klabu zinataka asilimia fulani ya mashabiki waruhusiwe kuingia uwanjani lakini inakisiwa huenda ikaongeza kiwango cha maamumbikizi,” alisema Mark Catlin, Ofisa Mtendaji wa klabu ya Portsmouth inayocheza daraja la kwanza.
Catlin aliongeza kwa kusema, “Endapo mambo yataendelea kuwa hivi yalivyo sasa, itasababisha matatizo ya kiuchumi kwa klabu za Uingereza. Kiasi kikubwa cha fedha zilizotumika kwenyeklabu mbalimbali miezi sita iliyopita ni mkopo wa awali. Hakuna vyanzo vingine vya mapato. Serikali inatakiwa kusaidia sekta ya michezo katika hali kama hii kama ambavyo ilisaidia sekta zingine mfano maeneo kama mikahawa na hoteli kuwa na punguzo la asilimia 50 kuanzia jumatatu hadi jumatano Agosti 3 hadi 31, lakini hatujaambulia kitu. Tumefanya kila jitihada kuwa tayari kuanza ligi ili kufikia malengo, lakini sasa tunadidimia. Nafahamu kuwa hali haijafika chini kabisa, lakini huenda ikatokea klabu kuporomoka kama majengo ya bweni,”
Tanzaniasports imeambiwa na baadhi ya maofisa wa Ligi Kuu England kuwa kusuasua hali ya kiuchumi miongoni mwa vilabu ambao wanasisitiza kuwa kuhofia maambukizi kutokana na watu 1,000 haithibitishi kuwa hali itakuwa mbaya. Mtazamo huo umekwenda sambamba na barua ya wasimamizi wa Ligi kuu kwenda serikalini mwishoni mwa wiki iliyopita kuelezea hali ya mwelekeo wa usafiri.
Ofisa mmoja wa Ligi Kuu ambaye hakuwa tayari kutajwa jina lake amesema, “Endapo hali hii itaendelea kwa muda, tunaweza kuona vilabu vikifutika katika ramani ya soka. Kwa vilabu vya nje ya Ligi Kuu England hali hiyo inasababisha kyumba kwao. Hakuna mapato ya Televisheni, hakuna mapato ya mechi,hakuna mapato bila mechi, na halafu vilabu vina mikataba na wachezaji na viongozi wengine wanaotakiwa kulipwa mishahara yao. itafika mahali soka la kulipwa litapata matatizo, na niwe mkweli sio mbali sana kutoka sasa tutasikia matatizo hayo. Hali ni mbaya, hakika ni mbaya mno,”
Hata viongozi wa vilabu wanahofia matokeo ya hali iliyopo sasa endapo serikali itashikilia msimamo wake wa kuzuia mashabiki wasiingie uwanjani, itakuwa hasara na wateja wataanza kuondoka.
“Bajeti yetu imendeshwa bila kutegemea mashabiki mwishoni mwa msimu uliopita. Mashabiki wanachangia tusinunue wachezaji lakini tumevurugwa mno, hata kama tunatamani kuendelea na mashindano hilo linatokana na sapoti ya wamiliki chini ya makubaliano maalumu kati yetu. Baadhi ya vilabu vilianzakuuza tiketi za msimu mpya mwishoni mwa msimu uliopita, zimeuza karibu elfu kumi hadi elfu kumi na mbili, lakini sisi tulianza kuuza tiketi zetu wiki moja iliyopita kwa asilimia ishirini hadi thelathini. Kama hatuwezi kuuza zaidi, na wasiruhusiwe kuingia viwanjani tutalazimika kurejesha fedha za mashabiki wetu. Hata hivyo kuna timu zimeshatumia fedha za mauzo ya tiketi, zitafanyaje kwa sasa? Hilo ndio la msingi,” anasema Peter Ridsdale, mshauri wa mmiliki wa timu ya daraja la kwanza ya Preston North End, Trevor Hemmings.
Mwenyekiti wa klabu ya Tranmere Rovers, Mark Palios anasema, “Sina matumaini kama mashabiki wanarejea viwanjani haraka, itatumiiza sana, lakini afadhali kupata kidogo kuliko kukosa kabisa,”
Palios, ofisa mtendaji wa zamani wa Ligi kuu, anaelezea hali za vilabu vingine vilivyoko Ligi moja na Tranmere na Ligi daraja la pili ambazo zimelazimika kuchukua mikopo ya ziada ili kuwalipa wachezaji, ikiwa na maana wanatumia pauni 30,000 kwa wiki kwaajili ya wachezaji pekee.
Takwimu zinaonesha kuwa timu zinapata mapato takribani pauni milioni moja na laki sita kupitia mauzo ya tiketi na mapato mengine kiasi cha pauni laki saba na elfu hamsini yanapatokana na mauzo ya vyakula,vinywaji na vitu mbalimbali siku ya mechi.
