in , , ,

Ange Postecoglou amefuata nyayo

KAMA kuna kocha ambaye anasonya wakati huu basi ni yule aliyekuwa Tottenham Hostspur, Ange Postecoglou. Ni dhahiri shahiri kuwa kocha wa Spurs ametupiwa virago na klabu hiyo imeanza mchakato wa kusaka kocha mpya. Kufukuzwa kwa kocha huyo kumeongeza ufa kati ya wachezaji na viongozi wa timu hasa mwenyekiti wao Daniel Levy. TANZANIASPORTS inachambua masuala muhimu ambayo yamechangia kufukuzwa kwa kocha huyo pamoja na hasira za wachezaji  dhidi ya uongozi. Vilevile uchambuzi huu umejikita kuangalia imani ya kocha huyo katika kupata mafanikio ya ukocha kwenye Ligi Kuu England.

Msimu wa pili na ubingwa

Kocha Ange Postecoglou ameondoka katika klabu ya Tottenham Hotspurs akiwa na falsafa yake anayoiamini zaidi na ambayo haikueleweka mbele ya viongozi. Tishio la Spurs kuteremka araja lilikuwa kubwa kiasi kwamba tishio la kufukuzwa lilionekana mapema zaidi. Sifa alizokuwa anapewa kwa kuifanya Spurs icheze vizuri, ushindi wake mnono dhidi ya waliokuwa mabingwa watetezi Man City kwa mabao matano ni miongoni mwa mambo yaliyokuwa yanampa sifa kocha huyo. Hata hivyo hali ya Spurs ilibadilika ghafla na mwenendo wake kushuka daraja ulionekana dhahiri. Hata hivyo imani kubwa aliyokuwa nayo ni kutwaa taji katika msimu wake wa pili. Msimu wa kwanza hakumaliza na taji lolote, lakini msimu wa pili aliwapa imani viongozi na wachezaji wake kuwa lazima ashinde. Ange alitumia mfano wa ubingwa aliowahi kuchukua huko Scotland.

Wakati msimu pili ukiwa unaelekea mwishoni ilikuwa dhahiri kuwa kocha Ange Postecoglou hakuwa na nafasi ya kutwaa taji hilo. Tottenham Hotspurs walizidiwa kwa pointi 36 na Liverpool hivyo wakapoteza matumiani ya kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu. Hata hivyo Spurs wamemaliza msimu wakiwa na taji la Europa League ambapo aliwafunga Man United. Licha ya kutwaa ubingwa huo amefukuzwa. Hapa imani yake imefanya kazi lakini katika mazingira magumu.

Kufuata nyayo

Mabosi wa Tottenham Hotspurs wana kasumba ya kuwafukuza makocha licha ya kufanikiwa kutwaa mataji au kuwafikisha katika hatua nzuri. Mauricio Pochettino alifukuzwa Spurs miezi kadhaa baad aya kuwaongoza kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Licha ya kuifikisha timu hiyo kwenye hatua hiyo bado ilionekana si kitu muhimu cha kumbakiza mwalimu huyo, badala yake akatupiwa virago.

Jose Mourinho, alikuwa kocha hodari na bingwa wa mabingwa. Mourinho ametwaa mataji ya Ligi ya Mabingwa, Ligi Kuu England, Europa League na mengineyo lakini alifukuzwa siku 6 kabla ya kuwaongoza Spurs kwenye fainali ya Kombe la Ligi England mwaka 2021.

Na sasa, Ange amekuwa kocha wa tatu kufukuzwa katika mazingira yanayofanana na watangulizi wake. watangulizi wake wamefanikiwa kuweka rekodi kwa timu lakini hawakudumu. Hali kadhalika Ange Postecolgou hajadumu licha ya kuipa taji la kwanza la Europa League klabu hiyo.

Daniel Levy alifanya uamuzi mapema?

Hakuna ubishi kwamba Daniel Levy ndiye mtu anayedhibiti kila kitu katika klabu ya Tottenham Hotspurs. Ndiye alfa na omega. Ndiye mmiliki na mwajiri wa makocha wanaoingia klabu hapo. Lakini mwenendo wa Spurs bila kujali ubingwa waliomletea ni dhahiri alifanya uamuzi mapema sana ili kuepuka makosa kama yaliyotokea nyuma. Wakati anamfukuza Jose Mourinho zilikuwa zimebaki siku 6 kucheza mchezo wao wa fainali ya Kombe la Ligi. 

Ulikuwa umauzi mbovu lakini mwenye mali aliusimamia na Mourinho akaoneshwa mlango wa kutokea. Pochettino licha ya kuifikisha fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza naye alioneshwa mlango wa kutokea.

Kufukuzwa kwa Ange Postecoglou huenda lilikuwa suala la muda tu kutokana na matokeo mabovu ya klabu hiyo. Levy anajulikana kama mmiliki wa timu menye mkono wa chuma. Linapofika suala la makocha kushindwa kufanya vizuri huwa anawafukuza haraka sana. Levy amewahi kuwafukuza makocha wakubwa kama vile Mauricio Pochettino na Jose Mourinho. Hivyo suala la kumfukuza Ange Postecoglou huenda likaw ajambo jepesi lakini sehemu pekee ambayo itaokoa kibarua chake ni kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Frankfurt.

Nini hasa kinachomkabili?

Ange Postecoglou ni kocha ambaye aliingia England akiwa na sifa za kutwaa mataji huko Scotland. Katika Ligi ya Uskochi kocha huyo alikuwa miongoni mwa miamba ya soka. Sifa zake za kiufundi ndizo zilizomfanya apate ajira ya kuifundisha Spurs, lakini tangu alipowasili huu ni msimu wa pili ambao unaelekea ukingoni huku akiwa hana uhakika wa kunyakua taji lolote. Kikosi chake kimekuwa kikicheza mpira wa kuvutia, lakini anaonekana kukosa kikosi cha kwanza thabiti ambacho kinaweza kupigania hadhi ya timu hiyo. 

Spurs wamefungwa katika mechi 16 na kushinda michezo 11 na kutoka sare 4 katika michezo 31 waliyocheza hadi sasa. Hii inadhihirisha mwenendo wa Spurs msimu huu si mzuri. Katika mechi 31 kisha kufungwa 16 ni jambo la hatari ambalo mwalimu anatakiwa kuhojiwa nini kinachotokea katikati ya uwekezaji huo. 

Uvumilivu walionao viongozi wa Spurs huenda ukafika mwisho kwa mwalimu huyo kwani haionekani kama anaweza kuendelea na kibarua hicho msimu ujao. Spurs imekuwa timu ambayo vijana wa mjini wanaweza ina homa ya vipindi, wanaweza kucheza vizuri mechi moja kisha wanakwenda kuvurunda nyingine. Mfano unapambana na timu kama Man City na kuionesha kuwa wewe ni mwamba lakini unakuja kufungwa na timu kama West Ham au  Everton lazima kuwe na hali ya sintofahamu.

Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Ni ipi taswira ya Kombe la Dunia la klabu?

Tanzania Sports

Kilio cha Ronaldo katika miguu ya Yamal, Williams