*Chelsea wazinduka, Mourinho ang’aka

 

 

Manchester City wameendelea kupata matokeo mazuri katika mechi yao ya tatu ya msimu, ambapo wakicheza ugenini waliwazima Everton 2-0.

 

Vijana wa Manuel Pellegrini wameonekana kutulia na kuwa na dhamira ya kurejesha ubingwa waliopokonywa msimu uliopita na Chelsea.

 

Wanafanya vyema, ikiwa ni tofauti na walivyoanza msimu uliopita, hasa ugenini.

 

Wafungaji walikuwa mlinzi Aleksandar Kolarov na mchezaji aliyetokea benchi, Samir Nasri na hadi sasa ukuta wao haujaruhusu bao lolote.

 

Everton waliingia uwanjani wakijiamini kutoka na ushindi mzuri waliopata dhidi ya Southampton wikiendi iliyopita, lakini waliachia bao la kwanza, sababu kubwa ikiwa ni udhaifu wa kipa, Tim Howard.

 

Mshambuliaji wa Everton aliyecheza vyema mechi iliyopita na kufunga, Romelu Lukaku alijaribu tena kufanya mambo lakini alishindwa, ambapo moja ya jitihada zake ziliishia kwa mpira kugonga mwamba wa goli.

 

Vijana wa Roberto Martinez walijitahidi kupambana lakini ngome ya City, ikiongozwa na nahodha na beki wa kati, Vincent Kompany ilikuwa imara, ambapo mwenyewe aliokoa bao la wazi lililokuwa litiwe kimiani na Gareth Barry kwa kichwa. Aliokoa mpira ukiwa kwenye mstari.

 

Chelsea USHINDI WA KWANZA WA MSIMU

Wachezaji wa Chelsea wakifurahia baada ya kupata bao la kuongoza dhidi ya WBA
Wachezaji wa Chelsea wakifurahia baada ya kupata bao la kuongoza dhidi ya WBA

 

Chelsea wamepata ushindi wa kwanza wa msimu, baada ya kupambana dhidi ya West Bromwich Albion ambao mwishoni mwa msimu ulipita waliwafunga mabingwa hao watetezi 3-0.

 

The Blues walipata ushindi kwa shida, wakienda 3-2 ugenini na kocha Jose Mourinho akafyatuka tena akisema kwamba watu wengi wanapenda wafungwe na kuwa ushindi huo utawasononesha.

 

Ilikuwa mechi ngumu, kwani nahodha na beki wa kati wa Chelsea, John Terry alitolewa kwa kadi nyekundu kutokana na kucheza rafu dhidi ya Salomon Rondon, ikiwa ni mechi ya pili mbaya kwake, kwani katika kichapo kutoka kwa Man City alipumzishwa baada ya dakika 45 kutokana na kiwango duni.

 

Hata hivyo, mchezaji wao mpya aliyesajiliwa kutoka Barcelona kwa pauni milioni 21, Pedro Rodriguez aliwatia shime washabiki wa Chelsea kwa kuongoza mashambulizi kwenye mechi yake ya kwanza, akafunga bao kisha kusaidia jingine.

 

Ilikuwa mechi ambayo mabao yote matatu yalifungwa na wachezaji raia wa Hispania katika Pedro, mshambuliaji tishio Diego Costa na beki Cesar Azpilicueta.

 

Ilikuwa West Brom wanaofundishwa na Tony Pulis wapate bao mapema, lakini kipa namba moja wa Chelsea aliyerejea baada ya kutumikia adhabu ya kadi nyekundu, Thibaut Courtois aliokoa penati ya mapema ya James Morrison.

 

Hadi mapumziko Chelsea walikuwa wakiongoza kwa mabao 3-1, la west Brom likitiwa kimiani na Morrison ambaye pia alifunga la pili baadaye. Rondon alicheza mahali pa Saido Beraniho aliyepumzishwa kutokana na shinikizo la Tottenham Hotspur kutaka kumsajili, lakini ofa yao ya pauni milioni 15 inaelezwa kukataliwa na The Baggies.

 

Kocha Pulis amelalamikia kanuni kuruhusu dirisha kuwa wazi hata baada ya ligi kuanza, jambo linalowafanya wachezaji wanaotakiwa na klabu nyingine kushindwa kutuliza akili na kujituma mchezoni, kama sasa anaposhindwa kumchezesha Beraniho, mzaliwa wa Burundi.

 

Japokuwa Rondon alicheza vyema mahali pake, huenda West Brom wangepata matokeo mazuri zaidi kwa sababu Beraniho ndiye mpiga penati wao, na kutokuwapo kwake jana uwanjani kulishuhudia Morrison akigombea kupiga penati na Chris Brunt. Aliikosa na baadaye akaondoka akiwa amekasirika.

 

 

WATFORD SULUHU NA SOUTHAMPTON

Etienne Capoue, kiungo wa Watford fC, akishindwa kuunganisha mpira wa kichwa...
Etienne Capoue, kiungo wa Watford fC, akishindwa kuunganisha mpira wa kichwa…

 

Watford na Southampton wameishia kutoka suluhu kwenye mechi iliyokosa msisimko, na sasa wote wawili wamemaliza mechi tatu bila kushinda hata moja msimu huu.

Mchezaji wa Watford, Etienne Capoue alikuwa na nafasi nzuri zaidi ya kufunga kwenye mchezo huo wa Jumapili, lakini kwa mshangao wa wengi alipaisha shuti lake akiwa umbali wa yadi mbili tu.

Hata hivyo, kocha wa Saints, Ronald Koeman ameeleza kufurahishwa na sare hiyo, ambapo walikuwa hatarini kupoteza mechi, ambao mshambuliaji wa Watford, Odion Ighalo kutoka Nigeria alikosa bao baada ya majalo hatari ya Ikechi Anya.

Graziano Pelle wa Saints naye alikosa kufunga baada ya mkwaju wake mkali kupaishwa juu ya lango na kipa Heurelho Gomes. Leo Arsenal wanawakaribisha Liverpool dimbani Emirates

advertisement
Advertisement

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

De Gea, Van Gaal hapakaliki

UMEFIKA MWISHO WA TERRY CHELSEA