Tranmere imeuza tiketi elfu tatu za msimu huu, lakini inatarajia kurejesha ifikapo mwezi desemba endapo mashabiki hawataruhusiwa kurejea viwanjani. Upo uwezekano wa kupata hasara ya pauni laki mbili, hali ambayo ingekwua tofauti kama wangepata amshabiki angalau asilimia 33 tu kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
Tanzaniasports imeambiwa na mabosi wengi wa vilabu vya England kuwa hawana matumaini kwa sasa kutokana na nakisi ya fedha ambazo zilitokana na mauzo ya tiketi, na hawajui wataziba vipi pengo hilo. Hata hivyo wameihakikishia Tanzaniasports kuwa upo uwezekano wa mashabiki kurudi viwanjani msimu wa 2021/2022, hivyo kwa wakati huu vilabu vinabeba mzigo mkubwa wa gharama za uendeshaji.
Wamiliki wa vilabu nao wanasubiri muda ambao mashabiki watarudi viwanjani bila kuvaa barakoa, wakiwa tayari kushangilia,kuimba nyimbo,kunywa,kula na kupiga gumzo bila hofu ya kuambukizana corona.
“Siwezi kuhamasisha mashabiki waje viwanjani kwa sababu sina taarifa za kutosha kuhalalisha mwito. Mashabiki warudi kukiwa na hali ya usalama, sio kwa sababu za kukusanya fedha kutoka kwao. Haileti maana kulazimisha mashbiki warejee viwanjani mapema wakati bado wapo karantini, inaweza kuwa mbaya zaidi kiuchumi na kiafya. Nina mashaka, tunataka kusababisha matatizo wakati tupo katikati ya kupata kinga ya ugonjwa huo. Vilabu vimepata hasara kiuchumi, naunga mkono wao kupata fedha ila sio kuharakisha mashabiki,” anasema Accrington Stanley, mmiliki wa wa Andy Holt.
Vilabu vimeepuka kutoa ofa za mishahara mikubwa kwa wachezaji wala mikataba minono zaidi. Tanzaniasports inafahamu baadhi ya vilabu vya Ligi Daraja la Kwanza vitatoa kiasi cha pauni elfu tatu kwa wachezaji wa kulipwa kwa wiki ikiwa hakutakuwa na fedha za viingilio na watalipwa pauni elfu moja ikiwa msimu utasimamishwa.
Hata hivyo inajulikana pia vilabu vya Ligi Kuu na Ligi daraja la kwanza zimeshinikizwa kucheza mechi bila mashabiki licha ya kupata hasara ya mamilioni ya mapato. Hata vilabu tajiri viliweka wazi wiki iliyopita kuwa vitakuwa tayari kucheza mechi bila mashabiki.
Hivi karibuni rais wa Chama cha vilabu vya Ulaya (ECA) na mwenyekiti wa Juventus, Andrea Agnelli alizungumzia jambo hilo kwenye mkutano wa baraza la vilabu.
“Kama kuna jambo la kutuuganisha, ni vilabu vikubwa, kati na vidogo, ambavyo vina viwanja kuamua kuwakosa mashabiki au kuwa nao. Tumejeruhiwa na hii hali. Vilabu kote duniani vimepata hasara ya pauni bilioni tatu na laki saba.
Siku chache baadaye Ofisa Mtendaji wa Ligi kuu, Richard Masters alisema, “Vilabu vimejiandaa, vipo tayari kuendelea kupima wachezaji na kusimamia mpango wao wa kuwahitaji mashabiki kuanzia tarehe moja mwezi Oktoba mwaka huu kama vitapewa ruhusa na serikali.
Serikali ipo katika mchakato wa kutekeleza vipimo kwa njia za kisasa, pamoja na kuandaa hati za taarifa zitakazoruhusu kumbi za starehe na burudani kurejea katika hali ya kawaida. Masters amesema vilabu vimekubaliana lazima kudhibiti idadi ya mashabiki na kwamba watakuwa asilimia 25 hadi 30. Hali hiyo itashuhudia vilabu vikipoteza mapato zaidi ya pauni milioni 540, ambapo msimu uliopita walipata hasara ya pauni milioni mia saba.
Klabu ya Brighton & Hove Albion ilipocheza dhidi ya Chelsea imefanya majaribio ya kuingiza mashabiki 2,500 uwanjani. Tottenham Hotspur, inatoa nafasi ya mashabiki 8000 kwenye mchezo dhidi ya Everton, huku ikiwa na mipango ya kuruhusu mashabiki 31,000 au nusu ya mashabiki uwnajani kuanzia mwezi ujao.
Comments
Loading…