in

MAFANIKIO YA UONGOZI WA BARBARA NDANI YA SIMBA

Barbara Gonzalez

Mnamo septemba 7 mwaka 2020 bodi ya wakurugenzi wa klabu ya simba sports club ikiushitua umma wa wapenda soka na michezo wa afrika mashariki. Siku hiyo bodi hiyo ilatangaza mkurugenzi mpya wa klabu ya Simba sport club kwa mazoea ya wengi walitarajia ayajwe mtu ambaye ni maarufu na ambaye atakuwa ni mzoefu katika soka la Tanzania na afrika kwa ujumla. Kwa mshangao wa wengi siku hiyo mwanamama Barbara Gonzalez alichaguliwa kuwa mkurugenzi mtendaji mpya wa timu ya Simba na hatimaye kumrithi mtu ambaye alikuwa ameshaanza kutengeneza alama yake katika soka la afrika mashariki na afrika kwa ujumla bwana Senzo Mbatta ambaye ni raia wa nchi ya Afrika kusini. 

Barabara amekuwa ni mkurugenzi wa kipekee katika soka la afrika. Mosi amechaguliwa kuwa ni mkurugenzi mtendaji wa klabu kubwa huku akiwa na umri mdogo wa miaka 30. Katika umri mdogo kama huo ni nadra sana kwenye soka kuaminiwa kwenye nafasi kubwa kama hiyo. Wengi ambao hukabidhiwa nafasi hiyo huwa ni watu ambao wanakuwa wana umri wa makamo  yaani miaka 40 na kwenda juu zaidi. Katika mojawapo ya mahojiano yake ya awali aliyowahi kuyafanya baada ya kukabidhiwa mikoba hiyo alisema kwamba lengo lake ni kuifanya samba kuwa ni mojawapo ya klabu kubwa afrika kama ilivyo klabu cha nchini Misri cha Zamalek. Kwa kifupi anampango wa kuifanya klabu hiyo iwe ya kimataifa Zaidi.

Wadau wengi wa soka walimkosoa na wengi waliona kama hawezi kupata mafanikio yoyote yale ndani ya kilabu hicho. Wengi waliona kwamba mwanamama huyo hawezi kuivusha klabu hiyo na kuipeleka katika hatua za mbele kisoka.ilipofika januari 8 mwaka 2021 ratiba ya michezo ya klabu bingwa afrika ilitolewa na timu hiyo aliyopewa mikoba ya kuisimamia ilikabidhiwa katika kundi gumu ambalo limejumuisha wababe wa soka la afrika Ikiwemo Al Ahly ya Misri, AS Vita ya jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na El Mereikh ya Sudan. Watu wengi waliona kwamba samba haiwezi kufanya lolote katika kundi hilo na baada ya mechi za kwanza tu timu hiyo itakuwa imeshatolewa na kasha kuaga mashindano hayo. Katika safari hiyo klabu ya Simba ilishangaza wadau kwa kuifunga As Vita katika uwanja wa nyumbani kwake na katika mechi ya pili walishangaza watu kwa kumfunga timu kongwe na nguli ya Al Ahly ndani ya uwanja wa taifa wa Tanzania ama kwa jina linguine uwanja wa Mkapa.

Katika ligi ya ndani Simba iko vizuri na katika upande wa timu ya wanawake anaimudu vizuri amefanikiwa kutengeneza mazingira ya kibiashara kwa kufanya timu hiyo kupata watazamaji na wafuatiliaji wa timu hiyo. Mnamo februari 8 mwaka 2o21 mwanamama huyo alimteua mwanamama mwenzie Fatema Dewji kuwa ni msimamizi mkuu wa timu ya wanawake wa Simba maarufu kama Simba Queens. Katika mda mfupi wa uongozi wake ameweza kujenga washambuliaji hatari wa kike katika kilabu hicho kama vile mwanadada Oppah Clement. Ndani ya mwezi machi amefanikiwa kuuza mchezaji mmoja kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Morokko. Mwanadada huyo sio mwingine bali ni mchezaji mashuhuri wa Simba Queens yaani namzungumzia Mwanahamisi Omari maarufu kama “Gaucho”

Ndani ya mda mfupi wa uongozi wa Barbara ndani ya msimbazi amefanikiwa kuifanya kilabu hicho kama nembo ya utalii wa nchi ya Tanzania kwani jezi za timu hiyo kwa sasa zimebeba maneno ya “Visit Tanzania” ambayo yanalenga kuhamasisha wageni kuifuatilia klabu hicho popote pale ambapo watakuwa wamesafiri kwenda kucheza mechi nje ya nchi. 

Hakika ni wazi mwanamama huyo ameonyesha umahiri wake wa uongozi katika kipindi kidogo ambacho ameongoza kilabu hicho na sasa mda utaongea Zaidi juuya mafanikio yake katika siku za usoni.

Report

Written by Kahema Fimbo

Mwandishi wa habari wa kujitegemea mwenye uzoefu wa kuandika kuhusu habari za michezo anayeishi Dar es salaam Tanzania. Ana uzoefu wa miaka 2 wa kufanya kuandika na kasha kuchapisha Makala zake katika mitandao kadhaa nchini Tanzania. Ni mpenzi na pia ni mdau wa michezo. Amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi kwenye vyama vya michezo nchini Tanzania ikiwemo katibu mkuu taifa chama cha mchezo wa kabaddi Tanzania (Tanzania kabaddi sport association), mwenyekiti kamati ya habari chama cha shule za michezo Tanzania (Tanzania sport centres and academies association- TASCA) na pia makamu mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya mkuranga( Mkuranga district football association- MDFA).
Nje ya michezo ni mwanajamii na amewahi kujitolea na pia kuwa kiongozi katika taasisi mbalimbali nchini Tanzania za vijana kam vile YOA, TYVA, YUNA, na kadhalika.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Yanga v SIMBA

Lini TFF wataleta utamu wa takwimu VPL?

Tanzania Sports

Simba wanguruma Ligi ya Mabingwa Afrika