in , , , ,

JIPYA GANI KEN GOLD ITAKUJA NALO LIGI KUU?

Hivi karibuni klabu ya KEN GOLD kutoka katika jiji la Mbeya imekuwa ni klabu ya kwanza kutoka katika ligi ya Championship kufuzu na hatimaye kuingia katika ligi kuu ya Tanzania bara kwa msimu huu. Walifanya hivyo baada ya kuifunga klabu ya FGA talents ya Songea. Katika mwanzo wa msimu klabu ya FGA talents makazi yake yalikuwa mjini Morogoro lakini ikahamia mjini Songea katika mechi za katikati ya mzunguko wa pili wa ligi ya Championship league. Huo ulikuwa ni mchezo wa 29 wa ligi ya Championship. Klabu ya Ken Gold makazi yake yapo katika wilaya ya Chunya lakini katika kucheza mechi zake za nyumbani imekuwa inatumia uwanja wa Sokoine ambao upo Mbeya mjini.

Ken Gold ni timu ambayo inamilikiwa na watu binafsi na sio timu ya umma wala ya taasisi. Imeingia ligi kuu baada ya kukaa kwenye ligi ya Championship kwa misimu kadhaa. Inamilikiwa na mmiliki mmoha ambaye ana miliki pia shule za Ken Gold pre and primary schools ambazo zipo Chunya. Ushindi wa mabao 2 kwa sifuri ambao uliiupata mnamo tarehe 2 Aprili mwaka huu wa 2024 ulihakikishia timu hiyo kucheza katika ligi kuu ya Tanzania. Kupanda huko kutaongeza chachu ya soka ambayo mashabiki wa Mbeya walikuwa wameshaanza kuipoteza baada ya vilabu vya Mbeya kwanza na Mbeya City kushushwa daraja katika misimu iliyopita baada ya kushindwa kufanya vizuri na hatimaye kupoteza nafasi za kuendelea kuwa katika ligi kuu na hivyo kujikuta vimeteremshwa daraja. Imeingia ligi kuu kwa jumla ya pointi 67 ambazo ni pointi ambazo zimewahakikishia wao kupanda ligi kuu. Wamepanda ligi kuu huku wakiwa wana mchezo mkononi ambapo katika mchezo wa tarehe 28 mwezi wa nne wamewaambia mashabiki wao kwamba wajitokeze kwa wingi kwenda kushuhudia mchezo wao ambao ndio watakapokabidhiwa kombe la ligi ya Championship. Taarifa waliyoitoa kwa umma inasema kwamba tiketi 1000 za mashabiki kuangalia pambano hilo tayari zimeshalipiwa na mkurugenzi wa klabu hiyo.

Sio jambo la kushangaza kuona klabu ya kutoka maeneo ya Chunya mkoani Mbeya kufanikiwa kuingia ligi kuu kwanza kwa wanaofahamu wanatambua kwamba mkoa huo una historia kubwa ya mwamko katika mchezo wa soka.kwani kwa msimu huu tu ulikuwa una vilabu viwili ambavyo ni timu ya Prisons pamoja na timu ya Ihefu ambayo makazi yake yalikuwa ni Mbarali. Ihefu ilirudi msimu uliopita katika ligi kuu baada ya kushuka daraja katika msimu uliokuwa umetangulia. Kwa sasa klabu ya Ihefu tayari imeshauzwa na tayari imeshahama mkoa na kwa sasa iko mkoani Singida na sababu za kuuzwa huko bado haijawekwa wazi. Kuuzwa kwa klabu ya Ihefu umekufanya mkoa wa Mbeya kubaki na klabu moja tu katika ligi kuu ambayo ni klabu ya Prisons ambayo inamilikiwa na jeshi la magereza.

