in , , ,

Jezi za England hazishikiki

*Sunderland wapigwa tena

Wadau wa soka wamekitupia lawama Chama cha Soka (FA) cha England kwa bei mbaya ya jezi za Timu ya Taifa – Three Lions.

Fulana hizo zitakazotumika kwenye fainali ya Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka huu zimeanza kuuzwa kwa bei mbaya ya pauni 90, yaani karibu Sh 250,000 za Tanzania.

Waziri Kivuli wa Michezo, Clive Efford amesema mkakati wa bei hiyo unasikitisha na kukatisha tamaa wadau wa soka wakati kiungo wa klabu ya Queens Park Rangers (QPR), Joey Barton amesema inaogofya kuona mwenendo wa namna hiyo.

FA imejaribu kujiweka kando kuhusiana na bei, kikirusha mpira kwa watengenezaji ambao ni Nike wanaosema kwamba bei hiyo ya juu ni kwa jezi zilizoandaliwa kukabiliana na hali ya hewa ya joto ya wakati huo, lakini kwamba kuna nyingine za bei ya pauni 60 wakati jezi kwa ajili ya watoto wenye umri kuanzia miaka minane hadi 15 bei yake ni pauni 42.

“Nimechukizwa sana eti washabiki watoe hadi pauni 90 kwa ajili ya kununua jezi mpya za England. Naona sasa watu wa soka wanajielekeza zaidi kwenye biashara na kuchuma faida badala ya kuangalia jumuiya yetu na washabiki na hali zao, watu ambao wamesaidia kuendeleza soka kwa vizazi vingi,” alilalamika waziri huyo kivuli.

England wanakwenda Brazil chini ya Kocha Roy Hodgson lakini hawana matumaini makubwa ya kusonga mbele kwenye hatua za mbali, kwa sababu ya aina ya wachezaji walio nao wakilinganishwa na timu nyingine.
 
SUNDERLAND SIKIO LA KUFA

Timu ya Sunderland iliyo katika hatari ya kushuka daraja imewakaribisha West Ham nyumbani kwake na kuambulia kichapo cha mabao 2-1.

Sunderland wanaofundishwa na Gus Poyet walishalala kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Andy Carroll dakika ya tisa na Mohamed Diame dakika ya 50 kabla ya Sundrland kuanza jihad na kufanikiwa kuchomoa moja dakika ya 60 kupitia kwa Adam Johnson.

Dakika za mwisho zilikuwa ngumu kwa West Ham kwa jinsi Sunderland walivyoshambulia mfululizo hadi kipa wake Vito Mannone aliyetoka Arsenal akawa akipanda hadi langoni mwa adui zao kwa ajili ya kutafuta bao la kusawazisha bila mafanikio.

Sunderland wamecheza mechi 30 , wana pointi 25, wakiwa juu ya Fulham tu ambao wamecheza mechi 32 na kujikusanyia pointi 24. Cardiff wamcheza mechi 32 pia na wana pointi 26 wkati West Bromwich Albion ni wa nne kutoka mkiani, wamecheza mechi 31 na wana pointi 29, hivyo Sunderland wanachotakiwa kufanya ni kushinda mechi zao za mkononi ili wajinasue walau kidogo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Al Ahly watupwa nje

Mourinho: Nahitaji mshambuliaji wa kweli