in , ,

Jinsi kocha wa Yanga alivyoaibishwa kimbinu

WAKATI Yanga ya jijini Dar Es Salaam ikikumbana na kipigo mabao 2-0 toka kwa A Hilal ya Sudan wakiwa nyumbani kwenye dimba la Benjamini Mkapa, wapinzani wao wengine TP Mazembe na MC Algers zilitoshana nguvu kwa kutoka suluhu 0-0. Kwa matokeo hayo Yanga wanaburuza mkia katika kundi lao wakiwa hawana pointi, huku Al Hilal wakiongoza kundi hilo kwa pointi 3. Kipigo hicho ni cha kwanza kutoka kwa kocha Sead Ramovic ambaye amechukua nafasi ya kocha Miguel Gamondi aliyetupiwa virago hivi karibuni. TANZANIASPORTS inafanya uchambuzi yakinifu kuhusiana na mchezo huo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa vijana hao wa Jangwani na Twiga

Aibu ya kwanza ya kocha Ramovic

Kocha wa Yanga aliingia katika mfumo wake na kuipanga timu kwa uono wake ikiwa na mabeki wawili nyuma huku mbele yao kukiwa na viungo watatu wanaotokana na mabeki wa pembeni, kisha wachezaji waliobaki walikuw ana jukumu la kudhibiti eneo la katikati kuelekea langoni mwa adui. Kwa maelezo hayo timu hiyo ilikuwa mfumo wa 2-3-4-1. Katika kujibu mapigo Kocha wa A Hilal, Ibenge aliwapanga wachezaji wake katika mfumo wa 4-1-3-2, kwa maana alijilinda kwa wachezaji watano kamili kisha watatu walitumika kutuliza kasi ya mchezo (tempo) huku w awili wakiwa katika mshambulizi ya kushtukiza. Mkakati wa kwanza wa Al Hilal ulionekana baya pale ambapo alitafuta suluhu katika dakika 45 za kwanza. Hadi filimbi ya mwamuzi ilipopuliza, sio Yanga wala Al Hilal iliyofanikiwa kuliona lango la mwenzake.

Tisa dhidi ya aibu ya pili

Kocha wa Yanga Sead Ramovic aliingia kipindi cha pili akiwa na mkakati uleule wa kusukuma zaidi mashambulizi. Bado aliendelea kutumia mabeki wawili yaani Ibrahim Bacca na Dickson Job. Wakati kocha wa Yanga akiendeleza kufikiria kushambulia bila kuimarisha ulinzi alijikuta katika wakati mgumu baada ya mashambulizi ya kushtukiza ya Al Hilal yalivyomuaibisha. Katika mfumo wa mabeki wawili maana yake beki wa tatu wa katikati ambaye ni kiungo namba sita anakuwa mbele kidogo ya eneo la 18. 

Kwa maana Bacca na Job wanajikuta wakiwa peke yao nyuma katika mgawanyo wa mmoja kwenda kulia na mwingine kwenda kushoto. Kwa kawaida mgawanyo kama huo unaacha pengo katika eneo lao la katikati kama namba sita hana uwezo wa kurudi haraka eneo hilo na kuongeza nguvu kwenye ulinzi. Bao la kwanza la Al Hilal limepitia upande wa kushoto wa Yanga kwa shambulizi la kushtukiza. Baaca alijikuta akiwa peke yake licha ya kuhitaji msaada. Katika mfumo huo ni rahisi kumsogelea golikipa ndiyo maana shambulizi moja ya kushtukiza liliwafikisha langoni mwa Ynaga kirahisi mno. 

Sababu ilikuwa wachezjai 9 wa Al Hilal walikuwa katika eneo lao la ulinzi, na hivyo viungo walikuwa na jukumu la kupiga mipira mirefu. Bao la pili lilipatikana kwa mtindo uleule wa shambulizi la kushtukiza, mpira mrefu ulipigwa kueleka kushoto mwa Al Hilal ambako ni kulia mwa Yanga alikokuwa Dickson Job. Wakati Dickson Job akitimiza jukumu lake ya kwenda kukabiliana na mshambuliaji wa Al Hilal, eneo aliloondoka lilikuwa wazi, kwani viungo wa eneo la ukabaji hawakurudi haraka kutokana na mfumo kuwabana. 

Hata Bacca alipojaribu kuingia eneo la katikati kwenye 18 alikuwa ameshachelewa kwani mshambuliaji wa Al Hilal alikwishaingia eneo la hatari mita chache kutoka alipokuwa golikipa kisha akatumbukiza wavuni bao hilo. Kimfumo Yanga walivurugwa kwa kiasi kikubwa kwa sababu hapakuwa na uwiano kati ya kushambulia na kujilinda. Kwa kuona makosa yake kocha Sead Ramovic akamwingiza Kibwana Shomari ili kusaidia ulinzi. 

