in , ,

Man City: Fumbo la kwanza la macho na hatima ya EPL

Man City: Fumbo la kwanza la macho na hatima ya EPL

Mambo yameanza; hatimaye Manchester City wamefumba macho kwa mara ya kwanza msimu huu kwenye Ligi Kuu ya England (EPL).

Jamaa hawa wa Uwanja wa Etihad walio chini ya Pep Guardiola wamepoteza mechi kwa kufungwa na chelsea, ambao nao walianguka awali kwa kupigwa na Wolverhampton.

Haikuwa ikitarajiwa kabisa kwamba wangefumba kutokana na kasi na mserereko ambao wamekuwa nao tangu kuanza kwa EPL, iwe nyumbani au ugenini na walikuwa wakiongoza ligi muda mwingi.

Kwa kuanguka huko, Liverpool wamechukua usukani wa uongozi wa ligi, wakiwatangulia wenzao kwa alama moja; nafasi ya tatu ikishikwa na Tottenham Hotspur huku Chelsea na Arsenal wakifungana kwa alama kwenye nafasi zinazofuata, tofauti ikiwa ni mabao ambapo Chelsea wana tofauti nzuri zaidi ya mabao. Manchester United wameachwa mbali kwa alama nane na wawili hao baada ya kufanya vibaya mara nyingi.

Man City ndio mabingwa watetezi ambapo msimu huu inaonekana kwamba ushindani mkubwa upo kutoka kwa Liverpool wa Jurgen Klopp, lakini pia huwezi kuwadharau Spurs, Chelsea na Arsenal.

Bado Man City wanaonekana watapambana kuhakikisha wanarudi kileleni kutetea ubingwa wao kutokana na uzito wa kiwango chao. Hapana shaka Man City wanasubiri kwa hamu lini Liverpool watafungwa, maana hadi sasa ndiyo timu pekee ambao bado hawajapoteza mchezo kwenye ligi kuu hiyo.

Katika vikao vingi visivyo rasmi vya washabiki wa soka, imekuwa ikichukuliwa kwamba Guardiola kutetea taji kwa mara ya pili ni jambo ambalo ni la kawaida na litatokea, kutokana na jinsi walivyo na walivyokwenda vyema kwenye mechi 15 za kwanza msimu huu.

Ni muhimu kujua kwamba hayo hayajapata kuwa maoni ya mwalimu wala wachezaji wake ambao msimu uliopita walimaliza ligi wakiwaacha wenzao kwa mbali, na lilikuwa taji la kwanza la Guardiola nchini England tangu aingie akitoka Bundesliga alikofanya vyema akiwa na Bayern Munich.

Bila kujali jinsi kushindwa kunavyouma, ni wazi kwamba City hawatahangaika sana na kupoteza huko mechi, badala yake watajipanga upya ili waanze tena mserereko wa ushindi; kusema hivyo na kujiandaa namna hiyo ni jambo moja lakini utekelezaji ni jambo jingine na ushindi ni uwanjani si upana wa kikosi au wingi wa fedha walio nao wenye timu na mishahara mikubwa ya wachezaji au dau kubwa la usajili.

Nina imani kwamba watu wa City, hasa wachezaji na mwalimu, walisahau mambo ya kichapo hicho mapema kabla au wakati waliporejea kwenye uwanja wao wa mazoezi. Dakika 44 za mwanzo walifanya kazi nzuri uwanjani, isipokuwa umaliziaji tu ndio ulionekana kuwa wa tabu.

Guardiola anaamini kwamba timu yake inafanya vyema kama ilivyokuwa msimu uliopita, lakini tofauti tu ni kwamba wapinzani wao wanapanda kwa kasi, kama Arsenal ambao wamebadilishwa kabisa na kocha mpya, Mhispania Unai Emery na wamerejesha ile kujiamini wachezaji lakini pia washabiki wao sasa kuwa wasio na mioyo myepesi au kuwaza kushindwa.

Tayari Guardiola ameshasema kwamba hawapo pale kwa ajili ya kuwa ‘invincible’ yaani kama Arsenal ambavyo hawakufungwa kabisa msimu mmoja wapo, bali kwamba wapo kwa ajili ya kuwa mabingwa na kwamba mabingwa hufungwa na anayezungumza vinginevyo anazungumzia mambo yasiyokuwapo.

Ni wazi ushindani utakuwa mkubwa kadiri muda unavyokwenda na sasa timu tano za juu zinapishana kwa alama nane tu. Ndio hizo zinapewa nafasi kubwa, lakini watu watapenda sana kujua wakati wa msimu wa sikukuu pengo kati ya timu moja na nyingine litakuwaje na iwapo Januari timu nyingine zitaanza kuwa katika taabu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Miguu ya Modric itamfumbua Neymar

Tanzania Sports

Kwanini Liverpool atashinda dhidi ya Napoli ?