in , , ,

Kipindi kigumu bado kinakuja


Je, mbio za ubingwa zimekwisha? Hapana bado. Nafasi ya makosa kwa wale wanaowafuatia Arsenal imepungua sana, lakini Arsenal wana mechi ngumu kadhaa kabla ya Krismasi. Wakitoka salama katika kipindi hicho, wataonekana wasioweza kuzuilika. Lakini wakiteleza mara moja au mbili, wengine wataanza kupata matumaini. Hata hivyo, Arsenal wanaonekana imara sana. Ulinzi wao unalinganishwa na ule wa Chelsea msimu wa 2004-05 — unaotoa utulivu mkubwa. Arsenal wamekabiliwa na shuti moja tu lililolenga goli katika mechi zao tatu zilizopita: jambo la ajabu kabisa. Hata hivyo, wako nafasi ya 17 kwa mabao ya kutolewa katika mchezo wa wazi. Ushindi wa tabu wa bao moja kwa bila siyo wa afya sana, unaweza kwa urahisi kubadilika kuwa sare za kukatisha tamaa. (Fulham na Crystal Palace)

Wengine hawana uimara huo. Chelsea wanapanda na kushuka. Tottenham hawana kiwango kizuri nyumbani na wanakosa ubora wa wachezaji binafsi. Liverpool kwa sasa wako kwenye vita ya nafasi ya nne bora. City wana Haaland lakini wako kwenye kipindi cha mpito. Si udhalilishaji kusema kwamba Bournemouth wana nafasi nzuri ya kufuzu Ligi ya Mabingwa. Hii inatuacha katika hali ya ajabu ya kujiuliza kama Manchester United ni tishio kimya kimya. Takwimu zao za msingi ni nzuri na wanaweza kunufaika kutokana na kutoshiriki michuano ya Ulaya. Lakini United? Kweli tunaweka matumaini kwa United? Kwa sasa, ubingwa uko mikononi mwa Arsenal. Wanaweza kuwa na hofu tu kama kutakuwa na shinikizo kwenye uongozi wao. Hata hivyo, tuone watakuwa wapi baada ya safari yao kwenda Villa Park tarehe 6 Desemba.

Msimu bado unaanza tu


Saa ndio zimebadilishwa hivi karibuni,(Hapa UK) bado tuko Oktoba na safari bado ni ndefu sana. Arsenal wameanza vizuri lakini hawajaonekana kama timu isiyoweza kushindwa. Tottenham, City na Liverpool wako pointi tano, sita na saba tu nyuma. Katika hatua hii ya msimu, pengo kama hilo linaweza kuzibwa kwa urahisi. Na tusisahau Bournemouth. Wako pointi nne tu nyuma ya vinara, hawana usumbufu wa michuano ya Ulaya na wana kocha bora — hakika wamepata haki ya kuota ndoto.

Arteta atajua vyema kuliko kuwaza ndoto za ubingwa mapema, hasa akielekea katika ratiba ngumu ya Novemba yenye safari za ligi dhidi ya Burnley, Sunderland – ambao wana tofauti ya pointi tano tu – na Chelsea, pamoja na mchezo wa nyumbani wa derby dhidi ya Tottenham. Katikati ya hayo, kuna mechi za Ligi ya Mabingwa dhidi ya Slavia Prague na Bayern Munich, jambo linalofanya safari hiyo kuwa hatarishi. Zaidi ya hayo, kila timu hupitia vipindi vya kupanda na kushuka katika msimu wa mechi 38. Timu zingine hufanya mazoezi ya maandalizi kwa lengo la kumaliza msimu vizuri, hata kama inamaanisha kuanza kwa kusuasua. Wakati fulani, Alexander Isak ataanza kufunga tena; mapambano ya Liverpool kutetea taji bado hayajaisha. Na tusisahau City pia.

Washindani wanakosa uthabiti


Hakuna mbio za ubingwa zinazokuwa zimekwisha kabla ya robo ya kwanza ya msimu, lakini Arsenal wako katika nafasi nzuri sana. Kumaliza wakiwa wa pili mara tatu mfululizo kumeunda hisia za “sasa au kamwe”, na kwa sasa wanaonekana kujibu kwa ufanisi na ukatili. Ulinzi wao imara unamaanisha kwamba hata wasipocheza vizuri, wanahitaji bao moja tu kushinda, na uwezo wao wa ajabu katika mipira ya adhabu unawapa nafasi kubwa zaidi ya kufanya hivyo. Jambo muhimu, wanaweza kushinda kwa mitindo miwili tofauti. Kikosi chao kinaonekana kilicho kamili zaidi katika ligi, wakiwa na wachezaji kadhaa kwa kila nafasi; wamepata pengo la pointi nne licha ya kuwakosa Ødegaard, Havertz na Noni Madueke.

Lakini si kwamba Arsenal wanaonekana wazuri tu; ni kwamba ni vigumu kuona nani anaweza kuweka mwenendo thabiti wa matokeo ili kuwazidi. Liverpool, kama Slot anavyokiri, wameeleweka kimchezo; City nao wanajaribu kuingiza wachezaji wapya kadhaa na wanaonekana kuwategemea sana Haaland; Chelsea hawana makali bila Cole Palmer na wana upungufu nyuma. Chini ya shinikizo, timu yoyote inaweza kuyumba; lakini hakuna anayeonekana kuwa na uwezo wa kuweka shinikizo hilo.

Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Arsenal waongoza EPL kwa alama nne..

Ruben Amorim

Mwaka mmoja wa Amorim katika Manchester United