in , ,

MANCHESTER UNITED TUSIIPUZE , TUKAIDHARAU.

*Kuna kosa ambalo Manchester United walikuwa nalo msimu uliopita*

Walikuwa wanatengeneza nafasi nyingi sana za magoli lakini walikuwa wanatumia chache.

Kitu ambacho kiliwafanya wasiwe wapinzani halisi wa ubingwa msimu uliopita.

Jose Mourinho alikaa akaona hilo lilikuwa tatizo kubwa.

Tatizo ambalo lilimfanya asiweze kufikia nchi ya maziwa na asali.

Hakuruhusu tena msimu huu aonje radha ya uchungu wakati ulimi wake uliumbiwa sukari.

Kila muda hutamani utamu kichwani mwake ndiyo maana akawa kocha mwenye mafanikio makubwa.

Kocha anayefikiria kikombe kila muda, kwake yeye njaa ya kubeba vikombe haijawahi tibika.

Ndiyo maana muda wote hufikiria kutengeneza jeshi imara, jeshi ambalo ƙlitamsaidia kwa kiasi kikubwa kufikia mafanikio makubwa.

Ndiyo maana ilikuwa sababu ya yeye kuwaleta kina Lukaku , Lindelof pamoja na Matic.

Watu ambao wanatengeneza jeshi ambalo Jose Mourinho hulihitaji kusimamisha ufalme wake.

Ufalme ambao msimu uliopita ulishindikana kwa sababu ya kushindwa kutumia nafasi nyingi walizokuwa wanatengeneza.

Lakini msimu huu ni tofauti , mechi mbili wana magoli nane.

Waweza kuona ni kitu cha kawaida sana lakini kina nguvu ya kutoa dira ya wapi wanakotaka kuelekea.

Mwanzo wao unaonesha ramani ya kipi wanachokitaka kukijenga.

Wamefanikiwa kutoruhusu goli hata moja katika mechi zote mbili, ukuta wake ni imara na hii ni kawaida kwenye timu ya Jose Mourinho.

Ukuta ambao umechagizwa ugumu wake na Nemanja Matic.

Ambaye amekuwa mtu anayelinda mabeki vizuri na kukaa eneo ambalo linampa nafasi Paul Pogba kusogea mbele na kuweza kuisaidia timu kutengeneza nafasi na kufunga kitu ambacho msimu uliopita hakikuwepo.

Usambazwaji wa mipira kutoka eneo la kati kwenda eneo la mbele unakuwa wa kiasi kikubwa, hali ambayo kina Henrikh Mkhitaryan inawafanya wawe na mipira mingi bila wao kusogea mara nyingi katikati ya uwanja kuchukua mipira.

Na hapa ndipo wanapokuwa na nafasi ya kutengeneza nafasi nyingi za magoli na kufunga.

Lukaku ameongeza kitu kimoja ambacho msimu uliopita Zlatan hakuwa nacho, ana speed kuliko Zlatan.

Speed ambayo inampa uhuru wa kujipanga akae eneo lolote la mbele na kukokota mipira vizuri. Pia amekuwa akitumia nafasi vizuri tofauti na Zlatan ambaye alikuwa anatumia nafasi chache kwenye nyingi alizokuwa anapata.

Kuhusika kwa wachezaji wengi katika ufungaji wa magoli ni kitu ambacho hakikuwepo kwa muda mrefu kwenye kikosi cha Jose Mourinho.

Katika magoli 8 wamehusika wachezaji wanne ambao ni wastani wa goli 2 kila mechi kitu ambacho kinaleta mgawanyo mzuri wa ufungaji wa magoli.

Msimu uliopita kuna baadhi ya wachezaji kama Henrikh Mkhitaryan hawakuwa kwenye kiwango chao kikubwa lakini msimu anaonekana yupo kwenye kiwango chake kizuri, mechi mbili ana pasi nne za mwisho.

Hamasa ya ushindi ndani ya wachezaji ni kubwa ndiyo maana kila mchezaji anayetokea benchi anaonesha mabadiliko.

Anaonesha timu inataka ushindi, na ushindi huletwa na mtu yoyote kwenye timu ndiyo maana Martial amekuwa akiingia na goli lake.

Kitu ambacho kinampa kocha mbadala wa kubadilisha kila anapoona timu imeelemewa sehemu fulani na inahitaji mtu wa kusahihisha sehemu waliyoelemewa

Kitu ambacho kinaonesha msimu huu kuna kitu ambacho wamekipania na hatutakiwi kuwabeza kisa wamecheza na Swansea pamoja na Westham.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Kuna mgogoro unapikwa Chelsea

Tanzania Sports

USHINDI WA CONTE ULIKUWA BAHATI AU UWEZO ?