LIGI Kuu ya England (EPL) inaendelea, ukiwa umebaki muda mfupi kufikia tamati, huku baadhi ya timu kufanya zisivyotarajiwa.
Hali hiyo imesababisha wamiliki au viongozi wa klabu kuwafukuza makocha na kupachika makocha wa muda, wakiamini kwamba wangeziiondosha vikosi vya timu husika kwenye unyonge nje ya uwanjani na kuwaoa ufanisi uwanjani.
Kama ambavyo madereva wa F1 wanavyoonesha uthamini, hakuna haja ya kukanyaga breki pale unapogeuka juu chini. Ni sawa kabisa na hawa makocha wa muda au wa mpito. Uharibifu umeshafanyika; ajali inatokea.
Timu ikiwa mbali na eneo la kushuka daraja na pia haipo kwenye vita hiyo – kuna kila dalili ya kupona kikombe hicho – meneja wa mpito hufanya nini hasa? Huwapa watendaji fursa ya kutafakari, sawa, lakini unakuta ni mawazo ya hao hao wajumbe wa bodi ya wakuriugenzi yanayosababisha madhila. Na hufikiria juu ya maamuzi yao pia. Pengine kinachotakiwa si muda Zaidi, bali watu wenye kufikiri vizuri Zaidi.
Iwe iwavyo, katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, katika soka ya England pengine imeandika rekodi ya kuweka mwisho wa aina ya ukocha wa mpito katika soka ya kisasa.
Fikiria kuhusu Manchester United msimu uliopita, Chelsea na Tottenham Hotspur msimu huu. Kipi ambacho hakikufanya kazi? Uteuzi wa makocha wa mpito. Kumpa ukocha wa muda mtu ambaye kila mtu anajua hana uwezo wa kupata kazi hiyo.
Ralf Rangnick, Frank Lampard, Ryan Mason. Sio kosa lao. Wanajitahidi kwa kadiri wanavyoweza, wametendwa kiaina hasa. Ni kama kuwa kocha kamili wa Watford. Kila mtu anajua kwamba utakuwa umeondoka baada ya miezi michache. Kila mmoja aweza kubaini kwamba unapita tu. Hakuna mamlaka, hakuna kudumu, hakuna tishio la matokeo.
Katika mechi tatu zilizopita za Spurs kwenye EPL, wamepata kuwa nyuma kwa mabao 5 -0, 2-0 na 3-0 kabla ya kuja kufunga. Hiyo haikubaliki. Jumapili walifunga mabao matatu Anfield, na kugonga mtambaa wa panya mara tatu, nab ado wakapoteza mechi hiyo. Kulikoni? Kwa sababu walikuwa tayari nyuma kwa mabao 3-0 ndani ya dakika 15. Kwa hiyo Lucas Moura alipofanya kosa baadaye mchezoni, bao la Diogo Jota likawa la ushindi. Unaona? Hakuna uendelevu.
Licha ya ujasiri wao wa kupambana kurudi mchezoni, Hapana ubishi kwamba Spurs kama klabu wameanguka tangu kuondoka kwa Antonio Conte. Kwa hakika Mason ni kaimu wa kocha wa mpito baada ya Cristian Stellini. Na hiyo sasa imesaidia nini? Conte alipoondoka, bado kulikuwapo na uwezo wa wao kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Kwa sasa upo uwezekano mkubwa kwamba Spurs hawatakuwa kabisa kwenye mashindano yoyote ya Ulaya
Brighton & Hove Albion wapo alama mbili nyuma yao, wakiwa na michezo mitatu mkononi Zaidi yao. Brighton nao walipoteza kocha msimu huu, lakini wakachagua kocha wa kudumu mara moja.
Hoja inayojengwa ni kwamba Spurs hawangeweza kupata kocha ambaye wangemtaka ikiwa wangeanza harakati hizo Machi. Lakini je, watampata kocha wanayemtaka sasa, bila ya ahadi ya kuwa katika soka ya Uefa? Na je, ingeweza kuwa bora Zaidi kubaki na kile walichokuwa nacho? Hivyo ndivyo, ukizingatia hali tata iliyopo sasa.
Kila mmoja aweza kuelewa kwa bnini Chelsea waliamua kwamba Graham Potter hakuwa mtu sahihi kwa kasi ile na kwa kuwa Mauricio Pochettino alikuwa tayari, ingeeleweka iwapo angechukuliwa kuziba pengo la Potter. Lakini badala yake ikawa ni kutoka kwa Potter Kwenda kwa Frank Lampard, jambo ambalo halijaboresha mambo. Hakuna aliyeona Chelsea ikpindua meza kwa ajili ya kufuzu kwa michuano ya Ulaya msimu huu, lakini sasa wanapiga hesabu tu kuona kwamba hawazidi kushuka kwenye msimamo wa ligi.
Ikiwa Manchester United wangemtaka Eric ten Hag mwaka mmoja uliopita na hawangeweza hadi mwisho wa msimu, basi wangebaki na Ole Gunnar Solskjaer. Muda wote wa Rangnick pale alichofanya ni kuharibu matarajio yake ya kuja kuwa mkurugenzi wa ufundi.
Comments
Loading…