Menu
in , , , , , , ,

Mambo ya msingi katika Usajili Ulaya

LIGI zimemalizika, na sasa kila timu inajenga kikosi chake. Viongozi wanahaha huku na huko kuhakikisha wanapata wachezaji wanaowahitaji. Wachezaji nao wanatafuta namna bora ya kuhama ili kujiunga na timu mpya kwa sababu mbalimbali. TANZANIASPORTS inaangazia mambo muhimu yanayozingatiwa na viongozi wa soka Ulaya kuelekea msimu ujao, ambapo mavuno ya kila upande yamekuwa kujiandaa kwa mashindano ya kila namna msimu ujao.

Nafasi za mabeki

Timu nyingi zinasajili wachezaji wa nafasi hii kama njia ya kupunguza idadi ya mabao ya kufungwa. Tathmini inaonyesha kuwa mabenchi ya ufundi yanakubali ufanisi wa magolikipa wao, huku wakihitaji kuboresha mabeki waliopo na kusajiloi wapya. Kuanzia Real Madrid, hadi AC Milan, na Chelsea, Arsenal, Man United, Bayern Leverkusen hadi PSG kila timu inahitaji ufanisi wa idara hii. 

PSG ambayo ni bingwa wa Ulaya ilijikuta ikipepesuka kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia la Klabu baada ya kumkosa beki wao mahiri Pacho. Ukweli Pacho ndiye nguzo ya PSG akishirikiana na Maquinhos wameifanya timu hiyo kuwa imara. Lakini kufungwa mabao 3-0 na Chelsea kwenye fainali hiyo kumeifanya timu hiyo kufikiria mara mbili kuhusiana na nafasi ya beki. Bila shaka PSG watahitaji mbadala wa Pacho ambaye atashindana na Beraldo katika nafasi ya namba 4 au 5. Real Madrid wenyewe wamesajili beki wa kushoto, beki wa kulia, na beki wa kati. Hali kadhalika timu zingine zimejikita kuimarisha safu hii ili kupunguza makosa na idadi ya mabao ya kufungwa.

Washambuliaji , mawinga na viungo

Tanzania Sports

Si Liverpool, Arsenal wala Man United wote na timu zingine za Ulaya zimeingia sokoni kusajili wachezaji wa nafasi hii. Baadhi ya timu zimegundua kukosa ufanisi katika eneo la ushambuliaji na viungo. Liverpool wamejikita kwenye kiungo, huku Man United na Arsenal wanaonekana kupambana kusajili washambuliaji ili kuongeza ufanisi wa mabao ya kufunga. 

Msimu uliopita Arsenal waliishia hatua ya nusu fainali baada ya kutupwa nje ya PSG, kwahiyo bajeti yao imenona kidogo baada ya kuongezeka mapato, kwahiyo eneo la ushambiliaji ndilo linalolengwa zaidi. Wachezjai mbalimbali wamehusishwa kujiunga na Arsenal katika safu ya ushambuliaji. Eneo lingine ambalo Arsenal wanahusishwa nalo ni winga, ambapo wapo tayari kuwabomoa majirani zao Chelesea. 

Man United kama walivyo Liverpool wanajikta kwenye eneo la kiungo wa ushambuliaji ili kuimarisha ushindani kikosini na ubunifu wa kupata mabao. Hali kadhalika AC Milan wameingia kwenye dirisha la usajili kuimarisha eneo la kiungo chao. Barcelona wao wamemkosa nyota waliyekuwa wanamfuatilia, Nico Williams ambaye amekubali kubaki katika klabu ya Atlentic Bilbao kwa misimu 8 ijayo. 

Uamkuzi wa kubaki Atletic Bilbao umemaanisha kuwa Lamine Yamal hatakuwa na nafasi ya kucheza pamoja na rafiki yake huyo kwenye klabu ya Barcelona na hivyo watasalia kwenye kucheza timu mbili tofauti ngazi ya klabu, huku ushirikiano wote utaendelea ngazi ya timu ya Taifa.

Kombe la dunia la klabu ni mavuno

Wachezaji mbalimbali wanasajiliwa kutokana na mashindano mapya ya FGainali ya Kombe la Dunia ngazi ya klabu, kuanzia Arias na Danilo raia wa Brazil na Richardo Rios raia wa Uruguay wamekuwa kwenye rada za klabu mbalimbali za Ulaya. Mashindano hayo ya FIFA yameongeza chachu ya kuibua vipaji vya soka ambavyo vimeanza kuwindwa na timu mbalimbali za Ligi ya Ulaya. Kuanzia Ligi ya Ufaransa, Hispania, Ujerumani, Italia, na nyinginezo kama Uholanzi, Uturuki, Ugiriki na Urusi zimekuwa zikitajwa kusajili wachezaji waliong’ara au wenye vipaji vikubwa katika mashindano hao. Estevao tayari alikuwa amesajiliwa na Chelsea, na hivyo anakuwa mchezaji aliyeonesha sababu za klabu ya hiyo ya London kumsajili nyota huyo kutoka Brazil.

Makocha hawajabaki salama

Makocha wa timu mbalimbali wamebadilishwa na wengine wapya wameibuliwa kutoka kusikojulikana na kuongoza timu. Kuanzia timu za Ligi Kuu hadi madaraja ya chini zimeripotiwa kuajiri makocha wapya na wakurugenzi wa michezo ili kuimarisha timu zao kiuongozi. Kwa mantiki hiyo makocha hao wanakabiliwa na kibarua cha kuzijenga timu zao mpya kuelekea msimu ujao na kuleta mafanikio klabuni. Kama ilivyo desturi ikiwa kocha hafanikiwi basi lazima atupiwe virago.

Bajeti za kibano

Timu nyingi zinaonekana kukwepa kusjaili wachezaji wa bei kubwa. Timu hizo zimejikita kusajili baadhi ya wachezaji ambao wamemaliza mikataba yao na kuwa huru. Baadhi ya wachezaji wamesajili kwa bei ndogo sababu muda wao wa kuuzwa kwa bei ya juu ulishamalizika na hivyo kuruhusiwa kuzungumza na timu nyingine. Timu nyingi zinaonekana kupunguza matanuzi sokoni na hivyo zimebaki kwenye msimamo w akubana bajeti zao kwa kusajili wachezaji ambao wapo kwenye mstari wa kile wanachoweza kulipa tu. Endapo mchezaji anauzwa kwa bei ghali, basi ni rahisi kuona tangazo la timu kujiondoa kumfukuzia nyota fulani.

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

Leave a Reply

Exit mobile version