Ufahamu mdogo kuhusu Al Hilal

Tanzania Sports

Uchezaji wa Al Hilal ya Ibenge unbafahamika kuwa ni ule ambao unacheza kwa taswira mbili. Taswira ya kwanza ni kupunguza makali ya wapinzani wao, kuwafanya wakose nafasi za kufunga na wasiweze kupata bao lolote mchezoni. Taswira ya pili ni mfumo wa kucheza kwa mashambulizi ya kushtukiza. Wachezaji 8 hadi 9 wanapokaa eneo lao kujilinda maana yake wanategemea kucheza kwa ‘counter attacks’. 

Mwalimu wa Yanga alipaswa kuambiwa hili mapema kwa sababu AL Hilal wamecheza hivi mara nyingi hata kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kwenye mashindano mbalimbali au mechi za kirafiki. Al Hilal kwa kutambua kuwa kocha wa Yanga hajawafahamu vema nguvu yao ilipo ndipo walimpunguzia majukumu Mohamed Abdelrahman ambaye ni nahodha na mshambuliaji wa kutumainiwa wa timu kwa kumtoa nje. 

Wachezaji walioingia kipindi cha pili ni aina ya wachezaji wenye kutafuta ushindi kwa kushtukiza kisha kuwaacha wapinzani wakiwa hawana la kufanya. Kocha wa Yanga aliaibishwa kwa sababu mbinu zake hazikuwa za kusaka ushindi kwa uwiano wa kujilinda. Kucheza mabeki wawili maana yake unawatuma kazi mabeki wa pembeni waungane na viungo wao kujazana langoni mwa adui.. lakini swali linakuja safu ya ulinzi katika mashindano hayo inawezaje kubakiwa na wachezaji wawili tena ukicheza dhidi ya wazoefu wa mashindano ya Kimataifa?

Mabadiliko yasiyo ya kimbinu

Mwalimu wa Yanga aligundua makosa yake hivyo alitaka kuimarisha safu ya kiungo ili iweze kulinda eneo lao kwa kumtoa Dube  Abuya, lakini akachanganyikiwa zaidi pale alipomtoa Max Nzengeli wa eneo hilo. Mwalimu alishindwa kubadili mfumo wa kucheza badala yake akawatoa wachezaji mhanga kana kwamba hawafanyi kazi yake vizuri. Viungo wawili kwa wakati mmoja huku timu haijafunga bao lolote ulikuwa uwezo wa juu wa ubabashaji. Eneo la ushambuliaji mwalimu alimwingiza Kennedy Musonda maybe ametoka kuwa miongoni mwa wafungaji bora wa hatua ya kufuzu AFCON. 

Silaha kama hii haikuppaswa kuwekwa benchi badala yake ingetafutiw anafasi tangu mwanzo. Kwa mfano, alipingia Musonda mfumo wa ushambuliaji ulikuwa na washambuliaji Prince Dube na Musonda ikiwa na maana anacheza na katika mfumo wa ‘diamond’ 4-4-2, lakini haikuwa hivyo. Yanga walijikuta wameongeza mshambuliaji badala ya mbunifu. Tukumbuke Yanga walihitaji winga au mchezaji mwenye kasi ya kuwapangua mabeki wa Al Hilal, kwa maana Cletous Chama alihitaji mtu wa pili mwenye kasi kueleka eneo la 18. Hata hivyo mabadiliko ya mwalimu hayakuwa na kimbinu bali kuingia wachezaji wakatumikie mfumo ambao unamfelisha pakubwa.

Yanga bila vipimo vya mchezo

Yanga walicheza mechi yao ya mwisho Novemba 7. Kwa siku 19 wamecheza mazoezi peke bila kuwa na mechi ya kujipima nguvu. Kocha alikuwa akifundisha wachezaji kisha akaenda kujaribu mbinu zake kwenye mchezo wa mashindano. Katika kuweka mambo sawa kwa mbinu zake mwalimu alipaswa kuomba mchezo wa kurafiki ili kuzipima uzito na ubora wa mbili zake mpya. Hadi dakika 90 unagundua kuwa mfumo unaotumika hauna vionjo vya nyongeza ambavyo vinaweza kuongeza kitu katika vipaji vikubwa vya wachezaji wa Yanga. Kifupi hata wachezaji wa Yanga wamemzidi kocha wao mpya kwa mbali mno wasifu na uzoefu wa mashindano ya kimataifa.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

24 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tony Yeboah

Ghana inapoteza kizazi chake cha dhahabu?

Tanzania Sports

Yanga Walifeli Kwenye Usajili au Benchi la Ufundi?