in , , ,

KIONGOZI: SIO LAZIMA ULIWAHI KUCHEZA MCHEZO HUO

Arsène Wenger, akimkumbatia meneja wa Manchester City, Pep Guardiola, kabla ya mchezo kati ya timu zao

Katika dhana ambazo ni sumu katika uhai wa michezo nchini Tanzania ni dhana ya kwamba mtu hawezi kupewa uongozi wa klabu ama chama cha mchezo  kama hajawahi kuwa mchezaji ima wa ridhaa ama wa kulipwa wa mchezo huo. Katiba nyingi za vyama vya michezo ambayo imesajiliwa nchini Tanzania ukiziangalia utazikuta zina kanuni kwamba kiongozi wa mchezo huo husika lazima awe amecheza mchezo huo. Na baadhi zimeenda mbali na kusema kwamba awe ni yule ambaye amewahi kuitumikia timu ya taifa katika mchezo huo.

Hali hii imekuwa inarudisha nyuma maendeleo ya michezo kwa namna Fulani. Mtendaji wa michezo iwe ni kocha ama mtu ambaye anashughulika na majukumu ya masuala ya utawala wa michezo(Sports Management) sio lazima awe aliwahi kuwa mchezaji ndio aweze kuwa na mafanikio katika majukumu yake ya usimamizi wa michezo. Historia inaonyesha wadau mbalimbali tu wamewahi kuwa na mafanikio katika usimamizi wa michezo licha ya kwamba hawajahi kuwa ni wachezaji mahiri katika mchezo huo. Ngoja nitoe baadhi ya mifano ya hao wadau ifuatavyo:-

Arrigo Sachi wa Italia. Huyu ni mojawapo ya makocha wakubwa kuwahi kutokea katika nchi ya Italy. Kocha huyu hajawahi kabisa kuchez soka katika ngazi yoyote ile. Alifundisha klabu ya Fusignano kutoka mwaka 197 mpaka mwaka 197 na ikawa ina mafanikio.

Avram Grant kutoka taifa la Israel.kocha huyu amekuwa kwenye michezo hususani kwenye soka kwa mda wa miaka 47 licha ya kwamba kwa sasa ana umri wa miaka 67. Kocha huyu amewahi kufundisha vilabu mbalimbali duniani ikiwemo kufundisha klabu ya Chelsea na huyu kocha hajawahi kabisa kucheza soka.

Brian Kerr ambaye aliwahi kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka ya Ireland. Kocha huyu licha ya kwamba hakuwahi kucheza soka la kulipwa ila aliwahi kuiwezesha timu yake kushinda kombe la ubingwa wa ulaya kwa wachezaji walio chini ya umri wa miaka 18 na mara nyingine kwa walio chini ya umri wa miaka 16.

Andre Villas Boas wa Ureno. Kocha huyu alipata leseni ya ukocha ya daraja la C ya UEFA wakati akiwa na umri wa miaka 17 na daraja B akiwa na umri wa miaka 18 na akapata leseni daraja A na daraja la Pro wakati akiwa na miaka 19. Mwaka 2010 alifanikiwa kubeba kombe la Europa na la ligi ya Ureno na kasha kuweka rekodi ya kuwa kocha mdogo Zaidi kuwahi kubeba makombe hayo katika historia.

Leornardo Jardim kocha ambaye aliyewahi kuwa kocha mkuu wa klabu ya Monaco ya Ufaransa katika mwaka 2014 mpaka 2018. Aliongoza klabu hiyo kuwa na mafanikio na kocha huyu hajawahi kabisa kucheza soka lolote la kulipwa katika ngazi yoyote ile.