Ken Gold imefuzu kuingia ligi kuu baada ya misimu kadhaa kucheza katika ligi ya Championship ambapo hapo awali walikuwa wamesajili baadhi ya wakongwe wa ligi kuu kwa ajili ya kucheza katika timu yao lakini hawakufanikiwa huko awali bali wamefanikiwa mwaka huu.  Takwimu zinaonyesha kwamba vilabu ambavyo vimekuwa vinafuzu kuingia katika ligi kuu bara baadhi yao hushindwa kuhimili mikiki ya ligi kuu na vimekuwa vinajikuta vinarudishwa katika ligi za chini na baadhi yao kupotea kabisa. Tumeshuhudia vilabu kama Lipuli, Stand United, Alliance FC, Mbao FC na vinginevyo vilipanda ligi kuu kwa nguvu kubwa na toka vishuke daraja havijawahi kuweza kurudi tena katika ligi kuu bara. Vilabu hivyo vimeshindwa kurudi ligi kuu na pia vimeshindwa kabisa hata kubaki katika ligi ya championship kwani vimeshuka mpaka madaraja ya chini ikiwemo daraja la  daraja la pili.

maswali makubwa ambayo klabu ya Ken gold itaulizwa yako mengi ila kuna baadhi ambayo ndio ya msingi kama wachambuzi wa michezo tunapaswa kujiuliza. Na maswali yenyewe ni kama yafuatayo:

  1. Je itaweza kuwa na nembo kubwa ya kibiashara na idadi kubwa ya mashabiki ambapo wataweza kuvutia wadhamini katika klabu hiyo?. Tumeshuhudia vilabu ambavyo vimeingia katika ligi ya Tanzania bara vingi vimeshindwa kuwa na nembo kubwa ya kibiashara na hatimaye vimeshindwa kuvutia wadhamini na wawekezaji katika vilabu hivyo. Mbeya kwanza msimu wake ambao uliingia katika ligi kuu ilishindwa kushawishi wadhamini wapya na ilijikuta imebakia na hali ngumu ya kuweza kujiendesha kwenye ushindani wa ligi kuu na hatimaye ikashuka daraja na kurudi daraja la kwanza.
  2. Je itaweza kutokufuata mkumbo wa kusajili wachezaji wa kimataifa na badala yake kutumia Zaidi wa ndani?. Tumeshuhudia vilabu kama Tabora United ilinunua wachezaji wengi wa kutoka nje ya nchi na wachezaji hao wakashindwa kutoa huduma kwa kiwango kile ambacho mabosi wa timu hiyo walitarajia wangekipata na hatimaye kujikuta klabu hiyo inavunja mikataba na wachezaji hao ambayo ilikuja kuwagharimu kiasi kikubwa cha pesa vilabu hivyo.
  3. Je itaheshimu mikataba ya benchi la ufundi ambalo limeipandisha daraja klabu hiyo? Je itaweza kuendelea na mikataba ya ajira ya benchi la ufundi walioipandisha timu hiyo daraja ama itaipuuza na kisha kuachana na benchi hilo na kuamua kuchukua makocha wapya?. Tumeshuhudia klabu kama Mashujaa wa lake Tanganyika pindi ilipopanda daraja ilitimua benchi lake la ufundi ambalo lilikuwa linaongozwa na kocha mzoefu Meja mstaafu Abdul Mingange na kuamua kumchukua kocha Abdallah Mohammed ama maarufu Baresi.
  4. Je itaheshimu mikataba ya wachezaji wake na haitawafukuza ovyo? Je klabu hiyo itaheshimu mikataba ya wachezaji wake na kutoamua kuwatimua ovyo. Tumeshuhudia vilabu kama Singida Fountain Gate na Tabora United vimekuwa inatimua ovyo wachezaji wake bila ya kufuata taratibu za kisoka na hatimaye vikajikuta vinapelekwa kushitakiwa FIFA na hatimaye vinatakiwa vilipe fidia na madai ya wachezaji hao na hatimaye kuviathiri kiuchumi.

Majibu ya maswali haya na mengineo mengi msomaji wangu kwa sasa hayatakuwepo ila kama wazungu wanavyosema “time will tell” muda utaongea basi siku za usoni tutapata majibu ya maswali hayo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

52 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

ALPHONCE SIMBU SHUJAA ASIYEIMBWA KWENYE MICHEZO

Tanzania Sports

FAIDA NA HASARA KWENYE BIASHARA YA MICHEZO ..