in

Kejeli za Simba, Yanga Zinachosha

Simba vs Yanga

Hivi visanga vinavyotoka katika soka la Tanzania havijawahi kutokea sehemu yoyote duniani.

Yanga na Simba hazijawahi  kuwa na timu imara zote kwa wakati mmoja tangu ligi kuu ya Tanzania Bara ilipoanza mwaka 1965.

Msimu huu inaonekana kabisa huenda timu hizi zina vikosi imara kila mmoja.

Yanga wamesajili nyota wengi wanaonekana ni washindani watakao leta chachu katika ligi, tofauti na ile ya msimu uliopita.

Lakini upande wa pili wa Simba unaonekana uko sawa kabisa hasa hawajafanya mabadiliko makubwa kutokana na ubora wa kikosi chao.

Baada ya yote hayo sasa kilichobaki kila upande unarusha  madongo kwa upande mwingine.

Popaganda za Yanga kwa Simba

Wanachokifanya kutibuliana kwa kuzusha mambo mbalimbali ili viongozi watibuane na wakose msimamo.

Uzee wa Onyango

Wapinzani  wanatumia fimbo hii ya kutania kuwa Joash Onyango ni mzee ili waweze kuchukua hisia za Simba na ikiwezekana hata mchezaji aingie hofu ili akose kuonesha kiwango chake halisi.

Kagere na Sven

Wanatumia njia ya ugomvi wa mchezaji Meddie Kagere na kocha wa Simba Sven ili uongozi upate kutetereka na waingize jambo lao ili wapate kupasua anga ya kufanikiwa.

Wakivurugana hawa basi kila kitu kitaenda kama vile wanavyotaka.

Mkude na Wawa

Kuna video inasmbaa mitandaoni inaonesha Mkude na Wawa wakisukumana basi wanatumia toboa hilo kuweka propaganda zao ili lengo litimie.

Kuondoka kwa Senzo

Pia hii ni kama fimbo ya kuiangamiza Simba juu ya mazira ya timu yao, inasemekana kuwa Senzo hakufurahishwa na uongozi wa Simba kwakuwa kila mmoja anajiona mjuaji.

Hii imemfanya aondoke na kutimkia Yanga  na inasemekana kabisa kuna umwinyi ndani yake hivyo sio kitu rahisi kwa Senzo kufanya kazi sehemu kama hiyo kwa weledi wake.

Milioni 20 za Mo

Kutokuweka wazi juu ya kuziweka milioni 20 za uwekezaji watu wengi wanatumia upande huo kuwapiga na kuwavuruga kabisa huku tajiri naye akileta jeuri akisema kuwa hivi kwa uwezo wake anashindwa kuweka milioni 20 ‘bank’.

Propaganda za Simba kwa Yanga

Yanga Simba
Yanga Simba

Hawa walianza wakati kocha hajafika waliongea sana huku wakitumia nyanja hiyo kuweka bayana kuwa kama watakuja kupoteza ligi itakapoanza basi wasiongee wameonewa bali kuchelewa kwa kocha.

Mabosi wa Yanga kuhonga waamuzi

Hii mpya kabisa huko mitandaoni kwa moto sana wanasema kuwa tayari makachelo wa Yanga wameanza kuhangaika kuwahonga mapema makocha na wakiweka wazi kuwa watakuwa macho kwa hilo.

Hii yote ni kujihami sidhani kama taasisi husikaa ikitaka ushahidi kama hawajapata basi watakuwa matatizoni wanaoendelea kusambaza habari hizi, lakini lengo lao kuharibu kabisa mambo wanayoyapanga Yanga.

Carlinhos kugoma kulala wawili

Utaratibu wa kulala wawili timu inapokuwa katika kambi upo kila sehemu hasa timu inapokuwa katika kambi,  lakini upande huu unatumia mwanya huo kusema kuwa nyota huyo kagoma ili wamvuruge na wawavuruge viongozi.

Nugaz na Bumbuli kusigana

Ushirikiano wao kikazi una maswali mengi
Wasemaji wa Yanga

Wamesema kuwa wasemaji wa Yanga Hassan Bumbuli na Antonio Juma Nugaz wamegombana ili watumie mwanya huo kuweka mtafaruku.

Kisinda kusaini miezi sita

Wanasema kuwa nyota huyu kasaini miezi sita na wao huenda wakamvizia kama walivyofanya kwa Morison.

Hapa hakuna kingine bali ni propaganda ili kuinyima timu hiyo ishughulikie kujibu mambo hayo wakistuka ligi imeanza na kupoteza michezo.

Mgogoro wa Hersi Said na Gharib

Hapa sasa ndio kabisa wameanza kusambaza kuwa mabosi hao wamegombana juu ya usajili wa nyota Tuisila Kisinda , Mukoko,  Carlinhos  na Sarpong.

Yote hayo yanafanyiika ili kuharibu timu hiyo katika kuendelea kuteka akili za viongozi ili watibuane

Yote hayo ili kuvurugana tu na kama zitaaingia akilini timu itayumba hakuna mbungi itakayoonekana uwanjani.

Mpira huu haujawahi kutokea duniani kote vijembe vinavyopigwa duniani sio hivi vya kuzushiana.

Hii inanipa raha mie kupenda kukaa Tanzania maana haijawahi kutokea hii katika soka.

Yote haya yanaweza kufanana endapo timu moja ikifanya vibaya katika mechi zake.

Yanga ambayo imesajili wachezaji wapya inatakiwa ipate ushindi angalau mechi tano huku Simba nayo inatakiwa itengeneze ushindi kama ilivyofanya msimu uliopita.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Msimu mpya

Tutarajie nini msimu mpya wa soka?

MO

Kigwangala, Mo Dewji Hapatoshi Twitter