Carlos Alberto Pereira kutoka Brazil. Kocha huyu hakuwahi kucheza soka la kulipwa. Alianza shughuli za ukocha mnamo mwaka 1968 akiwa na kijana mdogo wa umri wa miaka 23 kwa kufundisha soka katika timu ya taifa ya Ghana. Na hiyo ilikuwa ni baada ya kuhitimu masomo yake ya chuo kikuu ambapo alikuwa amebobea katika elimu ya viungo(physical education). Kufundisha kwake timu ya Ghana kulimsaidia kumjengea uwezo wa kujiamini na pia uzoefu kwani baada ya hapo alipata fursa kadhaa za kufundisha timu kadhaa. Anakumbukwa Zaidi kwa kusaidia taifa lake la Brazil kubeba kombe la dunia ambalo lililofanyika nchini Marekani la mwaka 1994. Alisaidia taifa lake kubeba kombe hilo ambapo mara ya mwisho kulibeba ilikuwa ni mnamo mwaka 1970 na hivyo akarejesha furaha kwa watu wa nchi yake na pia alirudisha morali ya kujiamini ambapo watu wa taifa hilo walikuwa wameanza kuipoteza kutokana na kutolibeba kombe hilo kwa mda mrefu.

Rolani Mokwena kutoka Afrika kusini. Kocha huyu kwa sasa ndiye kocha mkuu wa wababe wa soka la Afrika Kusini yaani klabu ya Mamelodi Sundowns. Kocha huyu amefanikiwa kubeba mataji kadhaa katika maisha yake ya soka. Na amewawahi kufundisha vilabu kadhaa nchini humo Afrika Kusini. Kwa sasa nchini Tanzania kocha Mokwena ni maarufu kutokana na kwamba klabu ya Yanga ilicheza na kikosi cha Mamelodi Sundowns katika hatua ya robo fainali ya klabu bingwa ya vilabu vya soka barani Afrika.

Maurizio Sari wa italia. Kocha huyu mtaliano ni mojawapoya makocha ambao huwa wanasifika kufundisha soka lenye kuvutia ambalo mashabiki huvutika nalo. Kocha huyu amewahi kufundisha vilabu kadhaa vikubwa kama vile Lazio, Napoli, Juventus na Chelsea. Katika kufundisha kwake soka hajapata mataji mengi sana makubwa ila ameweza kujijengea jina na heshima. Kocha huyu hakuwa kucheza soka la kulipwa. Kocha huyu anasifika pia kwa kuvigunduana kuviendeleza vipaji vya baadhi ya wachezaji ikiwemo Jorginho.

Sepp Blatter wa uswisi. Gwiji huyu wa soka duniani kwa sasa amefungiwa kujihusisha na masuala ya soka. Gwiji huyu umaarufu wake ulikuja pale aliposhinda kuwa raisi wa shirikisho la soka duniani FIFA. Katika uongozi wake wa soka licha ya kwamba alimaliza vibaya ila atakumbukwa kwa baadhi ya mambo ambayo aliyoyaafanya katika maendeleo ya soka. Gwiji huyu hakuwahi kucheza soka la kulipwa.

Arsene Wenger wa Ufaransa. Gwiji huyu wa soka duniani kwa sasa yeye ni mkurugenzi wa maendeleo ya soka duniani katika shirikisho la soka duniani FIFA. Gwiji huyo alivuma sana wakati anafundisha soka katika klabu ya Arsenal ya jijini London. Amefanya mambo mengi makubwa katika klabu hiyo na alisaidia kuifanya klabu hiyo iwe ni mojawapo ya vilabu vya michezo vyenye nembo(brand) kubwa za kibiashara.

Mifano iko mingi Zaidi lakini mda hautoshi tuishie na hayo. Niseme tu kwamba vyama vya michezo nchini Tanzania vijipange Zaidi kwa kupata viongozi wenye uweledi wa mambo mbalimbali ambao utavisaidia vyama hivyo kujiendesha kisasa na pia kuvifanya vipate mafanikio katika mashindano ya kimataifa viangalie sifa ya kiutendaji bora Zaidi na sio kulazimisha kuwa na viongozi ambao waliwahi kucheza mchezo huo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

42 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

WANAMICHEZO NA KUJIENDELEZA KIELIMU

Tanzania Sports

TUZO YA UFUNGAJI BORA YA MOHAMMED HUSSEIN MMACHINGA