in , , ,

Kwanini Liverpool atashinda dhidi ya Napoli ?

Kwanini Liverpool atashinda dhidi ya Napoli ?

Ndiyo makamu bingwa wa ligi ya mabingwa barani ulaya. Msimu jana walikuwa bora sana mpaka wakafika hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani dhidi ya Real Madrid.

Msimu huu wana nafasi ya kutolewa tena kwenye michuano hii kama wasiposhinda dhidi ya Napoli kwa jumla ya magoli 2-0.

Kwanini ninaamini Liverpool atashinda mechi ya Leo ?

1: Anfield siku zote limekuwa koti la chuma kwa Liverpool ni ngumu kuwaamuzia wachezaji kwa kuwaponda mawe kwa sababu huvaa koti la chuma linaloitwa Anfied.

Ni sehemu ambayo yule mchezaji wa ziada huonekana, na tafasri halisi ya mchezaji wa kumi na mbili ni shabiki huonekana katika uwanja wa Anfield.

Hii ndiyo silaha ya kwanza ambayo ninaiamini kuwa Liverpool wataitumia kuwaangamiza Napoli, mashabiki wa Liverpool wameumbiwa usiku wa ulaya.

Kwao wao kutoonekana katika usiku wa ulaya ni dhambi kubwa sana na watafanya kila waliwezalo kuwapa moyo wachezaji ili waweze kuendelea kwenye usiku wa ulaya ili wasitende dhambi ya kutokuwepo.

2: Msimu Jana Salah , Firmino na Mane kwa pamoja walifunga magoli zaidi ya 90. Ulikuwa umoja bora wa safu ya ushambuliaji katika ligi nyingi barani ulaya.

Msimu huu bado wapo, Salah kwenye ligi kuu ya England kafunga goli 10 akiwa ndiye mfungaji anayeongoza, Mane kafunga magoli 6 na Firmino kafunga magoli 4.

Hii ni safu ya ushambuliaji ambayo ina nafasi kubwa ya kuifanya Liverpool iendelee kubaki katika ligi ya mabingwa barani ulaya kwa kushinda mechi dhidi ya Napoli.

Mohamed Salah..alitupia nne, kwenye mchezo wa EPL

3: Inawezekana msimu jana Liverpool ilikuwa inakosa watu sahihi waliokuwa wanatoka kwenye benchi.

Hadithi hii haipo msimu huu, kuna hadithi tofauti ambayo imeanzishwa msimu huu. Kwanini nasema hivo ?

Msimu huu Liverpool wamekuwa na benchi kubwa hasa hasa kwenye safu ya ushambuliaji. Wana Shaqir, Origi na Dani ambao huwa wanaingia kutoka kwenye benchi na kubadilisha mchezo.

4: Naby Keita anabaki kuwa usajili muhimu wa Liverpool nyuma ya Allison ambaye ni usajili bora wa Liverpool msimu huu.

Naby Keita amekuja kuongeza ubunifu mkubwa katika eneo la katikati, ubunifu ambao umekuwa ukiwasaidia safu ya ushambuliaji ya Liverpool kupata huduma nzuri.

Uwepo wa Naby Keita utaisaidia Liverpool Leo kuwa na asilimia kubwa ya ubunifu katika eneo la mbele la Liverpool.

5: Liverpool imekuwa jiwe, ni ngumu kuipasua kwa ngumi tena kama ilivyokuwa mwanzoni. Safu yake ya ulinzi imekuwa bora tofauti na msimu Jana.

Van Djik amekuwa kiongozi bora kwa vijana kama Robertson’s, Gomez na Alexander Anorld. Amewafanya wawe watulivu katika eneo la nyuma.

Usajili wa Allison ni usajili bora kwa Liverpool msimu huu, amefanikiwa kufuta makosa mengi binafsi yaliyokuwa yanafanywa na makipa wa Liverpool msimu Jana.

Hakuna makosa binafsi mengi tena katika safu ya ulinzi ya Liverpool kama msimu jana, na hii ndiyo silaha ambayo inaweza kumfanya Liverpool awe na nafasi kubwa ya kushinda mechi dhidi ya Napoli bila kuruhusu goli, kwenye ligi kuu ya England mpaka sasa hivi Liverpool wana Clean sheets 10.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Man City: Fumbo la kwanza la macho na hatima ya EPL

Tanzania Sports

Mikono ya Allison inazidi kumuumbua Klopp