in , , ,

Manchester City hoi kwa Cardiff


*Spurs waponea tena kwa tuta

Klabu iliyopanda daraja msimu huu ya Cardiff City imewaduwaza Manchester City kwa kuwagawia kichapo.

Wakicheza mbele ya mashabiki wao, Cardiff wanaofundishwa na Malky Mackay walifanikiwa kuwabana vijana wa Manuel Pellegrini kwa kuwachabanga mabao 3-2.

Ilikuwa shamrashamra kubwa katika klabu hiyo ya Wales, licha ya Edin Dzeko kuanza kucheka na nyavu katika dakika ya 52 kabla ya Aaron Gunnarsson kusawazisha kwa kumshinda kipa Joe Hart aliyekuwa ametangulia kupangua shuti la mshambuliaji wa Cardiff Fraizer Campbell.

Alikuwa mshambuliaji huyo aliyepeleka kilio Etihad kwa kufunga mabao mawili mazuri, licha ya Alvaro Negredo kujitahidi na kufanikiwa kufunga bao la pili, lakini likawa la mwisho na Cardiff wakamaliza mechi kwa ushindi ambao haukutarajiwa na wenyeji waliushangilia sana.

Katika mechi nyingine, Tottenham Hotspur walifanikiwa tena kuibuka na ushindi wa penati dhidi ya Swansea kama mechi ya awali, kwa mchezaji wake mpya, Roberto Soldado kupachika bao la nne kwa msimu wake huu ulioanza vizuri.

Penati hiyo ilitiwa kimiani na Soldado baada ya mchezaji wa Swansea, Jonjo Shelvey aliyechezea Liverpool msimu uliopita kumchezea vibaya Andros Townsend.
Swansea walijitahidi kupata bao, ambapo walikosa nafasi kadhaa, ikiwa ni pamoja na mpira wa kichwa wa mlinzi wao, Ashley Williams kugonga mwamba.

Kocha Andre Villas-Boas alifurahishwa na ushindi huo mwembamba na namna ulivyokuja, huku winga wake wa kimataifa, Gareth Bale akitarajiwa kuiondoka klabu hiyo na kujiunga na Real Madrid.

Baada ya mzunguko huu wa pili, ambao hata hivyo ni mapema mno kuainisha jedwali la msimamo wa ligi, ni kwamba Chelsea wanaongoza, wakifuatiwa na Liverpool, Spurs, West Ham, Southampton, Man City, Man United,Arsenal, Aston Villa na Stoke.

Nafasi za tatu za mwisho zimeanza kushikwa na Swansea ambao wamefungwa mechi zote mbili za mwanzo sawa na Crystal Palace wakati Newcastle wanaangukia huko kwa kutoka sare mechi moja na kufungwa moja.

Jumatatu hii kuna kivumbi kwa mabingwa watetezi, Manchester United kukipiga na Chelsea katika dimba la Odl Trafford.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Arsenal, Liverpool watakata

MAANDALIZI MKUTANO WA UCHAGUZI TFF