in , , ,

HIZI NDIZO SABABU ZILIZOIBEBA CHELSEA MSIMU HUU

1: UCHACHE WA MASHINDANO.

Chelsea hawakuwa na mashindano mengi ukilinganisha na wapinzani wake
kwenye ligi . Hali iliyosababisha wao kuwa na muda mwingi wa kupumzika
ukilinganisha na timu zingine pinzani kwake. Mfano hawakuwa
wanashiriki UEFA au EUROPA kitu ambacho kilisababisha wao kutokucheza
katikati ya ligi hivo kuwa na nafasi kwao kupumzika na kutokuwa na
uchovu mkubwa.

2: INGIZO LA MOSES, MARCUS ALONSO NA PEDRO.

Hawakuwa na msimu mzuri sana kabla ya msimu huu, na nafasi yao katika
kikosi cha Chelsea kabla ya msimu huu ilikuwa inaonekana finyu sana.
Lakini tofauti na matazamio ya wengi , Alonso, Moses na Pedro wamekuwa
moja ya mihimili ya Chelsea kuchukua ubingwa msimu huu.
Inawezekana msiba wa mama yake Willian ndiyo ulimfanya Moses kuzaliwa
upya na kupata nafasi ambayo aliitimiza. Moses na Alonso wamecheza
vizuri kama Wingbacks na wamekuwa wakileta uwiano mzuri wa kati ya
mashambulizi na kuzuia upande wa kulia na kushoto mwa uwanja. Mijongeo
ya mashambulizi ilikuwa imara kwa pande zote mbili ndiyo maana Alonso
alihusika kwenye magoli vivyo hivo kwa Moses.

3: INGIZO LA NG’OLO KANTE

Msimu wa mwisho kwa Chelsea kubeba kombe walikuwa imara kwenye kiungo
kwa sababu walikuwa na Fabregas na Matic, lakini msimu uliofuata
viungo hawa walikuwa na uchovu mkubwa kitu kilichosababisha wao
kutokuwa na msimu mzuri. Msimu huu baada ya kumleta Kante kiliongeza
vitu viwili kwa Chelsea, cha kwanza ni uimara wa ulinzi wa nafasi ya
kiungo cha Chelsea, pili ni kumpa nafasi Matic acheze kama box to box
Middfielder kitu ambacho kilikuwa na faida kubwa sana kwani Matic
alikuwa na uwezo mkubwa wa kukaba na kupandisha timu. Huwezi zungumzia
mijongeo ya kina Moses na Alonso bila kusahau kumtaja Kante kwa sababu
Kante ndiye aliyekuwa anaratibu mijongee ya hawa watu.

4: MFUMO WA 3-4-3

Baada ya kuanza michezo sita (6) akiwa anatumia mabeki watatu, Conte
aliamua kubadili uwelekeo na hii ilikuja mara baada ya kufungwa na
Arsenal goli 3-0. Mfumo huu ndiyo ulikuwa mhimili wa mafanikio ya
Chelsea msimu huu.


5:UWEPO WA HAZARD NA MAGOLI YA COSTA
.

N’Golo Kanté, Eden Hazard na Thibaut Courtois.

Haikutakiwa Chelsea kujivunia mfumo wa 3-4-3 kwa sababu ulikuwa
unawafanya wawe imara katika eneo la ulinzi . Lakini kuna watu
walihitajika zaidi ili kukamilisha uimara wa mfumo huu.

Mtu wa kwanza ni mchezaji ambaye anatakiwa acheze kama mchezaji huru
na afurahie kucheza katika eneo hilo huru. Hazard ndiye aliyekamilisha
jukumu hili kwake. Alicheza huru na alitimiza majukumu yake ipasavyo.
Ubunifu wa mashambulizi ya Chelsea ulikuwa unatengenezwa na Hazard.

Mtu wa pili aliyehitajika ni mtu ambaye ana uwezo mkubwa wa kufunga.
Chelsea ilihitaji mshambulizi ambaye ana uwezo wa kufunga goli 20 kwa
msimu. Costa alifanya kitu ambacho alitakiwa kukifanya na kizuri zaidi
ni kwamba alikuwa anafunga magoli muhimu. Kuna wakati Chelsea walianza
kupata ushindi finyu kama wa goli 1-0, 2-1 kwenye ushindi kama huu
Costa alihusika sana kwenye ufungaji.

6:MAHUSIANO KATI YA CONTE NA CHELSEA.

Taswira iliyokuwa inakuja mbele yangu kila nilipokuwa namwangalia
Conte ilikuwa inajidhihirisha kwa ukubwa kuwa Conte na wachezaji wake
walikuwa na mahusiano imara, uimara ambao ulijenga imani kati yao
wawili hivo kuwa na uwezo wa kupigana kwa nguvu bila kumwangusha
mwenzake.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

HILI LA UWANJA, TFF INAZIDI KUCHANA NGUO ZAKE ILI TUONE NYETI ZAKE

Tanzania Sports

HONGERA YANGA, UBINGWA UWE MAWANI YA KUONA PAKUBWA