in

Kariakoo Dabi: Jua chanzo, ukali wake

mchezo wa soka, mahasimu wakiwa uwanjani

Unapokaa katika vijiwe vya kahawa na kuzungumzia moja ya dabi kali sana barani afrika basi huwezi kuiacha kariakoo dabi ikihusisha mahasimu wawili Simba na Yanga, na inakadiriwa kushika nambari tano kwa mvuto barani afrika,ila hata katika ukanda wa afrika mashariki na kati mchezo huu huleta msisimiko kwa wapenzi wa soka.

Upinzani baina ya timu hizi mbili umechagizwa na masuala mbalimbali ikiwemo ya kisiasa na kihistoria, kwani mpira wa miguu nchini uliingia nchini miaka ya 1920 chini ya utawala wa waingereza

na wakoloni walianzisha ligi ya mkoa wa Dar Es Salaam na hakukuwa na timu ya wazawa iliyoshiriki ligi hiyo na baada ya miaka kadhaa kupita timu ya kwanza kushiriki ligi ya dar es salaam ilikuwa ni ‘new strong’ na baadae na baada ya miaka miwili kupita timu nyingine ya wazawa ‘new young’ iliundwa na kucheza msimu mmoja tuu ikashuka daraja.

kitendo hicho kiliwakera sana baadhi ya viongozi na kusababisha kwenda kuunda timu mpya yaani sunderland (Simba), pia upinzani wao ulikolea zaidi baada ya timu za wazawa kuungana kuunda chama chao cha soka na sunderland wakati wakaungana na timu ya warabu, Arab Sports ili kuzima ndoto za wazawa kuwa na chama chao basi Yanga waliona wenzao kama wasaliti..

Baadae upinzani uliahamia katika mataji huku kila timu ikimduwaza mwenzake kwa kutwaa taji la mkoa wa Dar es Saalam mara nne kila mmoja katika misimu nane

pia upinzani wa simba na yanga si tu ndani ya uwanja ,huku vitendo vya imani za kishirikina hutawala pindi timu hizi mbili zinapokaribia kuvaana, ni ngumu sana kuelezea hisia na mapenzi ya mashabiki wa timu hizi mbili muda mwingine huchukua maamuzi magumu timu yake inapopoteza ,huku tukio la mwaka 1974 shabiki mmoja aliingia katika tanuri moto huko tabora baada ya simba kupoteza kwa mabao 2-1
pia ndani ya uwanja kuna matukio yakukumbukwa zaidi ikiwemo ile ya mwaka 1984 kufunga goli ndani ya dakika 90, iliyovunjwa na juma kaseja katika ushindi wa magoli 5-0 mwaka 2012,

wakati ile ya yanga kutwaa taji la ligi kuu tanzania bara mara 27 , wakati ambapo rekodi ya abdalah kibadeni ya kupiga hat trick katika ushindi wa magoli 6 ikiishindwa kuvunjwa mpaka leo.

simba na yanga zinatarajia kukutana tena katika muendelezo wa ligi kuu tanzania bara huku mchezo wa mwisho uliopigwa januari 4 kila mmoja aliambulia alama 1 baada ya kutoka sare ya mabao ya 2-2

ikumbukwe katika michezo 100 waliokutana huku yanga 36 huku simba akishinda 28 na kutoka sare mara 36 huku yanga huku yanga akiwa na wastani wa kufunga magoli 121 na wekundu wa msimbazi wakiingia kambani mara 101

pia kuelekea mchezo wa marchi 8 katika vikosi vya timu zote mbili kuna wachezaji waliowahi kuzitumikia timu zote mbili kwa upande wa simba Hassan dilunga huku kwa upande wa yanga kuna mrisho ngassa ,abdulaziz makame na haruna niyonzima..

mchezo huu pia unaangaliwa katika thamani ya vikosi kwani simba inakadiliwa kufikia thamani ya bilioni moja huku kikosi cha yanga kikikadiliwa kufikia thamani ya milioni 700, lakini thamani ya vikosi haina nafasi kubwa katika kuamua matokeo.

mchezo wa marchi 8 utakuwa ni wa kwanza kwa mwalimu wa yanga luc eymael huku kwa upande wa van debroeck ukiwa mchezo wa pili baada ya kupata sare katika mchezo wa januari 4.

pia mpaka sasa simba yupo kileleni katika msimamo ya ligi kuu akiwa na alama 62 kibindoni katika michezo 24 huku yanga akiwa katika nafasi 4 akiwa na alama 41

ikumbukwe toka mwaka 2009 katika michezo 22 simba akishinda katika michezo 7 huku yanga akishinda michezo 6 na wakitoa sare michezo 9

mchezo huu unatarajiwa kutoa jasho na damu kutokana na kila timu kuwa na viungo maridadi na wabunifu huku kwa upande simba ikitumia viungo kama silaha kubwa ya ushindi ikiongozwa na cleatus chma ,lius miqqusoene,jonas mkude na hassani dilunga wakati kwa upande wa yanga wakijivunia mapinduzi balama,mohamed banka,haruna niyonzima na david morrison, daah yani hili timbwiki la eneo la kiungo sipati picha iyo marchi 8

Hakika tambo zishakuwa nyingi kuelekea kariakoo derby ila mwisho wa ubishi ni pale yanga atakapo mkaribisha simba marchi 8 , ni ndipo mbivu na mbichi zitazujulikana na zitaenda kwa wana jangwani ama msimbazii….

