in

LA LIGA; EL Clasico bado ni mechi kubwa duniani?

Visa vya Camp Nou

Wikiendi hii Barcelona walikuwa wenyeji wa Real Madrid katika mchezo wa 7 wa Ligi Kuu Hispania kwenye uwanja wa Camp Nou. Mchezo huo uliomalizika kwa Real Madrid kuichapa Barcelona kwa mabao 3-1 yaliyofungwa na Federico Valverde, Sergio Ramos na Luka Modric. Wakati bao la kufutia machozi la Barcelona lilifungwa na kinda Ansu Fati.

El Clasico mara nyingi imechukuliwa kama mechi kubwa duniani. Ni ‘derby’ ambayo maarufu katika ulimwengu wa kandanda. Nyota kama vile Cristiano Ronaldo na Neymar Junior ni miongoni mwa waliocheza mechi lakini wameondoka katika Ligi Kuu Hispania. 

Hata hivyo Sergio Ramos na Lionel Messi bado wanachezea timu zao za La Liga, hali ambayo inaweza kuwashangaza wengi. Je, El Clasico bado ina mvuto uleule katika soka hapa duniani kwa sasa?

EL CLASICO YA KWANZA 

Upinzani mkali kati ya Real Madrid na Barcelona ni sehemu ya historia ya soka hapa duniani, ambapo ‘drrby’ ya kwanza ilichezwa mwaka 1902, na hadi sasa timu hizo zimekutana katika mechi 244 za El Clasico. 

Timu zote zimepata ushindi wa mechi 96 kila mmoja. Barcelona na Real Madrid ni timu kubwa na maarufu mbili nchini Hispania pamoja na duniani.

NI CLASICO YA MWISHO KWA MESSI?

Hili ni swali muhimu katika uchambuzi huu ikizingatiwa kuwa Lionel Messi ambaye ni kapteni wa Barcelona alitaka kuhama timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu. Hata hivyo viongozi wa Barceliona walipigania kila hali kuhakikisha staa wao huyo haondiki kwao na hivyo kubaki La Liga. 

Tanzania Sports
raha ya ushindi

Kuwepo kwa nahodha huyo kwenye mchezo huo ni miongoni mwa mambo yanayoibua mvuto wa mchezo wenyewe. Kuwaona Real Madrid walihangika kukabiliana na Barcelona, basi sababu ya kwanza ni kuwepo kwa Messi ambaye ni tishio kwao. Kwahiyo Messi ni injini ya Barcelona kwenye mchezo wao wa El Clasico dhidi ya Real Madrid. 

Inawezekana hii ni El Clasico ya mwisho kwa Messi kwenye uwanja wa Camp Nou, kwa vile hali yake ya baadaye haieleweki klabuni hapo kutokana na msuguano uliojitokeza kwenye dirisha la usajili. Messi ndiye mfungaji bora wa El Clasico akiwa amepachika mabao 26, lakini suala la mkataba wake halieleweki na haijulikani nini kitaendelea baada ya kumalizika mwakani 2021.

NYOTA WAPYA, ANSU FATI NA VINICIUS

Wapo nyota kadhaa chipukizi ambao wanatabiriwa kung’arisha mechi za El Clasico zijazo. Chipukizi hao wanatarajiwa kubeba mikoba ya akina Lionel Messi na Sergio Ramos. Suala la umri wa nyota wa sasa ndicho kiashiria cha kuibuka wapyal kwa mfano, Lionel Messi ana miaka 33, Sergio Ramos (34), Luka Modric (35), Gerard Pique (33), Sergio Busquets (32), Karim Benzema (32). Hapo ndipo makinda wanatakiwa kuandaliwa kuchukua nafasi zao kwa vile nyota waliotajwa hapo juu wanaelekea ukingoni.

Katika El Clasico ya wikiendi hii nyota wapya wameanza kukabidhiwa majukumu ya kuwa wapinzani wakali wa jao. Ansu fari (17), Rodrygo Goes (19), Vinicius Junior (20), Sergio Dest (17) wote hao walikuwa uwanjani kwenye mchezo wa wikiendi hii. Makinda hao wanajifunza kutoka kwa wakongwe, ambayo wanaelekea kustaafu kandanda. 

NYOTA WAKUBWA KUHAMA LA LIGA

Katika miaka ya karibuni nyota kadhaa wakubwa wameihama miamba hiyo ya La Liga. Kwa mfano Cristiano Ronaldo, Neymar Junior, Dani Alves, Gareth Bale, Xavi Hernandez, Andres Iniesta, Luis Suarez wote wamezihama Barcelona na Real Madrid miaka ya karibuni.

