in

Kigwangala, Mo Dewji Hapatoshi Twitter

MO

Kinachoendelea katika ukurasa wa Twitter wa Waziri wa Utalii na Maliasili,  Hamisi Kigwangala juu ya uwekezaji wa Mohammed Dewji   ‘Mo’  na zile milioni 20 zinaendelea kuchukua sura mpya.

Kigwangala ameandika mengi akihoji mambo mbalimbali ya uhalali wa ‘Mo’ kuendelea kuongoza Simba wakati huo bado hajaweka fedha za hisa katika ‘bank’.

Anauliza bodi ya Simba juu ya 49% ya hisa nani ataweza kumpa jibu sahihi juu ya fedha hizo kuwekwa sehemu sahihi.

Picha ya sinema hii ilianza pale Dewji alipomteua Mtendaji mpya Barbara Gonzalez  mara baada ya kuondoka Senzo Mbatha.

Alihoji juu ya uwezo wa Barbara Gonzalez ambaye alikuwa anafanya kazi katika kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (METL).

Amehoji mchakato wa kumpata Mtendaji Mkuu (C.E.O)  ulikuaje, ‘Mo’ alitumia njia ipi ili kupata mtu mwenye weledi na uzoefu wa kufanya Simba SC isonge mbele.

Tena ameomba kabisa kama kuna mtu anaweza kuweka wasifu wa Senzo ili aangalie uzoefu wake na huyu aliyeteuliwa sasa.

Tanzania Sports
Sehemu ya majibishano kwenye twitter

Hapa hoja yake  ina mashiko kwa mtu anayetaka maendeleo ya mpira lakini kama unachukulia ushabiki bila kupambanua mambo basi utaegemea upande mmoja.

Dewji naye akaibuka na kutaka kuzima yote hayo na kusema kuwa Kigwangala kama alitaka kujua bilioni 20 ziko wapi atafute mahojiano au angepiga simu moja kwa moja.

Huku akiweka wazi kuwa ameyasema yote hayo kwakuwa alimnyima mkopo wa pikipiki ndio sababu ya kufunguka kwa ambayo ameyaongea Kigwangalla.

Shuti hilo Kigwangalla amelipangua kwa kukubali kuwa alihitaji kukopa na ‘Mo’ alikataa ila sio sababu ya kusema aliyoyasema, amefanya hivyo kwakuwa yeye shabiki wa Simba anayetaka maendeleo.

Hapa wataalamu wa instagram wanasema hadi kufikia dakika ya 60 ngoma ipo sare ‘Patulo’, ila hii haibadilishi ukweli wa kutaka kujua mambo hata kama anayehojiwa ni ‘Tycoon’.

Katika mahojiano aliyoyafanya na kituo kimoja cha Radio ‘Mo’ alisema kuwa anatumia bilioni tatu kila mwaka kuhudumia Simba SC, huku akijinadi kuwa hawezi kushindwa kuweka hizo bilioni  20 ‘Bank’.

Tanzania Sports
malumbano

Hawa wote wapo katika nyumba moja ya kujenga soka la Tanzania kukua kimataifa,  lengo la Kigwangalla sio kulipiza kisasi kwakuwa alimnyima mkopo lakini alitaka kufahamu juu ya maswali yake ambayo aliyetakiwa kujibu angeyajibu kawaida tu wala kusingekuwa na misuguano.

Nimejaribu kupitia maoni mbalimbali katika hizo posti pomoja na makundi ya WhatsApp,  kila mmoja anaongea lake, wale shabiki wa Simba ambao hawataki Dewji aguswe wanatupa vijembe  kwa mtoa mada ambaye ni Kigwangalla, wachache sana wanamuunga mkono.

Wengi kati ya wanao muunga mkono kutoka upande wa pili wakiona hiyo in fursa kupigilia msumari. Imefika hatua hadi wanamkumbuka yule mzee wa Simba (Kilomoni) aliyezishikilia hati za timu.

Mabadiliko yanatakiwa sana lakini sio haya ya kwenda hatua mbili huku unarudi nyuma hatua kumi haina maana.

Jopo la Simba na wanachama wanatakiwa wajitathimimi na waweke mambo sawa ili ule mkubwa unaohubiriwa uonekane dhahiri.

Vinginevyo tutatwanga maji katika kinu na wasiruhusu Simba igawanyike makundi kama ilivyokuwa zamani, kundi la Ukawa na lile la Simba yenyewe kwakweli kutatoa mwanya mkubwa sana kwa timu nyingine 17 kunyakua kombe la ligi kwa urahisi sana.

Simba inatakiwa wajue kwamba shabiki ndio mtu anayeumia kupita kiasi, hiyo migogoro itaweza kuharibu furaha iliyopo hivi sasa na kama mambo yakiendelea basi tutaona madudu mengi.

Tanzania Sports
Kila mtu anasema lake kwenye Twitter

Labda nilivyoelewa Mo hajaweka hizo bilioni 20 katika akaunti ya timu anajua kabisa kila mwaka itamenywa na Mamlaka ya mapato Tanzania endapo haijapangwa kitu gani cha kuifanyia mapema. Hivyo kuepusha yote hayo ndio maana jama ana nyuti.

Hayo mawazo yangu tu, lakini kama hakuna cha kuogopa kwanini asiziweke hizo fedha ili kila kitu kiende sawa na kusiwe na maneno juu ya jambo hilo.

Nikukumbushe tu kuwa sheria ya Tanzania katika uwekezaji wa vilabu unafanana kidogo na ule Wa Kijerumani kwani Wanachama (Members) wanatakiwa wamiliki 51% ya hisia huku 49% wanatakiwa wamiliki wawekezaji  zaidi ya mmoja wagawane.

Ila kwa Simba imekuwa tofuati mmiliki mmoja aliye na 49% ndiye anayetoa sauti kwa timu kutokana na kutofuata utaratibu.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Simba vs Yanga

Kejeli za Simba, Yanga Zinachosha

Simba

VPL: Simba ni Moto, Yanga Yapooza..