Unapokaa katika vijiwe vya kahawa na kuzungumzia moja ya dabi kali sana barani afrika basi huwezi kuiacha kariakoo dabi ikihusisha mahasimu wawili simba na yanga, na inakadiriwa kushika nambari tano kwa mvuto barani afrika ,ila hata katika ukanda wa afrika mashariki na kati mchezo huu huleta msisimiko kwa wapenzi wa soka

upinzani baina ya timu hizi mbili umechagizwa na masuala mbalimbali ikiwemo ya kisiasa na kihistoria ,kwani mpira wa miguu nchini uliingia nchini miaka ya 1920 chini ya utawala wa waingereza

na wakoloni walianzisha ligi ya mkoa wa dar es salaam na hakukuwa na timu ya wazawa ikiyoshiriki ligi hiyo na baada ya miaka kadhaa kupita timu ya kwanza kushiriki ligi ya dar es salaam ilikuwa ni new strong na baadae na baada ya miaka miwili kupita timu nyingine ya wazawa new young iliundwa na kucheza msimu mmoja tuu ikashuka daraja

kitendo hicho kiliwakera sana baadhi ya viongozi na kusababisha kwenda kuunda timu mpya yaani sunderland(simba),pia upinzani wao ulikolea zaidi baada ya timu za wazawa kuungana kuunda chama chao cha soka na sundrland wakati wakaungana na timu ya warabu Arab sports ili kuzima ndoto za wazawa kuwa na chama chao basi yanga waliona wenzao kama wasaliti..

baadae upinzani uliahamia katika mataji huku kila timu ikimduwaza mwenzake kwa kutwaa taji la mkoa wa dar es saalam mara nne kila mmoja katika misimu nane

pia upinzani wa simba na yanga si tu ndani ya uwanja ,huku vitendo vya imani za kishirikina hutawala pindi timu hizi mbili zinapokaribia kuvaana, ni ngumu sana kuelezea hisia na mapenzi ya mashabiki wa timu hizi mbili muda mwingine huchukua maamuzi magumu timu yake inapopoteza ,huku tukio la mwaka 1974 shabiki mmoja aliingia katika tanuri moto huko tabora baada ya simba kupoteza kwa mabao 2-1
pia ndani ya uwanja kuna matukio yakukumbukwa zaidi ikiwemo ile ya mwaka 1984 kufunga goli ndani ya dakika 90, iliyovunjwa na juma kaseja katika ushindi wa magoli 5-0 mwaka 2012,

wakati ile ya yanga kutwaa taji la ligi kuu tanzania bara mara 27 , wakati ambapo rekodi ya abdalah kibadeni ya kupiga hat trick katika ushindi wa magoli 6 ikiishindwa kuvunjwa mpka leo

simba na yanga zinatarajia kukutana tena katika muendelezo wa ligi kuu tanzania bara huku mchezo wa mwisho uliopigwa januari 4 kila mmoja aliambulia alama 1 baada ya kutoka sare ya mabao ya 2-2

ikumbukwe katika michezo 100 waliokutana huku yanga 36 huku simba akishinda 28 na kutoka sare mara 36 huku yanga huku yanga akiwa na wastani wa kufunga magoli 121 na wekundu wa msimbazi wakiingia kambani mara 101

pia kuelekea mchezo wa marchi 8 katika vikosi vya timu zote mbili kuna wachezaji waliowahi kuzitumikia timu zote mbili kwa upande wa simba Hassan dilunga huku kwa upande wa yanga kuna mrisho ngassa ,abdulaziz makame na haruna niyonzima..

mchezo huu pia unaangaliwa katika thamani ya vikosi kwani simba inakadiliwa kufikia thamani ya bilioni moja huku kikosi cha yanga kikikadiliwa kufikia thamani ya milioni 700, lakini thamani ya vikosi haina nafasi kubwa katika kuamua matokeo

mchezo wa marchi 8 utakuwa ni wa kwanza kwa mwalimu wa yanga luc eymael huku kwa upande wa van debroeck ukiwa mchezo wa pili baada ya kupata sare katika mchezo wa januari 4

pia mpaka sasa simba yupo kileleni katika msimamo ya ligi kuu akiwa na alama 62 kibindoni katika michezo 24 huku yanga akiwa katika nafasi 4 akiwa na alama 41

ikumbukwe toka mwaka 2009 katika michezo 22 simba akishinda katika michezo 7 huku yanga akishinda michezo 6 na wakitoa sare michezo 9

mchezo huu unatarajiwa kutoa jasho na damu kutokana na kila timu kuwa na viungo maridadi na wabunifu huku kwa upande simba ikitumia viungo kama silaha kubwa ya ushindi ikiongozwa na cleatus chma ,lius miqqusoene,jonas mkude na hassani dilunga wakati kwa upande wa yanga wakijivunia mapinduzi balama,mohamed banka,haruna niyonzima na david morrison, daah yani hili timbwiki la eneo la kiungo sipati picha iyo marchi 8

Hakika tambo zishakuwa nyingi kuelekea kariakoo derby ila mwisho wa ubishi ni pale yanga atakapo mkaribisha simba marchi 8, ni ndipo mbivu na mbichi zitazujulikana na zitaenda kwa wana jangwani ama msimbazii….

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Corona inavyoharibu utamu wa michezo

Tanzania Sports

Watford wamewazuia ‘Liver’ kuifikia rekodi ya Arsenal