Kuondoka kwao kunaziumiza timu hizo pamoja na Ligi Kuu Hispania,ambapo viongozi wa shirikisho la soka nchini humo lililazimika kuingilia kati suala la LionelmMessi aliyetaka kuondoka Barcelona msimu huu. Mchezo wa jumamosi hii haukukosa tu viwango lakini El Clasico haitakuwa na thamani wala sifa kama zile za miaka ya nyuma.

BARCELONA,REAL MADRID ZIMEDORORA

imebaki historia
imebaki historia

Soka la Hispania linategemea nguvu ya klabu hizo mbili. Endapo timu hizo zinadorora maana yake La Liga nzima inaathirika. Soka la Hispania ndilo linalotawala barani Ulaya kwa miaka mingi, lakini baadhi ya mataifa yameibuka kuwa na nguvu kwenye soka kipindi hiki kuliko Barcelona na Real Madrid. Viwango vilivyopo katika klabu kama vile Bayern Munich, Liverpool,PSG na Manchester City havionkani kwa Barca wala Madrid kwa sasa.

Timu zote mbili Barca na Real Madrid zimepokea vipigo vya kushangaza katika mechi zao za hivi karibuni kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Chukulia mfano kipigo cha mabao 8-2 walichopata Barcelona kutoka kwa Bayern Munich msimu uliopita. 

Fikiria kipigo walichopata Real Madrid katika mechi mbili za Ligi ya Mabingwa hatua ya mtoano dhidi ya Man City. Fikiria kipigo walichopata Madrid nyumbani na klabu ya Shahktar Donesk kwenye mechi za makundi ya Ligi ya Mabingwa.  Kwahiyo El Clasico haitapata thamani zaidi kwa vipigo kama hivyo.

EL CLASICO BILA MZUKA

Miaka ya nyuma ilikuwa rahisi kuona hekaheka za mechi hiyo. Kuanzia nje ya uwanja ambako ungeweza kuona matamshi yenye utata,taharuki na hamasa zaidi kutoka kwa kocha kama Jose Mourimho, lakini sasa hakuna. Miaka ya nyuma ungeweza kuona mzuka mkubwa ndani ya uwanja ambao unachochea tafrani kwa makocha na wachezaji, lakini sasa umedorora.

Wengi wanafahamu ugomvi wa Pep Guardiola na Jose Mourinho, pamoja na marehemu Tito Vilanova. Wanafahamu vurugu za kusisimua El Clasico zilivyokuwa, sasa hali ni tofauti. Barcelona sasa wanafundishwa na Ronald Koeman, wakati Real Madrid wapo chini ya Zinedine Zidane. 

Ijumaa wiki hii baddhi ya vymbo vya habari vimemwita Zinedine Zidane kama ‘master’. Kwa sababu haonekani kutikiswa tikiswa wala kuzusha maneno yenye taharuki kuelekea El Clasico. Zidane haoneshi kuwa hekaheka nje ya uwanja wala kuibua migogoro kwenyer mikutano yake na vyombo vya habari. 

Hilo linavifanya vyombo hivyo kumwita kocha huyo ‘Master’ kwa sababu kila kitu anakitawala kwa kiwangi cha juu; kuanzia matamshi, majibu ya maswlai magumu,kulainisha taharuki na kuufanya mchezo wa El Clasico usiwe na patashika nje ya uwanja.

Ingawa taharuki ingalipo, lakini sio kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma. Barcelona na Real Madrid zimeondoka kwenye kona ya kuwa maadui na kubaki kuwa wapinzani wa kawaida ndani ya uwanja kwa dakika 90 na maisha mahusiano mengine yanabaki kuwa mazuri zaidi.

Report

Written by Mark Mpangala

*Markus Mpangala ni Mhariri, Mwandishi wa Makala Maalumu, Mwanahabari,Mwanablogu,Mwanafasihi na Mwanasafu, ambapo kwa kipindi cha miaka 12 amefanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali vikubwa na vidogo nchini Tanzania katika Michezo, Siasa, Elimu na utalii. Pia ni mchambuzi mchangiaji wa masuala ya siasa na utawala bora katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC SWAHILI). Ni mhariri na mhamasishaji wa usomaji wa vitabu*

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Azam Bingwa Chini Ya Yanga Na Simba

yanga vs simba

Yanga Inafaidika Na Wachezaji Wa Simba