in ,

Manchester United watwaa Kombe la FA

Manchester United wametwaa Kombe la FA baada ya mchuano mkali na
Crystal Palace kwenye dimba la Wembley.

Hii itakuwa ni furaha kwa kocha Louis van Gaal japokuwa hiyo
haimaanishi kwamba ana uhakika wa kubaki kocha msimu ujao, kwani bado
kuna taarifa kwamba wakati wowote watamtangaza Jose Mourinho kuwa
kocha hapo Old Trafford.

Alikuwa ni Jesse Lingard aliyewamaliza Palace with an extra-time
screamer to win Manchester United the FA Cup katika dakika za
nyongeza, akiwa ameingia badala ya mfungaji wa bao la kwanza, Juan
Mata.

Lingard alikutana na mpita wa Antonio Valencia na kufyatua kombora
lililokwenda kwenye kona ya juu ya lango, akiwainua maelfu ya
washabiki wa Man U vitini. Jason Puncheon alifunga bao zikiwa zimebaki
dakika 20 za muda wa kawaida, akimzidi maarifa kipa David De Gea
lakini Mata akasawazisha kwa kupokea mpira wa Wayne Rooney dakika tatu
baadaye.

Mwamuzi alikuwa Mark Clattenburg – anayechukuliwa sasa kuwa bora zaidi
England, na pia amechaguliwa kuwa mwamuzi kwenye mechi ya fainali ya
Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) baina ya Real Madrid na Atletico Madrid
jijini Milan, Italia Jumamosi ijayo.

Man U wanachukua kombe hilo ambalo kwa misimu miwili mfululizo
lilinyakuliwa na Arsenal ambao msimu huu walitupwa nje na timu ndogo
ya Watford, lakini walio pia katika Ligi Kuu ya England.

Habari zilizopo ni kwamba Mourinho anaweza kutangazwa kuwa kocha mpya
Old Trafford wakati wowote, hatua inayochukuliwa kujibu mapigo kwa Man
City kumtangaza Pep Guardiola kuwa kocha wao badala ya Manuel
Pellegrini.

United wanaamini kwamba Mourinho ataweza kuweka ushindani kuliko LVG
ambaye amekuwa akilaumiwa kwa mtindo wake wa kuchezesha. Hata hivyo
amebakiza mwaka kwenye mkataba wake, hivyo United watatakiwa kumlipa
fidia ikiwa watamtema, japokuwa zipo habari zisizothibitishwa kwamba
anaweza kuwa mkurugenzi wa soka.

Inaelezwa kwamba dili la kumchukua Mourinho lilikubaliwa hata kabla ya
mechi hiyo ya fainali, baada ya kushindwa kufuzu kwa UCL chini ya
kocha huyo, ndipo wakuu wakaona kwamba kuna haja ya kufanya
mabadiliko. Mourinho hana kazi tangu Desemba mwaka jana alipofukuzwa
na Chelsea baada ya kuanza vibaya ligi.

LVG katika mkutano wake na wanahabari baada ya mechi, alikataa
kujadili hatima yake, akisema kwamba inatosha kuwaonesha kombe kwa
sababu tayari ni wanahabari hao hao ‘waliomfukuza’ miezi sita
iliyopita.

“Nimeshawaonesha kombe, sitaki kujadili hilo na rafiki zangu wa vyombo
vya habari ambao walishanifukuza miezi sita iliyopita. Natumaini
kuwaona tena (msimu ujao), sitaki kuongelea suala la kuondoka klabuni
hapa,” akasema.

Mdachi huyu alitumia pauni milioni 250 kununua wachezaji wapya lakini
hawakufanya vyema mchezoni, kiasi cha kubadili wachezaji mara kwa mara
hadi majuzi alipokuja kuwang’amua akina Marcus Rashford na Anthony
Martial aliowatumia kwenye ushambuliaji kulikokuwa butu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

FAINALI YA KOMBE LA FA:

Tanzania Sports

Mourinho huyoo Man United