in

Mafanikio ya Simba ni kilio cha Taifa Stars..

SSC

Mwezi uliopita timu yetu ya taifa ya Tanzania , Taifa Stars walifanikiwa kushiriki michuano ya CHAN. Michuano ambayo iliwapa nafasi ya wao kushika nafasi ya tatu kwenye kundi lao.

Nafasi ambayo haikuwapa nafasi ya kuendelea mbele na michuano hiyo. Tukumbuke kitu kimoja, michuano hii inahitaji wachezaji ambao wamezoea presha za mechi za kimataifa.

Mchezaji huzoea presha za mechi za kimataifa kupitia klabu. Klabu ndiyo ambayo inaweza kupata nafasi kubwa ya kushiriki michuano ya kimataifa kupitia michuano ya kimataifa ya CAF ngazi ya vilabu.

Hapa nazungumzia michuano kama ligi ya mabingwa barani Afrika na ile michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika. Hii ndiyo sehemu nzuri kwa klabu kuwapa nafasi wachezaji uzoefu wa mechi za kimataifa.

Klabu ya Simba katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu wa mwaka 2018-2019 walifika katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Ukitazama asilimia kubwa ya wachezaji ambao walikuwa wanapata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza walikuwa ni wachezaji wa kigeni.

Mfano kwenye mechi ya As Vita iliyochezwa nchini Congo na Simba kufungwa magoli 5-0 walianzisha wachezaji saba wa kigeni ambao ni Zana Coulibay, Jurko Murshid , Pascal Wawa, James Kotei, Emmanuel Okwi, Meddie Kagere, Clatous Chama.

Wachezaji wa nyumbani ambao walipata nafasi kwenye mechi hiyo ni Aishi Manula, Mohamed Hussein , Mzamiru Yassin na John Bocco. Ni wachezaji wachache sana wa nyumbani kwenye michuano ya kimataifa, michuano ambayo tunataka wachezaji wetu wapate uzoefu.

Wiki hii Simba Sc walifanikiwa kumfunga AS Vita akiwa na wachezaji saba wa kigeni katika kikosi cha kwanza. Wachezaji hao ni Joash Onyango, Pascal Wawa, Tadeo Lwanga, Luis Miquissone, Larry Bwalya, Clatous Chota Chama na Chris Mugalu.

Wachezaji wa ndani waliopata nafasi kwenye kikosi cha kwanza ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamedd Hussein na Mzamiru Yassin. Idadi nyingine ndogo ya wachezaji wa nyumbani katika mechi za kimataifa.

Wakati ambao timu yetu ya taifa inapokuwa na uhitaji wa wachezaji wenye uzoefu katika mechi za kimataifa inakuwa haiwapati kwa sababu asilimia kubwa ya wachezaji wa kigeni ndiyo wanapata nafasi kwenye vilabu vinavyoshiriki michuano ya kimataifa.

Hapa ndipo hoja ya idadi ya wachezaji wa kigeni inapoanzia. Idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni katika timu zetu inatoa nafasi finyu kwa baadhi ya wachezaji wetu wa nyumbani kupata nafasi ya kucheza hasa kwenye mechi za kimataifa.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Marvin Park

Mfahamu mchezaji mwenye uraia wa nchi nyingi

Poulsen

Karibu Kim lakini Taifa Stars imebadilika